Kwanini Kanisa limejengwa katikati ya madarasa?

Shule zote za serikali zilikua za katoliki!?..mazengo ilikua ya katoliki?..minaki!?
 
Kuna na chama la mabwege, kama wakivyokuwa wanaitana wenyewe back in the days.... TOSAMAGANGA. Hapo napo kuna kanisa kati ya mabweni na madarasa. Lakini kwa TOSAMAGANGA hata waislam walishapewa sehemu permanent za kuabudia, so ugomvi haukuwahi kutokea kisa kanisa au msikiti uko wapi, licha ya shule kufuga kitimoto pia. Ugomvi nilowahi ushuhudia ni pale dogo mmoja alipokwenda masjid na kipande cha nghhhh.
 
Unazingua ujue

Mratibu elimu kata
Mdhibiti ubora manispaa
OCD
DED
Mkuu wa wilaya
Bodi ya Shule
Mwenyekiti wa Mtaa
Wote hao hawajaona hilo?

Tafuta ukweli kwanza kabla haujakimbilia kuanzisha uzi.
 
Siyo za Katoliki tu ...pia zipo nyingine zilkuwa za KKKT mfano Ilboru
 
Pia zingine zilkuwa chini ya Islamic, Anglican, AIC , Moravian nk
 
Nenda pia kama unaelekea salasala nyoosha kama unaenda tegeta utaona
Kanisa la zamani nyuma kuna frem za maduka

Ova
 
Kwa bahati mbaya mhusika aliyetaifisha hayo maeneo ya Kanisa, ameshafariki.

Hata ukienda shule ya Sekondari Ndanda, Chuo cha ualimu Morogoro, Chuo cha ualimu Korogwe, nk. Utayakuta hayo Makanisa. Na huwezi kuyaondoa tu kirahisi! Maana Serikali iliyakuta, na kwa kutumia sera yake ya Ujamaa na Kujitegemea! ikataifisha hayo maeneo kwa nguvu.
 
Kwa wanaopajua uwanja wa fisi Tandale, pale kuna kanisa afu pamezingirwa na vyumba wanawake wanajiuza
 
Siyo shule zote ni za wakatoliki jifunzage kuandika taarifa sahihi. Kwa hiyo hata Ilboru(Arusha) ilikuwa ya wakatoliki? Acha ushabiki wa kidini andika tarifa sahihi kwa faida ya wasioujua hasa vijana wa siku hizi
 
Makaz ni ya wenye madrasa. Kama kawaida wenye makanisa upenda kujenga kwa waislam kama wanvyokazania kujaza makanisa zanzibar
 
Hiyo ni shule ya wamisionari,kanisa na shule vilijengwa pamoja kama ilivyo Minaki.Hiyo ilikuwa ikiitwa St.Frances Collage ya wakatoliki.Hapo akifundisha kijana mdogo Julius baada ya kutoka Edinburg Scotland.Shule hii baada ya uhuru ilitaifishwa kama zingine za kanisa ili kuondoa upogo wa elimu katika nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…