Kaka Yaoh
Senior Member
- Sep 23, 2021
- 190
- 361
Hipo hivi,
Jumapili hii niliandaa tafrija nikaalika ndugu na marafiki zangu wa karibu waje kujumuika na mimi kwenye hii nyumba yangu mpya ambayo hipo nje kidogo ya mji wakati tafrija hii ikiendelea nikaona isiwe tabu kufungua mlango ili yeyote atakayetaka kujumuika na sisi basi nae akaribie lakini kwa mshangao hakuna aliyekuja kabisa.
Leo narudi zangu mtaani jioni baada ya mizunguko ya hapa na pale nakuta njiani kuna shimo kubwa ambalo kwa haraka nikatambua kuwa kuna bomba limekatika kwahiyo njia ya kuingilia kwangu haipitiki, hivyo nimelazimika kupaki gari kwenye maegesho ya karibu na kunifanya nitembee kwa mguu mpaka kwangu.
Nimeenda kwa balozi wa nyumba kumi kutoa malalamiko yangu juu ya kufungwa kwa barabara bila ya Mimi kama mkazi wa mtaa huu kupewa taarifa yoyote ile, balozi nae kanipa jibu kuwa atalishughulikia hili suala mpaka saa hizi yamepita masaa matatu hakuna feedback.