Kwanini jirani zangu hawanichangamkii?

Kwanini jirani zangu hawanichangamkii?

Wahaya mna taabu sana kwahiyo hujui kosa lako ni nini hadi usawa huu? achenio mashauzi ishini na jamii vizuri.
 
Sijaelewa tatizo lako hasa ni majirani kutokuja kwenye tafrija yako bila kuwaalika au bomba la maji kupasuka kufanya njia isipitike?

Nahisi kuna hali fulani ya maisha umejiaminisha unayo tofauti na wenzio kutarajia watu wakupapatikie.
Kutopata attention uliyotarajia ndicho hasa kinachokuumiza mengine ni ngonjera tu.
 
Majiranii wale wanaoka kibarazani asubuhi mpaka jioni wanapiga majunga kula yenyewe ya Tabu unategemea Wakupende?? Unategemea wampende Mkeo?? Ni ngumu sana yani Ukiishi na waswahili wewe kidogo maisha yako yana Nafuuu amini Watakuchukia tu unaweza mpa mtu salamu anakaa kimyaa kama hajasikiaaa[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] mjini hapa fanya mambo yako na usiumie wengine wakikuchukia maana sio shida zako labda kama wew bado hujajifunza una shobo nao.
 
Hipo hivi,
Jumapili hii niliandaa tafrija nikaalika ndugu na marafiki zangu wa karibu waje kujumuika na mimi kwenye hii nyumba yangu mpya ambayo hipo nje kidogo ya mji wakati tafrija hii ikiendelea nikaona isiwe tabu kufungua mlango ili yeyote atakayetaka kujumuika na sisi basi nae akaribie lakini kwa mshangao hakuna aliyekuja kabisa.

Leo narudi zangu mtaani jioni baada ya mizunguko ya hapa na pale nakuta njiani kuna shimo kubwa ambalo kwa haraka nikatambua kuwa kuna bomba limekatika kwahiyo njia ya kuingilia kwangu haipitiki, hivyo nimelazimika kupaki gari kwenye maegesho ya karibu na kunifanya nitembee kwa mguu mpaka kwangu.

Nimeenda kwa balozi wa nyumba kumi kutoa malalamiko yangu juu ya kufungwa kwa barabara bila ya Mimi kama mkazi wa mtaa huu kupewa taarifa yoyote ile, balozi nae kanipa jibu kuwa atalishughulikia hili suala mpaka saa hizi yamepita masaa matatu hakuna feedback.
bila kuwaalika Umeacha geti wazi waje waingie kama mbuzi,waliona ni dharau hizo "
nikaalika ndugu na marafiki zangu wa karibu"
 
Vipi mahusiano yako na majirani kipindi unajenga hiyo nyumba? Au umekuja kuwaarika tu wakati nyumba unahamia na huko nyuma ulikuwa unawalia bati na kuwapita kama ng'omb
Vipi mahusiano yako na majirani kipindi unajenga hiyo nyumba? Au umekuja kuwaarika tu wakati nyumba unahamia na huko nyuma ulikuwa unawalia bati na kuwapita kama ng'ombe?
Mara nyingi nikikutana na watu njiani kama wanapiga stori wakiniona tu nakaribia huwa Wana katabia cha kukaa kimya hii tabia inanichukizaga sana
 
[emoji23][emoji23][emoji23] Halafu anasema amekuta shimo akagundua kwamba bomba limekatika na njia imefungwa, akaenda kwa mjumbe kwamba Kwann njia imefungwa bila yeye kupewa taarifa [emoji23][emoji23] jamaa mtemi sana. Tatizo lipo hapo. Ndio maana mjumbe akasema tutalifanyia kazi Halafu kamute.
Mimi sio mtemi lakini nina haki ya kupewa taarifa sijajua hapo unapoishi wewe maana huyu balozi anazo namba za wakazi wote wa eneo lake Incase Kuna shida kama hizi taarifa ni muhimu kutolewa mapema
 
Ishi na watu vizuri nyumba yako itashika moto ukiwa kazini na hawatafanya kitu.

Mimi nilipohamia huku nikitoka asubuhi simpiti mtu bila kumsalimia. Nikifika kwa mama wa vitumbua napunguza mwendo "habari za saivi jirani zangu" halafu nawaungisha vitumbua nakuja navyo kazini.

Vijiwe vyote nawasalimia hadi vijiwe vya boda boda nikipita napiga horn Piii, afu nawapungia na wao wanajibu piii piii piii piii. Daah raha sana.

Sichangamani nao kupiga umbea ila nashiriki nao matukio. Msiba ukitokea nitatoka kazini mapema nitaenda msibani. Sherehe zao nachangia na ninaenda.

Acha kuringa .
 
Hipo hivi,

Jumapili hii niliandaa tafrija nikaalika ndugu na marafiki zangu wa karibu waje kujumuika na mimi kwenye hii nyumba yangu mpya ambayo hipo nje kidogo ya mji wakati tafrija hii ikiendelea nikaona isiwe tabu kufungua mlango ili yeyote atakayetaka kujumuika na sisi basi nae akaribie lakini kwa mshangao hakuna aliyekuja kabisa.

Leo narudi zangu mtaani jioni baada ya mizunguko ya hapa na pale nakuta njiani kuna shimo kubwa ambalo kwa haraka nikatambua kuwa kuna bomba limekatika kwahiyo njia ya kuingilia kwangu haipitiki, hivyo nimelazimika kupaki gari kwenye maegesho ya karibu na kunifanya nitembee kwa mguu mpaka kwangu.

Nimeenda kwa balozi wa nyumba kumi kutoa malalamiko yangu juu ya kufungwa kwa barabara bila ya Mimi kama mkazi wa mtaa huu kupewa taarifa yoyote ile, balozi nae kanipa jibu kuwa atalishughulikia hili suala mpaka saa hizi yamepita masaa matatu hakuna feedback.

Ni kwenye msiba tu ndio mtu haalikwi na sio kwenye sherehe.
 
Kama Kuna viumbe jeuri basi ni majirani wenye kipato Cha kawaida au Cha chini. Yaani hata ungepika pilau ungekula mwenyewe maana usipo alikwa unaenda kufanya Nini?

Kuhusu maisha Yako na majirani na uongozi wa mtaa, wewe unaonekana unajiweka daraja la kipekee ndiomaana wamekuacha uishi kivyako.
Teh!
 
Yani ndugu uwaalike alafu majirani wajilete tu kama wahuni?

Ungewaakika hata wawili watatu ungepungukiwa?
mashataka yake hayana mashiko yaani ufungue tu mlango kisa umepika pilau watu waje? majirani wanaalikwa tena one week before...hata wa5..swala la mabomba kupasuka kawaida na hao ni dwasco...alafu njia ni yake au ya mtaa?
 
Tajiri kuhamia tu anataka mtaa mzima umshobokee
 
Back
Top Bottom