Kwanini jirani zangu hawanichangamkii?

Kwanini jirani zangu hawanichangamkii?

Epuka mambo ya kiswahili kiswahili,hukuwapa heshima ya kutosha ndo maana hawakuja kama mke wako ni mtu wa watu ungepsta hata mashosti zake wangekuja,kiufupi mnafanana kitabia wewe na mke wako huenda SI watu wa kushinda Sana nyumbani ama mke wako anajifungia ndani muda wote,jufunze kusocialize na watu vingivevyo hao hao majirani watakuhujumu hasa kupitia mabeki 3
 
Epuka mambo ya kiswahili kiswahili,hukuwapa heshima ya kutosha ndo maana hawakuja kama mke wako ni mtu wa watu ungepsta hata mashosti zake wangekuja,kiufupi mnafanana kitabia wewe na mke wako huenda SI watu wa kushinda Sana nyumbani ama mke wako anajifungia ndani muda wote,jufunze kusocialize na watu vingivevyo hao hao majirani watakuhujumu hasa kupitia mabeki
 
Katika kosa utafanya kwenye haya maisha ni kujenga mazingira ambayo wale wanaokuzunguka ni watu wa status tofauti na wewe.

Utakutana na kila aina ya Drama ukiwa unaendelea kuishi hapo mahali. Unapoishi na watu umewazidi maisha hata kidogo, basi automatically wataanza kukutengenezea mizengwe ambayo wanafanya kusudi ili kukuonyesha tu kuwa hawaridhiki wewe kuwazidi.

Nakumbuka kuna mtaa niliwahi kuishi, tukaitisha kikao cha ulinzi. Watu wakawa wanapendekeza watafutwe walinzi wa kupiga patrol na kulinda mitaa kuanzia jioni hadi asubuhi. Ila baadhi ya washiriki wa kikao wakapinga hilo wazo kuwa hawawezi kuingia gharama ya kuchangia ulinzi wakati wao hawana magari wala mali za kuibiwa nje.

Kuna situation nyingine ilikuwa ni mtaani barabara iliharibika baada ya mvua kubwa kunyesha. Kukawepo mjadala wa kuchangishana kuleta kifusi na katapila kusawazisha hiyo barabara, watu wakarudia hoja ile ile, kuwa wao hawana magari so hawaoni umuhimu wa kuchangia.

Kilichotokea sasa, wale washiriki waliopendekeza walikodi kampuni ya ulinzi ambayo wakachukua kila muhusika mlinzi wake. Na wakachanga wakaleta kifusi wakajaza maeneo yao ambayo yamechimbika. Wakaachana na maswala ya barabara nzima.

Sasa hii inakupa picha gani kuhusu kuishi na watu usiofanana nao status ya kimaisha.
 
We jamaa yani uache geti wazi ili waje kama vile mbwa koko.

Binafsi hua siendi sehemu kama sijaalikwa
 
Ishi na watu vizuri nyumba yako itashika moto ukiwa kazini na hawatafanya kitu.

Mimi nilipohamia huku nikitoka asubuhi simpiti mtu bila kumsalimia. Nikifika kwa mama wa vitumbua napunguza mwendo "habari za saivi jirani zangu" halafu nawaungisha vitumbua nakuja navyo kazini.

Vijiwe vyote nawasalimia hadi vijiwe vya boda boda nikipita napiga horn Piii, afu nawapungia na wao wanajibu piii piii piii piii. Daah raha sana.

Sichangamani nao kupiga umbea ila nashiriki nao matukio. Msiba ukitokea nitatoka kazini mapema nitaenda msibani. Sherehe zao nachangia na ninaenda.

Acha kuringa .
Vizuri Madame [emoji120][emoji120][emoji120]
 
Hipo hivi,

Jumapili hii niliandaa tafrija nikaalika ndugu na marafiki zangu wa karibu waje kujumuika na mimi kwenye hii nyumba yangu mpya ambayo hipo nje kidogo ya mji wakati tafrija hii ikiendelea nikaona isiwe tabu kufungua mlango ili yeyote atakayetaka kujumuika na sisi basi nae akaribie lakini kwa mshangao hakuna aliyekuja kabisa.

Leo narudi zangu mtaani jioni baada ya mizunguko ya hapa na pale nakuta njiani kuna shimo kubwa ambalo kwa haraka nikatambua kuwa kuna bomba limekatika kwahiyo njia ya kuingilia kwangu haipitiki, hivyo nimelazimika kupaki gari kwenye maegesho ya karibu na kunifanya nitembee kwa mguu mpaka kwangu.

Nimeenda kwa balozi wa nyumba kumi kutoa malalamiko yangu juu ya kufungwa kwa barabara bila ya Mimi kama mkazi wa mtaa huu kupewa taarifa yoyote ile, balozi nae kanipa jibu kuwa atalishughulikia hili suala mpaka saa hizi yamepita masaa matatu hakuna feedback.
Ww si mzima
 
Back
Top Bottom