Kwanini kila video ya Ubongo Kids YouTube ina chata ya Upinde wa Mvua au rangi za Upinde wa Mvua?

Kwanini kila video ya Ubongo Kids YouTube ina chata ya Upinde wa Mvua au rangi za Upinde wa Mvua?

Inawezekana ni kama utambulisho wa video zao...
Mimi naona tupambane na tabia maana mtoto mdofo ambaye akili yake haijawa diluted anaona ni rainbow tu hata hajui hayo mengine. Hiyo ni rainbow tu siku mfano mkuu wakichagua ndizi ni nembo yao, basi ina maana ndizi zote tutazipoga marufuku kabisa wala hatuli tena
Hawa wanataka kuwazoesha hizo rangi kupenyeza agenda yao kama ambavyo tulizoeshwa wanawake kutembea uchi taratibu taratibu mpaka sasa tumezoea.
 
Hio rangi wale jamaa wajanja sana wameiwahi wakati waliikuta angani ikipendeza zake wakaona waichukue ila haina ubaya kabisa ni rangi nzuri yenye maana ya kuzuia gharika.

Kuichukia rangi ya upinde ni sawa na wakristo kuchukia mwezi na nyota kisa kuna dini inavitumia kama nembo yake

Au waislamu kuichukia alama ya jumlisha kisa wakristo wanaitumia kama msalaba
Huwa hupendi kuandika sana ila siku ukiandika tu ni madini tupu, nakupenda bure kwa huo utashi wako Numbisa Mama.
 
Hili ni jambo jipya kwa sasa kwa videos za Ubongo Kids. Hapo awali hazikuwa na hizi rangi za upinde wa mvua. Lakini hivi karibuni naona videos zao zote YouTube ambazo zinaenda kwa jina la AkiliAkili zina rangi za upinde wa mvua!

Ubongo Kids wametokea kuaminiwa kwa videos zao zinazoburudisha na kufundisha.

Ubongo Kids inafuatiliwa na watoto na shule kutoka nchi kadhaa Africa, ilianzia Tanzania sasa inasambaa bara zima.

Angalia na thibitisha nilichoandika kwa kuangalia videos zenyewe, mfano:




Mashoga watu wa ajabu sana. Wanataka kujimilikisha upinde wa mvua, wengine wote waogope kuutumia, hii siyo sawa kabisa. Hivi kwa nini wasitengeneze bendera yao badala ya upinde wa mvua?
 
Rainbow ilikuwepo kabla ya hii movement, na sisi wazee tuliosoma kuanzia miaka ya 90 tunajua jinsi gani enzi za utoto wetu livyokuwa tunavutiwa sana na rangi za upinde chekechea na la kwanza tunaimba nyimbo za rainbow.

And by the way hizo rangi ulizoweka hazijapangana kama bendera za hiyo movement.

Kwa mwendo huu basi kila kitu kinachovutia kitageuzwa kuwa chao.
Bendera yao inaanza na red inaisha na purple.
Mambo yalianz Toka enzi,unamjua Farouk Bulsara aka Fredy Mercury?
 
Mimi nguo ya upinde wa mvua kama nikiipenda nanuna vazaa cha muhimu mimi mimi sio mfuasi wa hayo mambo....naona tunapoelekea sasa kila rangi itatambulisha jambo flani,leo watatokea watu na kusema wao ni wafuasi wa Shetani na rangi za nguo zao ni NYEUSI...kwahiyo sisi ambao sio wafuasi wa shetani tusivae mavazi yenye rangi nyeusi?
 
Hili taifa bado kuna wajinga wengi sana sasa hizo rangi ndio ushoga?

Swala ni kuķataa rangi au kukataa tabia mbona kama tunavamia vitu tusivyoelewa.
Miafrika tuna laana!!yaani tuna lundo la matatizo toka uhuru hatujayamaliza sasa leo tunahamisha AGENDA kwenye jambo ambalo bado halijawa kubwa sana kwenye jamii yetu!
 
Back
Top Bottom