Kwanini kitabu cha Enoch kinapingwa vikali na Wanathiolojia?

Kama unayosema ni kweli je kuna baya lolote ametenda mwandishi kwa kuandika hivyo vitabu na labda hakuongozwa na roho mtakatifu hadi unakubali tusivisome?
 
Kuna nadharia nyingi bout the book of enoch inasemekana kilitolewa na mungu mwenyewe coz kilikua kinaelezea conflict btn fallen angels na binadamu so kilikua kinaelezea namna ya uundaji mbalimbali wa silaha ambazo zingefanya dunia iwe sehemu mbaya zaid ya sasa kwamana ya vita.

inasemekana that waz one of a reason enoch kuchukuliwa na Mungu pasipo kupata umauti ni binadamu pekee ambaye hakufa fatilia kitabu cha mwanzo so alichukuliwa ili kuprevent the knowledge of creating weapons isisambae sana though inasemekana baadhi ya fallen angels walikua na baadhi ya maandiko ya kitabu hicho n still cursed on earth working secret try be like God by destroying wat created by him ndo vitu kama uwepo wa powerful weapons kama nuclear etc
 
Kama unayosema ni kweli je kuna baya lolote ametenda mwandishi kwa kuandika hivyo vitabu na labda hakuongozwa na roho mtakatifu hadi unakubali tusivisome?
Unaweza kusoma kama una Imani thabiti kuhusu Biblia. Lakini kama Imani yako ni haba, basi tarajia kufisha Imani yako katika kitabu cha Biblia.

Ninachomlaumu ni kuunganisha mafundisho ya Imani za kipagani na Biblia, vitu ambayo kamwe haviigiliani.
 
Enock kwenye bible ameelezwa kma mtu aliyeishi maisha ya utakatifu duniani na Mungu alimpenda sana alkua anamuwaza Mungu masaaa 24. Hata akitembea njiani alkua anaangalia chini asije akakanyaga wadudu wadogo (hii ni sababu ya kuchukuliwa moja kwa moja mbinguni)

Naomba kujua je,mwandishi wa kitabu cha enock alkua yeye?hicho kitabu kinaelezea maisha yake??
 
Basi kumbe unataka kubishana sio facts.... Endelea basi kubishana...
Facts gani? Hujaweka fact yeyote zaidi ya assertion isiyo na ushahidi. Sina muda wa kubishana na mtu, ila nilikuwa naonesha ukweli kwamba kauli tupu kama hiyo hata mimi naweza kuisema. Kusema ni kitu kimoja ila ushahidi ni kitu kingine.
 
baby wangu kumbe unamjua Mungu eeh ngoja nitafute kitabu cha tomaso halafu kitakuwa cha kweli maana huyu tomaso alikuwa mwanafunzi wa yesu so ina maana aliyoandika ni ya kweli maana aliyaona unlike kina mathayo .luka marko wale walisimuliwa tu
Miss una hakika na haya unayoandika?.
 
Kwa mtazamo haya mambo ya imani ukitaka scientific proof kwa maana ya objective truth tutabishana mpaka kesho ila kinachotekea people just wondering n speculating on bible matters so ikitokea theory inayoconnect dots vizuri bhas itasambaa sana mana kuna theory mbalimbali za kuelezea matukio ya kwenye bible ambayo ikifatilia unaeza ukakubali kama journey to caanan, moses meet god etc.

ndo mana nikaanza mwanzo kuwa kuna mitazamo mbalimbali ambayo inatolewa na binadamu kama sisi angalizo langu ni kwamba dont put religion matters into scientific proof u'll go to hell coz religion is matter of beliefs hata kama unachoamini ni kweli au uwongo just believe tu n dnt question coz its a sign of not believin refer Noah aliamini sauti tu kwamba jenga safina kuna mvua itakuja lakin mvua haikuja kwa mda mfupi ilikuja baada ya miaka mia kadhaa kupita but he wa believing tu people laugh n mock him ila hakujali tu back to topic the book of enoch inasemekanan kiliandikwa na enoch mwenyewe ambaye alichukuliwa na mungu to heaven he was absolute holy n loyal to GOD
 
Unaweza kusoma kama una Imani thabiti kuhusu Biblia. Lakini kama Imani yako ni haba, basi tarajia kufisha Imani yako katika kitabu cha Biblia. Ninachomlaumu ni kuunganisha mafundisho ya Imani za kipagani na Biblia, vitu ambayo kamwe haviigiliani.
Unamlaumu mtu ambae kimsingi unakubali aliongozwa na roho mtakatifu ikiwa wewe huyo roho mtakatifu huna?

Kwanini unatanguliza mtu anaetaka kusoma vtabu hivyo awe ana Imani thabiti huoni unamchagulia mtu jinsi ya kuelewa maana hapa watu wamesema kuwa huyo jamaa ni miongoni mwa binadamu wawili ambao hawajafa Bali walichukuliwa na mungu na kwamba aliongea na mungu, na kama ujuavyo kwenye biblia wapo waandishi walioandika kwa kuhadithiwa tu na ndio unaweka angalizo mtu awe na Imani sasa amini alieona au aliehadithiwa?
 
ni kwa sababu wale malaika kama 200 waliohasi kutoka mbinguni wanikuja duniani na kutembea na wanawake huku duniani na ndipo kikatokea kizazi cha watu weupe ambao kwa sasa tunawaita wazungu so baada ya hapo wazungu walivyoona kwamba dunia itajua ikabidi wakitoe kitabu cha Enoch
 
Kuna bonge la kitabu lilitolewa pia lilikuwa linaitwa gospel of Thomas!....... Nafikiri hiki ndo kilikuwa kitabu bora kabisa katika bibilia!.....Sisi wanadamu hasa wa dini ya kikatoliki ni wabaya sana![emoji22]
Kwani kwenye biblia wanazotumia madhehebu mengine vimo?
 
