Kwanini JK (Kanali nusu mstaafu) hana ushawishi kwa Kagame (Jenerali Mstaafu)

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
219,468
Reaction score
911,184
Vita vya maneno kati ya JK na Kagame vinaasharia jinsi ambavyo Kagame haoni kama JK ana ushawishi au hata ufahamu wa historia ya Rwanda na hivyo kumkejeli jinsi ambavyo anaona inafaa. Kagame ameahidi kumvutia pumzi JK na akipata mwanya atamzabua kofi kutokana na JK kumshauri Kagame kukaa mezani na waasi wa Rwanda.

Kagame ni vigumu kuthamini ushauri wa JK kwa sababu zifuatazo:-

1) JK haifahamu vizuri historia ya Rwanda ambayo imejengwa kwa damu. Watutsi ambao ni wachache wametumia damu kuwatawala wahutu ambao ni wengi na jinsi ya kuwawezesha wengi (Wahutu) bila kuathiri haki za wachache (Watutsi) ndani ya Rwanda imeshindikana hadi leo.
Mfupa uliomshinda Mzee fisi je JK atauweza kwa utendaji huu tunaoufahamu hapa nchini?

a) JK kushauri mahasimu hao wakae meza moja bila ya kujua ajenda na mikakati ya kufanikisha vikao tajwa kwa Kagame anaona ni upuuzi ambao mjenga hoja -JK- lazima azabuliwe kofi ili aache kujiingiza kwenye mambo yasiyomhusu.

b) JK katika masuala ya Muungano na kero zake amekuwa akiendelea kutegemea kamati ya viongozi wa kitaifa watokanao na chama chake cha CCM tu bila ya kutafuta wapinzani katika kushauriana nao. Hivyo aidha ni unafiki au usahaulifu tu kumshauri Kagame afanya yale ambayo yeye mwenyewe JK hana mpango wa kuyafanya.
Charity always begin at home.................

c) JK katika uundaji wa kamati ya marekebisho ya katiba katumia ubabe wa uwingi wa wabunge wa CCM Bungeni katika kupitisha sheria ambayo imempa yeye madaraka ya kurekebisha Katiba atakavyoona inafaa na ushirikishwaji wa wananchi ni changa la macho tu. Sasa yawaje amshauri Kagame kujenga mazingira ya ushirikishwaji wa mahasimu wake jambo ambalo yeye mwenyewe JK hayuko tayari kulifanya. Tena hapa nchini ingelikuwa ni rahisi zaidi kwa JK kwani hakuna umwagaji wa damu katika wananchi kudai haki zao za kimsingi zaidi ya ukatili wa polisi ambao anayo mamlaka ya kuwakemea na wala hana mpango wa kufanya hivyo..

d) Katika kero za Muungano, JK aliwahi kudiriki kusema kamati ya kushughulikia kero tajwa na kuundwa na chama kimoja tu cha CCM wawe wanakutana angalau mara nne kwa mwaka hata kama hawana la kujadili ikimaanisha tu yeye JK anacheza mchezo wa siasa wa kuonyesha raia kazi inafanyika hata kama hakuna linaloendelea! Mbali ya hilo, JK hana mkakati wa kuzimaliza kero za Muungano nje ya CCM na ndiyo maana hawezi kufiria muundo mbadala wa kutafuta ufumbuzi wa kero za muungano nje ya chama chake sasa iwaje amtarajie Kagame atafute ufumbuzi wa kero za Rwanda nje ya chama chake cha RPF?

e)
JK hana taswira ya kuutetea na kulinda utawala bora na ndiyo maana katika kipindi chake mauaji yanayofanywa na polisi hadi leo yanazidi yale yaliyofanywa na maraisi wote waliomtangulia. Pia, katika historia ya nchi yetu kamwe Waziri Mkuu hajawahi kutamka hadharani kuwa ni sahihi kwa polisi kupiga raia wanaodai haki zao. Hadi wa leo, JK yuko kimya na wala hajamchukulia Pinda hatua yoyote ile ikiashiria anaafiki udhulumaji wa haki za kimsingi kabisa za binadamu! Hivi kwa kisa kipi Kagame amsikilize JK ambaye hana rekodi yoyote ile ya kuheshimu utawala bora?

