Kwanini kujenga nyumba imekuwa ni fashion kwa Watanzania?

Hujamuelewa mleta uzi hatakataa kujenga ila jenga ukiwa ushazungusha hela yako mara kadhaa yaani kama una biashara tayari ushazungusha faida hata mara kumi ndo uanze kujenga ili kukuza mtaji.
Kichwa cha habari cha huu uzi kinajieleza. Kama kujenga nyumba ni fasheni basi ni fasheni nzuri sana.
 
Hata kama unafanya biashara kumiliki ardhi na kujenga ni muhimu sana. Wajanja wote kwenye biashara wako mstari wa mbele kumiliki ardhi na kujenga.
Kumiliki ardhi ni jambo la msingi ila kuanza kujenga ni risk Sana itakayokufanya usiishi maisha bora na usifikie kufikia ndoto zako kwa wakati Mimi ni kijana chini ya miaka 30 nimfanyabiahara ninamiliki ardhi na nimeona umuhimu wakumiliki ardhi lakini kujenga ni risk Sana pale ambapo hauna msingi wa kujenga nashauri Sana kwanini usianze kujenga vyumba kazaa
 
Hufikirii gharama anazokwepa za kuama na kodi zitatumika kuongeza mapato?
 
Jambo jema Ila ungefanya mpango wa kumiliki ardhi tu ardhi inapanda thamani kila miaka kazaa

Mtu akiona ana mtaji wa huo anaona kashatoboa kumbe mtaji mdogo ambao hautakiwi kufanya shughuli nyingine mtu ana kata mill 7 anaanza kuporomosha jengo mwisho biashara huwa haidanganyi bidhaa dukani zinaanza kuadimika wateja wanakukimbia na ndio inakuwa mwanzo wa biashara yako kufa ndio chanzo cha kuwa masikini huku umejenga
 
Sasa unataka tusijenge tuishi kama manyani kwenye miti? Unajua kero za Kodi wewe? Hivi ukitokea msiba na wewe mpangaji umefiwa utakaa wapi? Masuala mengine sio ya kuyaandika mbele za watu dogo.
Kwani hao ambao sasa hivi wanapanga hawapati misiba? Ulipopanga ndio kwako kwa kipindi uluchopanga iwe msiba au sherehe unafanyia hapo hapo.
 
Bro unaishi TZ hii hiii?
Kuna mfalme mmoja alipewa taarifa kwamba wananchi wanaandamana,hawana chakula,mikate ya kula,mfalme akashangaa akawaambie wasaidizi wake kama hawana mikate,wapeni keki!!!
Huyu alikua juha kweli kweli,watu walikuwa hawana mikate,maisha ni magumu,mfslme akafikiri watu wameichoka mikate hakujua hali halisi ya maisha ya ufukara ya watu.
 
Watu wengi wamempinga mleta maada sababu hawakutaka kushughurisha akili zao. Kiukweli kujenga nyumba while bado huna sehemu ya kukuingizia kipato, mfano biashara ni uoga wa maisha. Hili nilikuja kulielewa tayari nimeshachelewa acha tuishi humo humo. Ila kumbuka nyumba ya kuishi si Assets Otherwise ujenge upangishe
 
Risk ya biashara hapa kwetu ni kubwa kuliko kujenga nyumba..

biashara hazitabiriki hapa nchini so bora ujenge tu ujue pesa umeizika..
 
Akili za kushindwa hizi.



Sent from my 2201117SG using JamiiForums mobile app
 

Na wanao panga nyumba kwann wasifikirie kumiliki nyumba zao?

Au ni sawa dereva amiliki gari yake na kinyozi salon yake lakini wapangaji wasimiliki nyumba zao?
 
Kama ulishawahi kukaa nyumba za kupanga,ukakutana na adha za wenye nyumba, lazima ukipata vihela uvikimbize kwenye ujenzi wa nyumba ya kuishi...
 
Wewe umejenga stoo ngapi. Usikute unatupa ushauri ukiwa unaishi kwa shemeji yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…