Huna haja ya kuogopa....Vitabuvya Apocripha vipo vingi sana,,,,,Hata kule kwenye Agano la Kale vipo kibao...Ila havina maana yoyote kwa maisha ya Mkristo zaidi ya kujaa uzushi na ushabiki...
Kumbe unajua unalolifanya mkuu,Apocryphal books vipo vingi,sana katika agano la kale(Old Testament), na vingi vimeongezeka mara tu baada ya uasi wa Wayahudi dhidi ya dola la Kiyunani(Greece empire) 331 BK - 168 BK,Kipindi hiki ndipo vitabu vingi vya kiharakati (Jews activist books)viliandikwa na lengo likiwa kueneza propaganda na kuwatia moyo(Unit), wayahudi kupambana na utawala wa Kiyunani,vingi vimeandikiwa Palestina na Misri hasa mji wa Alexandria (uliopata jina kutokana na jina la mtalawa wa kigriki,Alexander The Greet(333 BK -),miongon wa vitabu ni Maongezeko ya kitabu cha Ester(Ester's Additional chapters) na Daniel (BELI NA JOKA),TOBITHI,HEKIMA YA SOLOMON, WAMAKABAYO KITABU CHA KWANZA NA CHA PILI,NA HEKIMA YA SILA,vitabu hivi havihusishwi kama maandiko matakatifu kwa sababu zifuatazo;
1:Ni vitabu vinavyohamasisha watu mambo ya kisiasa si ya Kidini(Political reformations writings)Mfano,Vitabu vya makabayo

2:Hayina mapatano vitabu vingine vya Kiteolojia kama Taurat na Zaburi(Zab'ur),na Manabii(Nab-eem)(Non correspondent doctrines)Mfano,Beli na joka

3:Havina uhalisia(Fictitious writings),Mfano Tobithi,sura ya ini la samaki kutibu majini.

4;Kutopatana/kutolingana kwa matukio na vipindi vya kihistoria(Chronicles inaccuracy),

5:Ubinafsi wa uhusika,kuelezea matendo mema tu ya muhusika(Individuality) ambaye ni mwandish mwenyew

6:Kutojulikana kwa waandishi

7:Kuingiza mambo ya tamaduni na uganga (Witchcraft norms & traditions)yasiyopatana na neno la Mungu.

8:Muda wa uandishi,Biblia imeandikwa katika mpangilio unaofuatana(Chronological order), kati ya matukio na muda,Theologically Kitabu cha Mwisho kabisa kilichovuviw ni Malaki(Malach) cheny sura(chapters) 4 kinachonekana kimeandikwa 445 BC,na kutoka hapo kikatoa ahad ya kuja KRISTO NA AGANO JIPYA,rejea Malak 4:4-6.Baada ya hapo Mung akakoma kunena had alipotuma malaika kwa Zacharia na Maryamu,hivyo katika kipindi hiki cha ukimya(NON PROPHETIC TIME)ndipo vilipo ibuka hivyo vingine kama nilivyotangulia eleza.

NB,NITAKUW TAYAR KUJIBU PIA KUHUSIANA NA VITABU VINGINE VYA INJIL MFANO INJIL YA THOMAS NA BARNABAS.
Natanguliza shukrani, be blessed as you will find this comment useful!!.
Dukeson!!.
 
Mkuu c uweke attachment hapa
 

Vitabu Saba vya Agano la Kale ambavyo vipo katika Biblia Halisi (Catholic na Orthodox) hivyo siyo Apocripha. Vitabu hivyo vilikuwapo toka Biblia inakuwa Compiled na Kanisa Katoliki.

Alikuja kuviondoa Martin Luther Kipindi kile cha Reformation....
 
MKUU MARTIN LUTHER HAKUWAHI KUPUNGUZA KITABU CHOCHOTE ALICHOFANYA *ALITAFSIRI BIBLIA KUIWEKA KATIKA INDO - EUROPEAN LANGUAGES, KAMA GERMANY NA LATIN,MKUU PLEASE ELEWA.
Asante mkuu.... Nimetumia nafikiri... Sikuwa na uhakika lakini aliattempt kufuta wenzake wakampinga...
 
MKUU MARTIN LUTHER HAKUWAHI KUPUNGUZA KITABU CHOCHOTE ALICHOFANYA *ALITAFSIRI BIBLIA KUIWEKA KATIKA INDO - EUROPEAN LANGUAGES, KAMA GERMANY NA LATIN,MKUU PLEASE ELEWA.
Kwani Bible yenye vitabu kiprotenstant iliyo na vitabu vichache haina vitabu vya deuterokanoni alivitoa nani kama sio Martin Luther!!?

Naomba kujua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…