2)
Chaguzi ya Uraisi 2010 kuna utata mkubwa kati yake na Dr. Slaa ni nani alishinda Uraisi kutokana na Tume ya uchaguzi kufanya kazi kwa minajili ya kulinda masilahi ya CCM huku ikishirikiana na Idara ya Usalama pamoja na serikali za mitaa. Kagame pamoja na faulo zake kibao, hakuna anayemtilia mashaka ya uhalali wa chaguzi zote zilizomsimika madarakani. Kwenye mazingira ya namna hii, ni JK au Kagame ambaye anastahili kuwekwa darasani na mwenzie juu ya utawala bora?

3) Viongozi wengi wa TZ hususani CCM hukimbilia kutatua matatizo ya nje ya chi yetu na kutumia sarakasi hizo kufunika matatizo ya hapa nchini lakini wasichojua ni kuwa ili waheshimike ndani na nje ya mipaka ya nchi hii ni pale watakapoanza kutatua kwa dhati matatizo ya hapa ndani na kuyapatia ufumbuzi wa kudumu bila ya kujali masilahi ya muda mfupi ya vyama vyao.

4) Kwa karata hizi ni dhahiri Kagame yuko sahihi kabisa kumbeza JK kwa kumtishia na kunuia kumzabua kofi kwa kile ambacho ni
"kiherehere" cha JK kujiingiza katika tanuru la moto la wengine wakati hapa nyumbani moshi unafukuta kila mahali na JK haonyeshi hata dalili kujua majibu ya kero zetu yako katika nyanja ipi.
 
mkuu umechambua vizuri sana, naomba kama kuna mwenye jibu anisaidie, JK angetoa ushauri gani ambao nyinyi mngeuona ni wa busara zaidi? (msiniambie angenyamaza).

Sidhani kama ushauri alioutoa ni mbaya. Inawezekana kabisa kuwa substantively, ushauri wa Rais kwa Rwanda hauna tatizo.

Lakini tokea hili sakata lianze, hoja yangu imekuwa kuwa kabla ya kuyasema hayo hadharani, alishawahi kukaa informally au hata formally na Kagame na kumpa huo ushauri? What was the outcome?

Kama alishawahii kukaa nae na kumshauri hivyo lakini Kagame akaukataa huo ushauri, then it was fine for the President kwenda kwenye terraces za kimataifa na kusema aliyoyasema.

Lakini kama hawajawahi kukutana na kushauriana na Kagame juu ya hilo jambo, then surely hata kama ningekuwa mimi nisingejisikia vizuri kushauriwa out of the blue mbele ya kadamnasi ni-make peace na mtu ambaye bado naamini alinifanyia kitu mbaya.

Kama kweli unatataka kunisadia kuondokana na tatizo linalonikabili, then ongea na mimi kwanza. Sikiliza yangu ya moyoni.

Kama nikikataa ushauri wako na unaona tatizo linaweza kukuathiri hata wewe, then seek an alternative.

Tatizo hili suala linajadiliwa na watu wengi too emotionally, subjectively, and sometimes, irrationally.
 
kweli alikasirika hata kuweza kumuita rais wa nchi nyingine mpuuzi, mjinga na mpumba'vu kwamba akikutana nae anampiga? kisa ushauri ambao sio amri wala sharia?
 
Kwa kweli siwezi kujua kwa nini alikasirika hivyo. Sikuwepo Rwanda wakati wa genocide na wala sikuathirika nayo moja kwa moja.

Kuna siku moja nilikuwa na wabongo wenzangu na Mganda mmoja mwanamke wa makamo tukawa tunapiga story za East Africa tukatajikuta tunazungumzia kuhusu Idd Amin.

Yule mwanamke alikasirika ile mbaya na alituacha na kuondoka bila hata kuaga. Hatukujua ni kwa nini alikasirika hivyo.

Baadae rafiki yake alikuja kuniambia kuwa alikuwa na experience mbaya sana na Idd Amin mwenyewe kiasi kwamba hataki hata kusikia hilo jina.

Kwa hiyo, wakati sisi tulikuwa tunamwongelea Idd Amin kama tunavyoongea, kwa huyo mwanamke ilikuwa ni very sensitive issue due to her personal bad experience with the guy.
 
kweli alikasirika hata kuweza kumuita rais wa nchi nyingine mpuuzi, mjinga na mpumba'vu kwamba akikutana nae anampiga? kisa ushauri ambao sio amri wala sharia?

