Lanlady
JF-Expert Member
- Feb 27, 2019
- 1,836
- 6,303
Sio kwamba hatutaki kutozwa kodi.
Swali la msingi la kujiuliza ni kwanini makato yawe zaidi ya mara moja kwa kipato kimoja?
Mshahara unakatwa kodi (PAYE), bank husika wanakata service charge. Wakati wa kutoa unakatwa salio la kutolea. Na bado serikali ikate tena tozo. Huu ni uonevu.
Tumevumilia kwenye tozo za miamala ya simu, ila hili la bank HAPANA!
NI UONEVU! Hata kama kiasi ni kidogo ila kwanini kitozwe zaidi ya mara moja?
Kama nchi inapitia wakati mgumu, kwanini wasiuze magari ya serikali na kupunguza ziara na misafara isiyo na ulazima? Mbona hatuoni jitihada za makusudi za kubana matumizi ya serikali kwa kuondoa vikao na mikutano ya ana kwa ana na kufanya kwa njia isiyo ya ana kwa ana (zoom, video conference) ili kubana matumizi?
Ina maana njia pekee ya kukusanya mapato ni kupitia tozo?
Ni nani amewaambia kuwa wananchi wana fedha nyingi? Ilihali mfumuko wa bei uko juu! Gharama za maisha ziko juu. Wananchi wanalalamika kila iitwapo leo.
Tozo na kodi mara mbili kwa kipato hichohicho kimoja, ni uonevu!