Kwanini klabu ya Simba iandae mechi ya kirafiki timu ya Taifa ikicheza?

Kwanini klabu ya Simba iandae mechi ya kirafiki timu ya Taifa ikicheza?

Jibu hoja au hujaielewa.....wachezaji wa Simba wangechaguliwa ktk Timu ya Taifa hii mechi ya saa moja ingekuwepo!? Ndipo mtoa hoja anapotatizwa....?

yes ingekuwepo kwani simba ina wachezaji 6 tu? Au jana kwa dakika 90 wamecheza hao ambao waliiitwa na stars?
 
Tatizo uko kwenye dunia ya peke yako vilabu vingi tu duniani vinacheza match za kirafiki wakati timu zao za taifa zikicheza Sema muda unakuwa tofauti sio muda ule timu ya taifa inacheza kama walivyofanya simba sc na yote ni kuwa fanya wale ambao hawajaitwa kwenye team ya taifa kupasha miili joto ili kuenda sawa na wale walioitwa
 
Mechi ya simba ni mechi ya kirafiki ni kama zoezi tu,mbona Manula yupo kwenye timu ya taifa,kwani yanga mlikatazwa?wachezaji wa simba waliocheza Leo ni wale hawakuitwa taifa stars au wale walioachwa,kama nye yanga ni wazembe hamwezi kuita mechi ya kirafiki msitusumbue ndo maana mmebaki maskini timu ombaomba maana hamjitumi
Mkuu hao vyura wasikuumize kichwa ni wakupuuzwa
 
Kwanza Tuheshimu Watanzania na Badilisha Kauli Yako!!!
Hile Haikuwa Taifa Stars Bali Kilikuwa Ni Kigenge tu Cha Amunike Kilichokusanya Wachezaji Kutoka Baazi Ya Vijitimu Hapa Tz.
OK nimebadilisha kama ulivyotaka Ila nawe jifunze kuandika. Hile Ndio mini? Halafu Baazi ni kitu gani? Kajifunze kwanza kiswahili cha kuunda silabi ndio uje humu Kwa Wanaume!!!
 
OK nimebadilisha kama ulivyotaka Ila nawe jifunze kuandika. Hile Ndio mini? Halafu Baazi ni kitu gani? Kajifunze kwanza kiswahili cha kuunda silabi ndio uje humu Kwa Wanaume!!!

You are right.

Hongera sana Mwalimu wa Kiswahili usiyejua matumizi ya herufi kubwa na ndogo.
 
Nimependa wahariri was magazeti mengi ya Leo kuipotezea mechi ya Simba na Leopards.
 
Unajibiwa kulingana na mtazamo wako. Unamtazamo hasi dhidi ya Simba na mechi yao ya leo.
AFC Leopards leo wamecheza na Simba na wakati huohuo Kenya imecheza,umesikia wapi Wakenya wakilalamika dhidi ya mchezo wa leo? Jibu ni moja tu,hawana mtazamo hasi na akili finyu kama za kwako.
Duh! Kazi ipo nchi hii. Hivi hujiulizi mechi ya Simba na Leopards imechezwa wapi? Ndo maana Musyoke aliamua kutuletea mashindano ya vilabu hapa wakati wa mechi za fainali za kombe la dunia !!!!!
 
Na ndio maana mkawaambia wachezaji wenu wakiuke maagizo ya kocha wa timu ya taifa.... Ili wafukuzwe kambini waje wacheze mechi ya kirafiki... Jinga kabisa
Mkuu, kusudio la hiyo mechi lilikuwa kuifunika ile ya Stars na The Cranes. Nawashukuru wahariri wa magazeti mengi leo kuipotezea mechi hii ya chuki dhidi ya Taifa.
 
Acha ubabaishaji elewa hoja ya mtoa hoja, ameuliza Simba wachezaji wake wangeitwa Timu ya Taifa, hii mechi yao waliyoiandaa leo, wangecheza ama ingekuwepo? Ndipo panapo mtatiza, msome vizuri huenda hujamuelewa....
Mkuu, hao wanaotetea uamuzi huo watupe idadi ya mechi kwa vilabu vya Simba na Yanga ni ngapi zilichezwa siku moja na mechi za Taifa Stars.
 
Nini athari ya Simba kwa Taifa baada ya kucheza mechi ya kirafiki siku ambayo Taifa Stars anacheza?

Tena muda tofauti.
Niambie ni mechi ngapi Simba imecheza siku moja na Stars ikicheza?
 
Stars Bila Simba inawezekana
Mkuuu Simba alicheza Manula
Yanga akacheza Gadiel Michael.
Simba imeshiriki kwenye mechi kwa 100%
Yanga imeshiriki kwa 20% kwa kigezo cha wachezaji walioitwa na kutumiwa. Bandiko lako ni halina upembuzi.
 
Nimesema kama Stars wangefungwa jana....na Simba walivyoshinda jana... Lengo la Simba kuikomoa Stars lingekamilika.

Sema Dua la kuku ndio hivyo halimpati mwewe.

Jiulize hali ya Kocha wa Timu ya Taifa ingelikuwaje, lawama zingemuweka ktk mazingira gani ya kuandaa Timu kwa ajili ya mechi zijazo.

Suala la kulinda nidhamu ya wachezaji lingekuwaje, je shinikizo la kutaka afukuzwe lisingekuwepo?

Kuwa mkweli Simba walikuwa na dhamira mbaya dhidi ya Kocha na Stars kwa ujumla...

Jibu. Simba haikufanikiwa kuikomoa stars kwa kucheza jana kwa kuwa Taifa stars haikufungwa....

Next?
Mkuu, tokea sakata hili la wachezaji wa klabu ya Simba kuachwa Kaduguda kila akihojiwa yeye ni kutoa lawama tu.
 
Duh! Kazi ipo nchi hii. Hivi hujiulizi mechi ya Simba na Leopards imechezwa wapi? Ndo maana Musyoke aliamua kutuletea mashindano ya vilabu hapa wakati wa mechi za fainali za kombe la dunia !!!!!
Hebu acha kuhororoja na wewe..! Unaweza kuthibitisha pasi na shaka kuwa lengo la Simba lilikuwa hilo?
 
Nimependa wahariri was magazeti mengi ya Leo kuipotezea mechi ya Simba na Leopards.

Wacha Kujitekenya Wewe! Kwani Mechi imechezwa Magazetini?
Hebu Search Hapa JF, Twitter, FB na Insta uone Ni Nyuzi na Post Ngapi Zilizoizungumzia Mechi Hii Ya Simba vs FC Leopard (Kuisifu/Kuilaumu) Halagu Uhesabu na Zilizoizungumzia Taifa Stars Yenu uone Ni Mechi ipi iliyouza Kwenye Mitandao na Media.

Acha umbulula sisi Mpira tumecheza uwanjani na si kwenye Dimba wala Mwanasport au Nipashe.

This is Simba
 
Wakuu, nimetatizwa na uamuzi wa uongozi wa klabu ya Simba kuandaa mechi ya kirafiki na timu ya AFC Leopards tena ikichezwa hapa nchini wakati timu yetu ya Taifa ikicheza katika mashindano na timu ya taifa ya Uganda.
Najiuliza hivi wachezaji wao wangechaguliwa kuchezea timu yetu ya Taifa mechi hii ingekuwepo?
Huu ni mzaha mkubwa.
Mzaha gani kwani mechi ya simba imezuia mechi ya timu ya taifa kutochezwa? Acheni wivu watani.
 
Back
Top Bottom