Wanasema ili uheshimiwe you have to earn your respect.

Hivi JK anastahili heshima kutokana na conducts zake kama Kiongozi wa nchi, au heshima inakuja tu automatically kwa sababu yeye ni Rais?

Tujiulize kama huo ushauri angeutoa say B.W Mkapa, je P.Kagame angerespond namna hiyo?
 
Vita vya maneno kati ya JK na Kagame vinaasharia jinsi ambavyo Kagame haoni kama JK ana ushawishi au hata ufahamu wa historia ya Rwanda na hivyo kumkejeli jinsi ambavyo anaona inafaa. Kagame ameahidi kumvutia pumzi JK na akipata mwanya atamzabua kofi kutokana na JK kumshauri Kagame kukaa mezani na waasi wa Rwanda.

Mkuu kwenye jukwaa la kimataifa kuna uzi mmoja unaendelea kule kuhusu wakimbizi wa Rwanda, kuna watusi wengi sana kule wanatoa maoni yenye akili. Sitaki kumuangalia Kagame kwa kauli anazotoa hata kama ni kututishia watanzania au vipi. Nataka kumuangalia kwa vitendo vyake, na jaribu kupima kauli ya JK (hata kama wewe unamuona JK hafai) kama kweli ina maana yoyote au haina maana yoyote kuhusu hali ya Mashariki kwa DRC. Kwanini Museveni hajatoa vitisho kwa JK, kwanini J Kabila hajatoa vitisho kwa JK, ni kwamba wao ni wajinga au? Lakini kauli kama ya JK mbona imetolewa na wengine wa Ulaya na Amerika? au ni ujinga inapotolewa na JK ni bisara inapotplewa na mtu wa Ulaya na Amerika?

Kwani JK ni mtu wa kwanza kupuuzwa na PK? Unajua PK ana superioity complex na anataka kila mtu afuate kile anachoamini yeye. The issue here is people are fed up with PK, kwa sasa jamaa anaonekana kuwa anahatarisha usalama wa muda mrefu wa watusi, na anaendelea kucheza kwenye makaburi ya watu waliouawa kwenye genocide mwaka 1994 kwa maslahi yake kiuchumi na kisiasa. Anadai kuwa kwa sasa watu wa Rwanda wanajiita wanyarwanda, hatuna wahutu na watusi, lakini ukiangalia kiundani anajenga hisia kali zaidi za uhutu na ututsi kuliko hata Habyarimana, na anataka wahutu wote waombe radhi kutokana na makosa ya Interhamwe. NI sawa na mtu uombe msamaha kwa kosa alilofanya baba yako au babu yako....

Maana yake nini kupambana na FLDR wakati na wewe unaunda kundi la M23 linalofanya uchafu mkubwa hata kuliko wa FDLR? Kundi la FDLR kimsingi ni kundi ma wauaji wahuni walioshika mapanga, lakini M23 ni la wauaji wanaoungwa mkono na kupewa msaada na PK wenye silaha za kisasa, wabakaji, wezi na wanaajiri askari watoto. Who is evil here waitu. What is the difference between Bagosora na Makenga? or Ntangda the terminator?
 
Kwasababu Rais Kikwete alikuwa Jeshini kama KADA wa CHAMA; Wakati wa VITA vya KAGERA yeye alikuwa Mhamasishaji wa CHAMA... kwahiyo alikuwa mbali na MILIPUKO na MABOMU; alikuwa kama MWIMBAJI HARAKATI...

Na baada ya Mafunzo yake ya kijeshi ya Mwanzo MONDULI sidhani aliishika tena HIYO BUNDUKI...

Sasa Kama KAGAME na MUSEVENI walikuwepo wenye VITA vya KAGERA wakipigana bega kwa bega na wanajeshi wa Tanzania... Walijua fika Rais KIKWETE hakuwepo...

*** Sasa HIYO NDIO sababu ya KAGAME kumkashifu Rais KIKWETE sidhani; Sababu kubwa ni Wivu wa KAGAME kwa KIKWETE, kupata UGENI wa MARAIS wa MATAIFA makubwa back 2 back hawakuifikiria RWANDA; KAGAME ana EGO haamini ya kuwa kutakuwa na kiongozi bora zaidi yake... Hilo ni kosa lake; Saa nyingine sio KIONGOZI ni NCHI kuwa BORA i.e kuwa na USALAMA na MALIGHAFI za kuvutia...
 
umeeleza vizuri sana kaka kabla ya Jk kumshauri paul kagame angestahili kutatua matatizo yanayofukuta ndani kwanza kabla ya kuvuka mipaka.kwanza toa boriti lilopo kwenye jicho lako kwanza ndio upate kumnyoshea mwenzako kidole .

