Kwanini kina mama tu ndio huwa wanatueleza mabaya ya baba lakini sio rahisi kina baba kueleza mabaya ya mama?

Ndo maana mkaambiwa muwe viongozi nyie wababa
 
Ishini na wanawake kiakili, hii inajibu maswali mengi na kuepusha migogoro mingi kwenye familia. Wanaume sio waongeaji sana kwahiyo sio rahisi umkute analalamika unless iwe issue serious sana, pia wanaume hawana tabia ya kumbebesha mtu chuki.

Kwasababu akianza kukwambia mabaya ya mama yako automatically itamu affect mpaka yeye maana utaanza kum judge au kumkosea adabu ambayo shida itarudi kwake tena mama akianza kulalamika kuwa mwanae hamuheshimu, to make life easy anaona akaushie tu.
 
Ukaribu wa mtoto na mama ukiugundua, basi na swali lako limejibiwa
Nina ukaribu sanaa na binti yangu na kila likizo tupo wote na mambo ya shopping za Shule, out za weekend tupo wote.

Mimi na mama ake tulishaachana zamaniii, ila SITOKUJA KUMUELEZA MADHAIFU YA MAMA AKE.

Kwanini WANAWAKE WANAWEZA?

#YNWA
 
Ndio maana tukaitwa vichwa aka kiongozi, huwezi kuwa kiongozi halafu kila siku kulalamika, hata watoto watajifunza kulalamika, na kama ni wa kiume utawajengea hofu. Mtoto siku zote anaamini mama yake ndio binadamu mwema kuliko wote duniani, leo akimsikia baba yake analalamika kuhusu mama yake, atachanganyikiwa; na pengine atakosa imani kabisa
 
Wee hawa mama zetu bwana waajabu sana. Wanalalamika lakini wanabaki maana huduma ipo ebu baba afulie uone kama watabaki...baba atatukanwa matusi yote
 
Mi siwezi elezea ya wife kwakua mimi ni mwepesi kusahau na siyo kwamba sipendi kumsagia kunguni.
 
Wanaume wana vifua vya kuyabeba na kuyaficha kina mama hawana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…