Kwanini Kitimoto kinauzwa Bar na Hotel kubwa tu? Ni marufuku Mama ntilie na wauza Chips kuuza kitimoto?

Kwanini Kitimoto kinauzwa Bar na Hotel kubwa tu? Ni marufuku Mama ntilie na wauza Chips kuuza kitimoto?

Hivi kitimoto ni kwa ajili ya walevi na wenye kipato kikubwa tu? Kwa nini hii nyama inauziwa baa na hotel kubwa tu halafu iliyoiva pia inapimwa kuanzia nusu kilo tu?

Kwa nini hakuna mama ntilie wanaouza kitimoto kama mboga ya ugali na wali?? Hatuoni huu ni unyanyapaa kwa watu wasioweza kuagiza kuanzia nusu kilo?!

Hili hali inahitaji kubadilika kuwe na mama ntilie wanaouza kitimoto na wauza chips wanaouza mishikaki ya kitimoto.
Hujaenda Njombe, Sumbawanga, Mbeya, Songea na kwingine
 
IKiuzwa kwa mama ntilie makobazi watalalamika. Vyombo vya kitimoto vitachanganyika na vingine
Wanaouza mboga ya kitimoto wabandike kibao tu, halafu mbona Kambale, pweza, ngisi, jodari n.k wanauzwa kwa mama ntilie ila Wasabato hawalalamiki?
 
Wanaouza mboga ya kitimoto wabandike kibao tu, halafu mbona Kambale, pweza, ngisi, jodari n.k wanauzwa kwa mama ntilie ila Wasabato hawalalamiki?
Makobazi ni walalamishi si unawajua
 
Kitimoto bila PICHA yake sw na takataka TU
KAZI ni kipimo cha utu
 
nadhani majibu uliyapata ukitaka omba maeneo inapopatikana utapewa eneo
 
Back
Top Bottom