Wapendwa, msidanganyike. Enoki alikuwa na vitabu viwili. Cha kwanza, ni mile kilichohusika na majina ya malaika wote , ukiwa ni pomaja na wale majemadari 72 waliofukuzwa mbinguni. Kitabu hiki, ndicho kinachotumiwa na waganga, na hata wahubiri wa makanisa ya sasa katika kazi ya utoaji wa mapepo. Waganga Hawa, pia hutumia vitabu viwili vya mfalme sulemani alivyoviandika na kuvitumia katika mambo ya uuguzi. Kwa hivyo,kitabu cha Enock cha majina ya malaika, hakina faida yoyote kwa Mtu asiyekuwa na mambo ya uganga.wanaokitumia kitabu hiki, ni wale wanaotaka kutumia watu vipande, na kutibu kwa njia ya uganga. Sasa kama mkristo, unakatazwa kutafuta msaada kutoka kwa watu, viumbe vilivyoko mbinguni,(malaika), ya nini kuhangaika na kitabu chenye majina ya malaika?. Kitabu cha pili cha Enock ni kitabu kinachohabari zote za maisha na kazi aliyoifanya Bw. Yesu. Yaani vitabu vya Injili (Mathayo, Marko, Luka , na Yohana. Maelezo ni Yale yale , tofauti ni kuwa badala ya jina la Yesu imeandikwa "kiongozi wa watu".) Hivyo hakukuwa na sababu yoyote ya kuhangaika na kitabu cha Enock . Anayetaka kusoma kitabu cha pili cha Enock, asome Injili za mathato, Marko, Luka, na Yohana,.Achana na vitabu vya Enock vitakutenga na jina tamu, la Yesu maana wa Mungu Aishiye milele.