Na mara nyingi huwa tunakimbilia ya wengine huku yetu yanatushinda na hata hatujui tuyaanzie wapi.........
 
Kwasababu Rais Kikwete alikuwa Jeshini kama KADA wa CHAMA; Wakati wa VITA vya KAGERA yeye alikuwa Mhamasishaji wa CHAMA... kwahiyo alikuwa mbali na MILIPUKO na MABOMU; alikuwa kama MWIMBAJI HARAKATI...

Na baada ya Mafunzo yake ya kijeshi ya Mwanzo MONDULI sidhani aliishika tena HIYO BUNDUKI...

Sasa Kama KAGAME na MUSEVENI walikuwepo wenye VITA vya KAGERA wakipigana bega kwa bega na wanajeshi wa Tanzania... Walijua fika Rais KIKWETE hakuwepo...

*** Sasa HIYO NDIO sababu ya KAGAME kumkashifu Rais KIKWETE sidhani; Sababu kubwa ni Wivu wa KAGAME kwa KIKWETE, kupata UGENI wa MARAIS wa MATAIFA makubwa back 2 back hawakuifikiria RWANDA; KAGAME ana EGO haamini ya kuwa kutakuwa na kiongozi bora zaidi yake... Hilo ni kosa lake; Saa nyingine sio KIONGOZI ni NCHI kuwa BORA i.e kuwa na USALAMA na MALIGHAFI za kuvutia...

nngu007 haya nayo ni ya kwako wao wanabishiania mambo mengine na wala siyo haya. Tatizo la maelezo yako ni kuwa kama JK asingeropoka nje ya vikao vya EAC unafikiri haya yangelimkuta? And why now?
 
Mkuu kwenye jukwaa la kimataifa kuna uzi mmoja unaendelea kule kuhusu wakimbizi wa Rwanda, kuna watusi wengi sana kule wanatoa maoni yenye akili. Sitaki kumuangalia Kagame kwa kauli anazotoa hata kama ni kututishia watanzania au vipi. Nataka kumuangalia kwa vitendo vyake, na jaribu kupima kauli ya JK (hata kama wewe unamuona JK hafai) kama kweli ina maana yoyote au haina maana yoyote kuhusu hali ya Mashariki kwa DRC. Kwanini Museveni hajatoa vitisho kwa JK, kwanini J Kabila hajatoa vitisho kwa JK, ni kwamba wao ni wajinga au? Lakini kauli kama ya JK mbona imetolewa na wengine wa Ulaya na Amerika? au ni ujinga inapotolewa na JK ni bisara inapotplewa na mtu wa Ulaya na Amerika?

Kwani JK ni mtu wa kwanza kupuuzwa na PK? Unajua PK ana superioity complex na anataka kila mtu afuate kile anachoamini yeye. The issue here is people are fed up with PK, kwa sasa jamaa anaonekana kuwa anahatarisha usalama wa muda mrefu wa watusi, na anaendelea kucheza kwenye makaburi ya watu waliouawa kwenye genocide mwaka 1994 kwa maslahi yake kiuchumi na kisiasa. Anadai kuwa kwa sasa watu wa Rwanda wanajiita wanyarwanda, hatuna wahutu na watusi, lakini ukiangalia kiundani anajenga hisia kali zaidi za uhutu na ututsi kuliko hata Habyarimana, na anataka wahutu wote waombe radhi kutokana na makosa ya Interhamwe. NI sawa na mtu uombe msamaha kwa kosa alilofanya baba yako au babu yako....

Maana yake nini kupambana na FLDR wakati na wewe unaunda kundi la M23 linalofanya uchafu mkubwa hata kuliko wa FDLR? Kundi la FDLR kimsingi ni kundi ma wauaji wahuni walioshika mapanga, lakini M23 ni la wauaji wanaoungwa mkono na kupewa msaada na PK wenye silaha za kisasa, wabakaji, wezi na wanaajiri askari watoto. Who is evil here waitu. What is the difference between Bagosora na Makenga? or Ntangda the terminator?

