Kwanini kesi ya Mbowe imejikita kwenye ushahidi wa Mapolisi kukamata kuliko zana na mipango ya ugaidi?

Kwanini kesi ya Mbowe imejikita kwenye ushahidi wa Mapolisi kukamata kuliko zana na mipango ya ugaidi?

Inamaana ukila nyama choma na mo eneji, ni gaidi? Pia mie nasubiri ushahidi ambao upo kabla ya kukamatwa, sio huu wa pgo, nyama, kuamishwa central hadi tazara, ushahidi utolewe kuhusu ugaidi sio jinsi tulivyomkamata!
 
Tangu kesi ya Mbowe ianze ilielezea kidogo sana matukio ya Moshi ambako ndiko tulitegemea milango ilifanyika, sana tulichoshuhudia mbege party, manunuzi ya vocha za simu na safari za hapa na pale.

Wengi walitegemea hatua ya mwanzo wangeona zana za kutendea ugaidi kama vifaa vya kushambulia vituo vya mafuta, masoko, madaraja na si nyamachoma na mo eneji.

Hivi sasa kila shahidi upande wa mashitaka anaelezea matukio ya Dar baada ya ukamataji na si kisa cha ukamataji! Ni nini maana ya hii.

Mimi naona hapa kinachoendelea ni nani anajua kuongea zaidi ya mwenzake, na nani ameweka kumbukumbu ya alichofundishwa kuongea zaidi ya mwenzake

Sijui Jaji anayetakiwa achukue uamuzi atajikita kwenye ushahidi gani unaohusu vitendea kazi ya ugaidi, maneno au zana?

Tuone shahidi wa leo atatokea kwenye vikao vya Moshi au polisi wa Dar?
Umemaliza kila kitu. Nadhani Mahakama itaamua ndio kazi yake kutenda haki ila kwa sisi watazamaji ni kweli hatuoni ushahidi wa wazi au labda hatusikii yote huko ndani. Maana wenzetu nje huko hata wakijuwa wewe una misimamo hatari hawakukamati wanakuweka katika surveillance yao mpaka wajiridhishe sasa unataka kufanya kitu wanakuweka ndani na ushahidi wote lakini kama wanajuwa huyu mtu wa chama fulani cha kigaidi lakini yupo yupo tu kama nyoka asiye na sumu wanakuacha tu na kukuangalia.
 
Sasa idadi ya miti iliyopangwa kukatwa wangeweza kuitaja!
Watu wa mazingira wahusishwe, je miti yao wanataarifa ya kukatwa? Ni wazimu eti kwenda kukata miti kuziba barabara, watu watatu watatumia miezi mingapi kuziba barabara moja tu isipitike? Yaani ili likesi hata kulifuatilia unajihisi unaamwangalia mizengwee ITV!
 
Umemaliza kila kitu. Nadhani Mahakama itaamua ndio kazi yake kutenda haki ila kwa sisi watazamaji ni kweli hatuoni ushahidi wa wazi au labda hatusikii yote huko ndani. Maana wenzetu nje huko hata wakijuwa wewe una misimamo hatari hawakukamati wanakuweka katika surveillance yao mpaka wajiridhishe sasa unataka kufanya kitu wanakuweka ndani na ushahidi wote lakini kama wanajuwa huyu mtu wa chama fulani cha kigaidi lakini yupo yupo tu kama nyoka asiye na sumu wanakuacha tu na kukuangalia.
Kesi siyo siri tena maadamu watu wanaruhusiwa kuingia barazani, tangu imeanza habari ni zilezile.
Until now nothing hairraising!
 
Watu wa mazingira wahusishwe, je miti yao wanataarifa ya kukatwa? Ni wazimu eti kwenda kukata miti kuziba barabara, watu watatu watatumia miezi mingapi kuziba barabara moja tu isipitike? Yaani ili likesi hata kulifuatilia unajihisi unaamwangalia mizengwee ITV!
Ujue hawa watu watatu walikutwa na misokoto ya bangi na kwa hali halisi mtu akivuta bangi anaweza kufanya kazi pasipo kuchoka haraka, hivyo wangeweza kutekeleza azma yao ya kukata miti na kuitandaza barabarani toka Dar mpaka Iringa.
 
Hicho ndio wanauhakika nacho kwakuwa walifika wanaloita eneo la ukamataji, mengine ni mazito kwao kwani maigizo ni kipaji, na sii kila mmoja anacho
Sidhani hata hao mashahidi kama wanapenda kutoa ushahidi uenda wanatishwa watafukuzwa Kazi
 
Cha ajabu mbunge wa ccm huko Shinyanga aliyekutwa na silaha zaidi ya 10 yuko nje na hana tuhuma za ugaidi. Kisha kila siku magari ya serikali yanachoma mafuta kwenda mahakamani kulazimisha bastola moja ndio ilikuwa iende kutenda ugaidi!
Hawa sio wa kuwaamini kabisa wanaweza mbambika kesi yeyeto tangu walipofanya kwa wazee wa escrow na uhamsho hawashndwi kwa yeyeto tu
 
Ni Kwa vile Watanzania ni waoga, na kuhoji ni Kesi. Angalia jinsi Speaker alivyopanic..

DPP akishafungua Kesi mahakamani, police igp hawezi kusema fulani ni Gaidi Bila mahakama kudhibitisha

Rais hawezi kusema fulani ni Gaidi Bila mahakama kumkuta na hatia.

Ccm walimkana HAMZA, na ni mfadhili wao, na vitendo alifanya. Hiyo intelligence ya police Iko Wapi?

Mpaka Magaidi wanaingia kibiti, intelligence ilikuwa wapi?

Yaani mpaka Magaidi wafanye tukio ndio mkamate

Ushahidi: ziko wapi powersaw za kukata miti?

Wako wapi watu walioandaliwa kukata miti..
Hawana intelligence yeyeto nje ya ile ya kuvamia mikutano ya wapinzani
 
Hawana intelligence yeyeto nje ya ile ya kuvamia mikutano ya wapinzani
Siku walipokamatwa kwa dada muuza mbege waliambiwa ni magaidi! Inamaana polisi ndio waliofungua shitaka la ugaidi na si DPP, yeye alijulishwa tu!
 
Hicho ndio wanauhakika nacho kwakuwa walifika wanaloita eneo la ukamataji, mengine ni mazito kwao kwani maigizo ni kipaji, na sii kila mmoja anacho
Labda wange muongeza hapo Joti na Masanja mkandamizaji picha linge noga zaidi.
 
Kweli mkuu hsta DC Hai walimbambika kesi akafungwa miaka 30.
Kweli kabisa, Serikali ikamfunga mtu wao

Vyombo vya Dola vikatoa ushahidi dhidi ya mfanyakazi wa serikali.

Hongera, Mchangie Hela akate rufaa
 
Back
Top Bottom