Kwanini kijana hutakiwi kutoa mahari kwa karne hii

Unanikumbusha kwenye filamu ya Apocalypto, wanawake watumwa waliuzwa, walikaguliwa rangi ya meno na uimara wa matiti.
 
Umenena vema ingawa kwa kuangalia upande mmoja pekee. Jamii ulea watoto wote [me&ke] wawe wema na waweze kumudu majukumu yao hapo ukubwani.

Watoto wa kike kuna masuala yao yanatiliwa mkazo katika malezi na makuzi yao kama ulivo yaanisha hapa. Lakini umesahau kuweka ya wanaume pia.

Angalia ya wanaume sasa. Mimi nimeandaliwa kuwa baba. Nimepatiwa elimu huku nikisisitizwa kutojilinganisha na dada zangu maana mimi ni mtoto wa kiume, familia yangu hapo baadae itaishi kwa kupata mahitaji yote kutoka kwangu. Leo nina uwezo wa kuoa na kuhudumia familia yangu ipasavyo.

SWALI

1. Wazee wangu hawasitahiri kupata zawadi kutoka familia ya binti ili hali wameniandaa vema niweze kumudu kumtunza binti yao?

2. Uoni kwamba, mtoa mada ana hoja nzito?
 
Well sidhani kama unaweza kufananisha malezi anayopewa mtoto wa kike kulingana na majukumu yake na malezi anayopewa mtoto wa kiume kulingana na majukumu yake, malezi ya mtoto wa kike ni practical kwa maana kwamba anatakiwa aanze kujua kupika, kuosha vyombo, kufua, kusafisha nyumba, tangu akiwa nyumbani, malezi ya mtoto wa kiume ni theoretical yeye ataambiwa tu kwamba atatakiwa afanye kazi au biashara na anachopata ahakikishe anahudumia mkewe na watoto

Ndio maana mtoto wa kike kuolewa hawaangalii kama mwanaume tayari ana pesa na mali au hana, mwanaume hata akiwa masikini akitoa mahari atapewa tu mke wakiamini kwamba mafanikio yatakuja huko huko ndoani maana pesa haziji tu zinatafutwa, lakini wewe uliona wapi mtoto wa kike anaenda kujifunzia kazi za nyumbani akiwa tayari kwenye ndoa kama hajarudishwa kwao siku ya pili tu kwa maana anatakiwa aende kwenye ndoa akiwa tayari anajua hizo kazi

Halafu kingine hiyo ya kusema mahari ni shukurani kwa familia ya mke kwa kumlea binti ni minor reason tu ile major reason yenyewe huwa mnaifumbia macho, sababu kubwa ya kutoa mahari ni kutoa fidia kwa familia ya mke sababu mwanamke anapoolewa familia yake inahesabu imelose while ya mwanaume imegain, kwa maana kwamba mke na watoto wataenda kutumia majina ya upande wa mwanaume sasa kwa kuzingatia hilo mnataka familia ya mwanaume ipewe mahari kwa sababu zipi
 
Father wake kakataa katukatu, kasema kama nimeshindwa nimwachie binti yake pale...

Namimi stress siweezi

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Mtoa mada nakushauri ufwatilie alianzisha ndoa ni nani na utaratibu wa kutoa mahali ulianza ln na kwanini,vinginevyo unazungumzia mada yaliyokuzidi uwezo
 
1. Mwanamke huwa habadili jina ila huwa anabadili ubini wake au jina la ukoo kwasababu anahama ukoo wake na kuingia ukoo mwingine. Kubadili jina ni ishara ya kuhama ukoo wake na kuwa sehemu ya huo ukoo mpya.

2. Si mara zote mwanamke ananyang'anywa watoto. Ila kitendo cha watoto kuchukuliwa itategemea na sababu na sababu zipo nyingi. Inaweza kuwa sio mlezi mzuri wa watoto, watoto huwa wanafuata paternal clan sababu ndio uzao wao na asili yao inapotokea. Sasa sijui hapa unataka ufafanuzi upi zaidi.

3. Watoto kuitwa ukoo wa mwanaume ni ishara ya uongozi. Paternal clan ndio ina mamlaka juu ya watoto sababu ndio ukoo unaotakiwa kutoa malezi ya mbegu yao ya watoto na sio upande wa mama. Tazama koo ambazo watoto hupewa majina ya mama na kulelewa upande wa mama namna zinavyotoa wanaume dhaifu na wanawake majeuri.

4. Hiyo sio tamaduni na mila za africa nzima bali ni baadhi ya makabila na wanazo sababu za kufanya hivyo mojawapo ikiwa mali zinapokuwa mikononi mwa mwanamke akija mwanaume mwingine atazimiliki kama zake na hivyo jasho la mume na urithi wa watoto unaweza potea.

Kuna kisa kimoja za bibi kuwa na ali rithisha ng'ombe zake karibu 3000 kwa binti yake badala ya vijana wake, binti akaanza mahusiano na mwanaume akatapeliwa ng'ombe wote 3000 na huyo mwanaume. Kaka zake walienda kuwagomboa kwa kuwaiba na kurejea nao miaka kadhaa baadae ingawa hawakurejea ng'ombe wote 3000.
 
Mtoa mada nakushauri ufwatilie alianzisha ndoa ni nani na utaratibu wa kutoa mahali ulianza ln na kwanini,vinginevyo unazungumzia mada yaliyokuzidi uwezo

Aliyeanzisha Ndoa NI Nani?
Wahusika wakwanza kuingia kwèñye Ndoa NI kina Nani?
Je walitoa Mahari?
Kama walitoa Mahari, Nani aliyetoa Mahari? Mwanaume au mwanamke? Au huyo aliyeanzisha hiyo Ndoa ndiye aliyetoa Mahari?

Aliyetoa Mahari alimpa Nani?
 
Una mawazo ya ajabu sana. Na pia hio ni mtazamo wako kuhusu mahari,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…