Alichoongea JK kinaweza kuwa kina maana njema tatizo ni kuwa hakufuata protokali kabisa. EAC ipo kwa ajili ya kutatua migogoro kama hii na wala siyo nje ya vikao vya maraisi wa EAC. Swali ni kuwa Is JK talking to Kagame or consiously raising his own profile while dragging the nation in the mire of his own making?
 
Wanasema ili uheshimiwe you have to earn your respect.

Hivi JK anastahili heshima kutokana na conducts zake kama Kiongozi wa nchi, au heshima inakuja tu automatically kwa sababu yeye ni Rais?

Tujiulize kama huo ushauri angeutoa say B.W Mkapa, je P.Kagame angerespond namna hiyo?

Angelijibiwa vivyo hivyo. Alichopaswa JK kufanya ni kupeleka maoni yake EAC na wala siyo kumwaga mtama kwenye kuku wengi........
 
Kwa kweli siwezi kujua kwa nini alikasirika hivyo. Sikuwepo Rwanda wakati genocide na wala sikuathirika nayo moja kwa moja zaidi.

Kuna siku moja nilikuwa na wabongo wenzangu na Mganda mmoja mwanamke wa makamo tukawa tunapiga story za East Africa tutajikuta tunazungumzia kuhusu Idd Amin.

Yule mwanamke alikasirika ile mbaya na alituacha na kuondoka bila hata kuaga. Hatukujua ni kwa nini alikarika hivyo.

Baadae rafiki yake alikuja kuniambia kuwa alikuwa na experience mbaya sana na Idd Amin mwenyewe kiasi kwamba hataki hata kusikia hilo jina.

Kwa hiyo, wati sisi tulikuwa tunamwongelea Idd Amin kama tunavyoongea, kwa hiyo mwanamke ilikuwa ni very sensitive issue due to her personal bad experience with the guy.

Ninachojifunza hapa ni kuwa pa kuanzia kwa JK ilikuwa ni ushauri ampe Kagame ana kwa ana ndani ya EAC ambako ndipo mahali pake khalafu penye wengi haliharibiki neno. Na ninaanza kuwa na mashaka hivi kwenye vikao vya maraisi ndani ya EAC huwa wanaongea nini kama suala nyeti kama hili linaongelewa nje ya vikao kama siyo kuogopana?
 
  • Thanks
Reactions: EMT
kweli alikasirika hata kuweza kumuita rais wa nchi nyingine mpuuzi, mjinga na mpumba'vu kwamba akikutana nae anampiga? kisa ushauri ambao sio amri wala sharia?

Anachoona Kagame ni kuwa wapinzani wake JK amewapa moral support........kwahiyo he is against him. In Rwanda backing one side or the other is an act of war for the losing side.
 
Sidhani kama ushauri alioutoa ni mbaya. Inawezekana kabisa kuwa substantively, ushauri wa Rais kwa Rwanda hauna tatizo.

Lakini tokea hili sakata lianze, hoja yangu imekuwa kuwa kabla ya kuyasema hayo hadharani, alishawahi kukaa informally au hata formally na Kagame na kumpa huo ushauri? What was the outcome?

Kama alishawahii kukaa nae na kumshauri hivyo lakini Kagame akaukataa huo ushauri, then it was fine for the President kwenda kwenye terraces za kimataifa na kusema aliyoyasema.

Lakini kama hawajawahi kukutana na kushauriana na Kagame juu ya hilo jambo, then surely hata kama ningekuwa mimi nisingejisikia vizuri kushauriwa out of the blue mbele ya kadamnasi ni-make peace na mtu ambaye bado naamini alinifanyia kitu mbaya.

Kama kweli unatataka kunisadia kuondokana na tatizo linalonikabili, then ongea na mimi kwanza. Sikiliza yangu ya moyoni.

Kama nikikataa ushauri wako na unaona tatizo linaweza kukuathiri hata wewe, then seek an alternative.

Tatizo hili suala linajadiliwa na watu wengi too emotionally, subjectively, and sometimes, irrationally.
Last edited by EMT; Yesterday at 14:29.​

Hoja ya JK ilipaswa iwe hoja ya kujadiliwa na maraisi wote ndani ya EAC....................na wala siyo nje ya vikao vya maraisi wahusika.
 
mkuu umechambua vizuri sana, naomba kama kuna mwenye jibu anisaidie, JK angetoa ushauri gani ambao nyinyi mngeuona ni wa busara zaidi? (msiniambie angenyamaza).

