Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Wewe ulishaingia mageti mangapi yaliyoachwa wazi kwenye sherehe za watu usiowajua ?
MkuuHipo hivi,
Jumapili hii niliandaa tafrija nikaalika ndugu na marafiki zangu wa karibu waje kujumuika na mimi kwenye hii nyumba yangu mpya ambayo hipo nje kidogo ya mji wakati tafrija hii ikiendelea nikaona isiwe tabu kufungua mlango ili yeyote atakayetaka kujumuika na sisi basi nae akaribie lakini kwa mshangao hakuna aliyekuja kabisa.
Leo narudi zangu mtaani jioni baada ya mizunguko ya hapa na pale nakuta njiani kuna shimo kubwa ambalo kwa haraka nikatambua kuwa kuna bomba limekatika kwahiyo njia ya kuingilia kwangu haipitiki, hivyo nimelazimika kupaki gari kwenye maegesho ya karibu na kunifanya nitembee kwa mguu mpaka kwangu.
Nimeenda kwa balozi wa nyumba kumi kutoa malalamiko yangu juu ya kufungwa kwa barabara bila ya Mimi kama mkazi wa mtaa huu kupewa taarifa yoyote ile, balozi nae kanipa jibu kuwa atalishughulikia hili suala mpaka saa hizi yamepita masaa matatu hakuna feedback.
Ndugu yetu anawapeleka mchaka mchaka jirani zake halafu anataka wamchangamkieHata ingekua mimi jirani siji
Ushawahi ona wapi mtu anaingia ukumbini tu kwenye harusi kisa ukumbi uko karibu na kwake?
Mwaliko lazima mkuu especially kwenye sherehe ingekua msiba kweli
Anajikuta kanye West🤣🤣🤣🤣🤣🤣Ndugu yetu anawapeleka mchaka mchaka jirani zake halafu anataka wamchangamkie
Halafu wamemchimbia gap karibu na geti lake🤣🤣Jishushe, take it easy mzee baba. Kwa maelezo yako unaonekana umecreate gap kati yako na jamii inayokuzunguka, socialize na majirani na jamii ya hapo mtaani kwako.
Sasa mtoa mada anawachukulia hao majirani kama panya,ameacha tu mlango wazi akitegemea mtu from no where aone geti liko wazi aingie.Hapana
Umeingia kwa nyodo za kishamba mtaa utakushinda
Kwa maelezo haya, wewe ni ile aina ya majirani wanoko.nimejifunza jambo , kujenga nyumba unafanya sherehe je ungefanya mradi mkubwa si ungefuga mtaa,nina jirani zangu hapa mmoja ni mchaga dah huyu ni mshamba sana aliponunua kiwanja akawa analeta rafiki zake kuwaonyesha, mke wake mashauzi kweli mara wapige picha kwenye kiwanja, alipoanza kujenga nasikia akawa anatamba ntajenga nyumba ya moto mtaa mzima, alichojenga sasa mara kapaulia bati ya mama mjane, dirashani kafunga karatasi dah wabongo, huyu wa pili sasa naye ni bwana mifugo flan na mkewe bi mifugo basi kajamaa sijui ni kutoka familia duni, hata hajahamia kaisha korofishana na majirani anawatuhumu kumwibia material , jumba alilojenga ni hidden roof na ukikosea kulijenga unakuwa sijui umejenga nini halipendezi , wabongo nyumba si mafanikio miaka hii ni mamuzi jaman kujenga au kutojenga