Kwanini kina mama tu ndio huwa wanatueleza mabaya ya baba lakini sio rahisi kina baba kueleza mabaya ya mama?

Kwanini kina mama tu ndio huwa wanatueleza mabaya ya baba lakini sio rahisi kina baba kueleza mabaya ya mama?

Ndo maana mkaambiwa muwe viongozi nyie wababa
 
Ishini na wanawake kiakili, hii inajibu maswali mengi na kuepusha migogoro mingi kwenye familia. Wanaume sio waongeaji sana kwahiyo sio rahisi umkute analalamika unless iwe issue serious sana, pia wanaume hawana tabia ya kumbebesha mtu chuki.

Kwasababu akianza kukwambia mabaya ya mama yako automatically itamu affect mpaka yeye maana utaanza kum judge au kumkosea adabu ambayo shida itarudi kwake tena mama akianza kulalamika kuwa mwanae hamuheshimu, to make life easy anaona akaushie tu.
 
Ukaribu wa mtoto na mama ukiugundua, basi na swali lako limejibiwa
Nina ukaribu sanaa na binti yangu na kila likizo tupo wote na mambo ya shopping za Shule, out za weekend tupo wote.

Mimi na mama ake tulishaachana zamaniii, ila SITOKUJA KUMUELEZA MADHAIFU YA MAMA AKE.

Kwanini WANAWAKE WANAWEZA?

#YNWA
 
Ndio maana tukaitwa vichwa aka kiongozi, huwezi kuwa kiongozi halafu kila siku kulalamika, hata watoto watajifunza kulalamika, na kama ni wa kiume utawajengea hofu. Mtoto siku zote anaamini mama yake ndio binadamu mwema kuliko wote duniani, leo akimsikia baba yake analalamika kuhusu mama yake, atachanganyikiwa; na pengine atakosa imani kabisa
 
Nimejiuliza sana, mama zetu ni wepesi sana kueleza mabaya ya baba zetu na kuyaanika wazi, kauli kama kipindi unaumwa mimi ndio nilikupeleka hospital baba yako alikuwa amelewa chakari, baba yako alikuwa akipata hela basi humuoni nyumbani n.k...

Kauli za namna hiyo zimekuwa nyingi sana katika familia zetu, cha ajabu utakuta mama huyo huyo amedumu na mzee kwa miaka 30, utabaki unajiuliza amedumu vipi katika mazingira magumu hivi? Jibu lao simple sana "sikutaka kuwaacha peke yenu" sawa, sasa mbona unanawiri tu?

Upande wa akina baba ni tofauti sana, wao hawaaniki mabaya ya mama zetu, wanawasitiri sana na kutusisitiza tumpende na tumheshimu mama.

Kwani akina baba huwa hawafanyiwi ubaya na mama zetu? Na akina mama kwanini wasichague kuyaanika mazuri ya akina baba?
Wee hawa mama zetu bwana waajabu sana. Wanalalamika lakini wanabaki maana huduma ipo ebu baba afulie uone kama watabaki...baba atatukanwa matusi yote
 
Mi siwezi elezea ya wife kwakua mimi ni mwepesi kusahau na siyo kwamba sipendi kumsagia kunguni.
 
Nimejiuliza sana, mama zetu ni wepesi sana kueleza mabaya ya baba zetu na kuyaanika wazi, kauli kama kipindi unaumwa mimi ndio nilikupeleka hospital baba yako alikuwa amelewa chakari, baba yako alikuwa akipata hela basi humuoni nyumbani n.k...

Kauli za namna hiyo zimekuwa nyingi sana katika familia zetu, cha ajabu utakuta mama huyo huyo amedumu na mzee kwa miaka 30, utabaki unajiuliza amedumu vipi katika mazingira magumu hivi? Jibu lao simple sana "sikutaka kuwaacha peke yenu" sawa, sasa mbona unanawiri tu?

Upande wa akina baba ni tofauti sana, wao hawaaniki mabaya ya mama zetu, wanawasitiri sana na kutusisitiza tumpende na tumheshimu mama.

Kwani akina baba huwa hawafanyiwi ubaya na mama zetu? Na akina mama kwanini wasichague kuyaanika mazuri ya akina baba?
Wanaume wana vifua vya kuyabeba na kuyaficha kina mama hawana
 
Back
Top Bottom