JK angelipeleka mapendekezo ya kutafuta suluhu ya Kagame na mahasimu wake ndani ya EAC na alipaswa aende na mikakati kupitia Mzee Sitta ambaye ndiye wizara yake yahusika. Lakini Sitta hawamuhusishi na kazi nyingi za Sitta zinafanywa na Membe! Ndani ya mjadala mkali ambao ungelijitokeza maazimio yangelifikiwa na utekelezaji ungelikuwa hauna bughudha kama hizi tunazoziona hivi sasa.
 
Alichoongea JK kinaweza kuwa kina maana njema tatizo ni kuwa hakufuata protokali kabisa. EAC ipo kwa ajili ya kutatua migogoro kama hii na wala siyo nje ya vikao vya maraisi wa EAC. Swali ni kuwa Is JK talking to Kagame or consiously raising his own profile while dragging the nation in the mire of his own making?

I may not agree with the suggestion that JK did not follow proper diplomatic protocols or raised the issue through inappropriate channels. The issue if insecurity in DRC is in no way EAC issue, though some of the effects of the insecurity are affecting some members, labda tusema ni suala la SADC, kwa kuwa DRC ni member. I do not think that JK is attempting to beautify his image, he has a tarnished image within the party, the country and within the EAC, ndio maana wakati wa maadhimisho ya miaka 50 hakuna rais hata mmoja aliyekuja kutupongeza. Tarnished image can not change with undiplomatic move.

Kwani JK alitoa kauli hiyo kichochoroni, kwenye chombo cha habari au aliitoa kwenye mkutano? what about those who gave same or similar statement, are they also trying to beautify their images?
 
Kwa kweli siwezi kujua kwa nini alikasirika hivyo. Sikuwepo Rwanda wakati genocide na wala sikuathirika nayo moja kwa moja zaidi.

Kuna siku moja nilikuwa na wabongo wenzangu na Mganda mmoja mwanamke wa makamo tukawa tunapiga story za East Africa tutajikuta tunazungumzia kuhusu Idd Amin.

Yule mwanamke alikasirika ile mbaya na alituacha na kuondoka bila hata kuaga. Hatukujua ni kwa nini alikarika hivyo.

Baadae rafiki yake alikuja kuniambia kuwa alikuwa na experience mbaya sana na Idd Amin mwenyewe kiasi kwamba hataki hata kusikia hilo jina.

Kwa hiyo, wati sisi tulikuwa tunamwongelea Idd Amin kama tunavyoongea, kwa hiyo mwanamke ilikuwa ni very sensitive issue due to her personal bad experience with the guy.

Mkuu jana nilikuwa namsikiliza jamaa mmoja aliyekuwa anasema yeye alikuwa Kigali wakati wa chinjachinja, na alinusurika mara mbili. Wauaji wa interhamwe walimkosa yeye na mtusi mmoja ambao walibahatika kuimbia na kuwakwepa.

Jamaa anasema kuwa ni ajabu kuona wale wahanga wakuu hawana mdomo mrefu kama wanasiasa wanatumia genocide kujinufaisha na kutekelza ajenda zao. Jamaa alinipuuza sana nilipsema PK. Akasema huyo jamaa hajui yaliyokuwa yanatukuta Kigali, yeye aliishi exile miaka mingi, na aliingia Kigali wakati jamaa wamemaliza unyama wao Kigali na kukimbia. Jamaa anaongea kwa uchungu sana na anasikitika sana kusikia Paul Rusesabagina amepewa nishani ya amani wakati aliwachangia hela Interhamwe, na Paul Kagame anatumia jina la watusi waliouawa kwa sababu za kisiasa, wakati hata yeye mwenyewe aliwaua wahutu. Jamaa anaona kuwa kukaa na kuzungumza na kusameheana ndio njia pekee, ya kuondoa mzizi wa fitna. Kunyosheana vidole na kupigana hakutaleta suluhisho la kudumu.
 
JK ameshindwa kujua kua matatizo ya Rwanda ni ya kiitikadi kali iliyojengwa kwenye misingi ya ubaguzi wa makabila. ni kma kuwaambia makaburu miaka ya 50,60,70 kuongea na ANC..unthinkable
 
Back
Top Bottom