Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,096
- 4,948
Umeme kuwa wa mgawo katika nchi kunakimbiza wawekezaji na kuua biashara za watu ikiwemo mitambo.
Katika hali ya kawaida na katika kulinda taswira ya uwekezaji nchini si Busara kiongozi kutoka adharani na kujitetea kuhusu umeme kukatika. Busara na hekima za kiongozi nikujifungia na safu yake na kutafuta solution
Kinachoendelea sasa hivi nchini kuna kila dalili za kufelishana, yaani kiongozi A anapoondolewa ofisini akiwa huko mbali anatumia mbinu mwenzake asifaulu kwa mantiki ya tufeli wote.
Hii vita ya tufeli wote haina uzalendo nyuma yake badala yake imeongozwa zaidi na ubinafsi na uchu wa madaraka
Tumezalisha mitandao ya watu wanaodhani watakuwa marais wa nchi, wote wana umri sawa na wapo nyuma ya kiongozi mmoja. Kudhani kwamba uwaziri hautoshi kumepelekea wasitoe msaada kwa nchi badala yake waelekeze nguvu kutafuta fedha za kuunda makundi na network za urais
Turudi mezani tukanyane, tuwakanye bila kujali wazazi wao wana mchango gani kwenye mafanikio yetu. Tuache kudhani kwamba baba na mama zao ni bora kuliko nchi. Makundi yanatufanya tuwe watumwa kwa kujenga mianya ya kuuza rasilimali za nchi ili tuendeshe nchi
Msoga Gang vs Sukuma Gang siyo hitajio la nchi tupige vita. Hizi kauli za viongozi waliopo madarakani kwamba angekuwepo JPM umeme usingekatika zitufikirishe na tuone kwamba tuliowaamini awatuamini.