Kwanini kitabu cha Enoch kinapingwa vikali na Wanathiolojia?

Utingo wewe unazungumzia kusoma historia au kusoma neno la Mungu kama somo la historia hii ya elimu dunia?

Kama unaisona Biblia kama neno la Mungu basi lazima ujue Mungu ndiye hilo Neno. Kitabu cha Mwanzo1 tunajifunza Mungu alivyo uumba ulimwengu na vyote viujazovyo kwa kutamka Neno tu. Kitabu cha Yohana 1 kinatueleza kuwa huyu Mungu ni neno.

Lakini lazima ujue kuwa Mungu ni Roho na anapaswa kuabudiwa katika roho na kweli. Sasa huwezi soma Maandiko matakatifu kwa macho na akili hizi za nyama/mwili ukayaelewa ngo!! na rudia tena hutayaelewa ng'o!!. Ili uyaelewe lazima kumuomba Mungu akujaze Roho wake, otherwise ni kutwangwa maji kwenye kinu. Ndiposa utaona wengine wanalaumu watu kuwa too religious, haliepuki hilo as long as unajadili yaliyo katika Biblia. Shetani na mawakala wake hawakubali hili litokea maana watu watakapo lijua Neno la Mungu kwa uongozi wa Roho Mtakarifu ndio watakuwa wameijua kweli na kweli itawaweka huru. Wakiwa huru shetani hanachake tena.



Na washawasha!


 
Watu wengi hawajui kuwa Mungu anao mpango wake Maalumu au mpango mkakati kumhusu mwanadamu ambaye katika viumbe vyote vilivyo umbwa na Mungu basi mwanadamu ndiye aliyependwa na kuheshimika sana na Mungu. Najua mawakala wa shetani watasema Mungu anakuwa je na upendeleo?

Katika huu mpango mkakati wa Mungu kwa mwanadamu ndio utakuta haya yanajitokeza.

Ismaili mtoto wa kwanza wa Ibrahim kwa kuzaa na kijakazi Hajiri lakini si wa kwanza kwa maana ya Mpango wa Mungu kwa mwanadamu. Ni wa kwanza kwa mpango wa Ibrahim na Mkewe Sarah. Mtoto wa kwanza kwa mpango wa Mungu, Ibrahim na Sarah mkewe akawa ni Isihaka aliye Mzaa Yakobo/Yakubu ambaye alitwa Israel hapo baadaye.

Taifa la Israel yaani uzao wa Yakobo ni taifa teule la Mungu katika mpango wake wa kufanya kazi ya ukuhani kwa wanadamu. Ndipo sasa hata kuhani mkuu Yesu Kristo akaja duniani kupitia taifa hili na kufanya kazi ya ukuhani ambayo ndio imeleta ukombozi kwa mwanadamu.


Na washawasha!
 
Watu weusi kabla ya kuja watu weupe hakukuwa na historia ya wanaume kuingiliana kinyume na maumbile. Hakukuwa na ndoa za jinsia moja. Haya mambo ya Sodoma hayakuwepo.

There is nothing new under the sun! Watu weusi inawezekana waliingiliana sana ila hatuku documents vitu vyetu whether ni vizuri au vibaya.
 
There is nothing new under the sun! Watu weusi inawezekana waliingiliana sana ila hatuku documents vitu vyetu whether ni vizuri au vibaya.
You could be right or wrong. Mkuu vitu vingi vilivyokuwepo kale tumerithishwa kwa mapokeo km kulima, tohara, ufugaji, tiba za jadi n.k. Lakini hili halijaachwa halionekani ktk jamii zetu hata chembe kwa mfumo wa mapokeo, wala hakuna hata alama za michoro mapangoni ktk jamii zote za waafrika weusi.

Nenda Amboni na kwingineko hakuna. Jambo lililowahi kuwepo lazima alama zingebaki. I stand to be corrected. Lakini kwa wale jamaa weupe ushahidi upo kwamba michezo hiyo wameirithi toka kwa mababu zao, sema hapo kati walikuwa wamejaribu kuacha/kupunguza ila sasa wanarudia kwa kasi.
 
mkuu endelea unatuacha njia panda bado.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Niliambiwa nitafute history za ma empire za Cameroon, Central Africa nadhani na Congo kuna machifu sijui wafalme walikuwa wanalala na wanaume wenzao ushahidi inawezekana upo sema tuko na siri sana since tulijua ni makosa.

Kuna jamii hata ziliua vilema na mapacha Leo hii tunasema hakuna vilema au mapacha kwa hizo jamii Fulani lakini si kweli kama kulikuwa hakuna kumbe tuliua vilema na mapacha. Sijatafuta kujua ukweli kuhusu hizo empire lakini naamini there is nothing new under the sun.
 
Nimekupata mkuu. Ukifanikiwa kupata ukweli wa hilo jambo nishirikishe mkuu, dunia ina mengi na kila siku ni ya kujifunza jambo usilolijua.
 
Kanisa la katoliki ndo vinara wa kung'ofoa vitabu kwenye bibilia,nawalaani katika jina la muumba wa mbingu na nchi![emoji22]
Utapata dhambi bure ndugu, jiulize kwanini madhehebu yaliyotofauti na wakatoliki wanaitwa waprotestanti, wana protest nini? Biblia zinaxotumiwa na wakatoliki ina vitabu 72 lakini vya waprotestanti ni 68 je nani kapunguza vitabu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
shukrani sana mtoa mada kweli kuna mambo yanaendelea huku duniani hata pakuanzia hatuoni. natoa pongezi kwa waanzilishi wa Jamii forum hakika si nyie mliwaza bali mungu aliwapeni wazo angalo baaadhi ya watu wake waelimike. muwe wavumilivu kwa yote.
 
mkuu Eiyer kwenye post yako [HASHTAG]#108[/HASHTAG] umeongea kwa uchungu sana kaka,ni jinsi gani unavyojali angalao kwa uchache wengi wetu tujue kile kinachoendele hapa duniani.lkn tumejaliwa kupuuza yale ya msingi, naomba nikupe moyo brodher wengi tunakuelewa sana.
 
Habari za Siri kama zipi Mkuu
 
mkuu Utingo kun kitu nimekinot kwenye coment yako kupitia mistar ulioitoa kumbe kuna pia kitabu cha yashari? sikuwahi kusoma wala kudhania hili, na hata nikiuliza kwa kiongozi wangu wa kiroho nadhani hatanipa jibu, unaweza kutupa mwanga kidogo mkuu?
 
Kuna kitu nimenot pia kupitia coment ya Eiyer kuhusiana na wazungu, mf kanisa katoliki huwa linautaratibu wa kuwaheshimu na kuwaomba watakatifu ambao ni watu walioishi hapa duniani na asilimia kubwa ni wazungu wote africa wapo 3 nadhan,si bure haya.
 
Mkuu endelea kumwaga uelewa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…