Kwanini kuna juhudi kubwa za kuhakikisha kuwa Mbowe haendelei kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA

Fundi Mchundo

Platinum Member
Joined
Nov 9, 2007
Posts
10,448
Reaction score
8,705
Hii ni ndefu kwa hiyo kwa wale ambao kusoma para zaidi ya moja ni mtihani wala wasianze kuisoma.

Kuna wanachama na wafuasi wa CHADEMA pamoja na wapinzani wengine wa chama tawala ambao wanaamini kwa dhati kuwa ni wakati muafaka wa kubadilisha approach ya kuleta mabadiliko kwa sababu inayotumika sasa hivi kwa kiasi kikubwa haijafanikiwa.

Wanaamini hii ni kwa sababu Mbowe hawezi kumudu tactics ambazo ni aggresive na confrontational za wakati huo. Na chachu ya tactics hizo itatokana nje ya taratibu za kawaida kama tulivyoona vijana wa nchi jirani walivyotumia tik tok n.k.

Mambo haya yote hayaendani na hulka ya Mbowe ambayo kwa kiasi fulani ni ya traditional politics. Hawa walihitaji kiongozi ambae hana uvumilivu kama wao. Kiongozi ambae yuko tayari kwenda "mano a mano" na serikali bila kujali consequences.

Kwa mtazamo wao Lissu ndio kiongozi anaewafaa. Kwa sababu walimwona Mbowe kama kizingiti kwao wakatumia tactics za kumuaibisha na kumbeza ili aone hahitaji hizo fedheha ajitoe. Bahati mbaya kwao walikuwa hawajamsoma Mbowe vizuri. Hawakujua tactics hizo ndio zitamfanya aone chama chake kinataka kuwa hijacked kihuni.

Kitu vingine ambacho hawakuzingatia ni kuwa watanzania wengi hawapendi confrontation na hivyo kuna uwezekano mdogo wa wao kujitokeza kwa wingi kujiunga nao. Kingine ni kuwa tactic kama hizi hazileti matokeo ya kudumu na mara nyingi zinakuwa hijacked na wana siasa na kufa kifo cha kimya kimya. Tumeona Kenya. Tumeona Malawi. Hata Tunisia na Misri.

Ubaya mwingine ni kuwa ni vigumu ku control ili vurugu zisitawale. Picha za vijana wakiwa wana warushia mawe hazina tija.

Amandla...
 
Aidha, kuna wale wa upande wa pili ambao wanatambua kuwa Mbowe ni hatari kwa wao kuendelea kutawala kuliko Lissu. Hii ni kwa sababu Mbowe amejenga structure ambayo ina uwezo mkubwa wa resilience dhidi ya changamoto nyingi. Chama chake kimeweza ku prosper hata baada ya kuondokewa na wanachama wake waliokuwa wanaonekana mahiri. Kuanzia wakina Kabourou, Zitto, Slaa, hadi Msigwa. Wakaondoka viongozi wapiganaji kama Halima lakini hakikutetereka. Tumeona jinsi yule dada wa Dodoma alivyopambana. Au Aidan anavyopambana akiwa peke yake Bungeni na kwa kweli bila support kubwa ya chama chake. Hata pale kilipokataa kupokea ruzuku hakikutetereka. Huu ni ushahidi wa talent ya Mbowe ya kuibua na kulea vipaji vipya pamoja na kuleta mshikamano katika chama chake. Hii ni tofauti na Lissu ambae hajaweza kujenga infrastructure yake mwenyewe na haijulikani kama ana uwezo wa kukijenga chama chake kama kitabomolewa.
Hawa mbinu wanayoitumia kuhakikisha Mbowe hashindi ni tofauti na ile ya wafuasi wa Lissu. Hawa wanamsifia sana Mbowe na kuhakikisha kuwaonyesha watanzania kuwa wao wanamkubali kuliko Lissu. Of course, yote haya yanajenga hisia kuwa Mbowe ameunga juhudi. Aidha, mtu yeyote ambae ni kipenzi wa CCM hataweza kuchukua maamuzi magumu dhidi ya CCM. Kwa sababu hiyo wafuasi wa Chadema watamgeukia Lissa na kumtelekeza Mbowe ambae wana hisi kuwa ni kibaraka wa mbaya wao. Wakifanya hivyo lengo la wabaya wao litatimia. Faida nyingine kwa wapinzani wao ni kuvunjika kwa ushirikiano ambao kwa kweli ulikuwa formidable. Vipande vitakavyo baki havitakuwa na nguvu waliyokuwa nayo awali.

Amandla...
 
Hii ni ndefu kwa hiyo kwa wale ambao kusoma para zaidi ya moja ni mtihani wala wasianze kuisoma.

Kuna wanachama na wafuasi wa CHADEMA pamoja na wapinzani wengine wa chama tawala ambao wanaamini kwa dhati kuwa ni wakati muafaka wa kubadilisha approach ya kuleta mabadiliko kwa sababu inayotumika sasa hivi kwa kiasi kikubwa haijafanikiwa.

Wanaamini hii ni kwa sababu Mbowe hawezi kumudu tactics ambazo ni aggresive na confrontational za wakati huo. Na chachu ya tactics hizo itatokana nje ya taratibu za kawaida kama tulivyoona vijana wa nchi jirani walivyotumia tik tok n.k.

Mambo haya yote hayaendani na hulka ya Mbowe ambayo kwa kiasi fulani ni ya traditional politics. Hawa walihitaji kiongozi ambae hana uvumilivu kama wao. Kiongozi ambae yuko tayari kwenda "mano a mano" na serikali bila kujali consequences.

Kwa mtazamo wao Lissu ndio kiongozi anaewafaa. Kwa sababu walimwona Mbowe kama kizingiti kwao wakatumia tactics za kumuaibisha na kumbeza ili aone hahitaji hizo fedheha ajitoe. Bahati mbaya kwao walikuwa hawajamsoma Mbowe vizuri. Hawakujua tactics hizo ndio zitamfanya aone chama chake kinataka kuwa hijacked kihuni.

Kitu vingine ambacho hawakuzingatia ni kuwa watanzania wengi hawapendi confrontation na hivyo kuna uwezekano mdogo wa wao kujitokeza kwa wingi kujiunga nao. Kingine ni kuwa tactic kama hizi hazileti matokeo ya kudumu na mara nyingi zinakuwa hijacked na wana siasa na kufa kifo cha kimya kimya. Tumeona Kenya. Tumeona Malawi. Hata Tunisia na Misri.

Ubaya mwingine ni kuwa ni vigumu ku control ili vurugu zisitawale. Picha za vijana wakiwa wana warushia mawe hazina tija.

Amandla...

Swali hili lingekuwa hivi:

Kwa nini kuna juhudi kubwa sana za kuhakikisha Mbowe anaendelea kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA?​

CCM wanataka Mbowe abaki kwenye chama kama mwenyekiti,wanachadema wa kawaida wanataka Lissu aingie kama mwenyekiti ili anasue chama kilipokwama.Mbowe kwa miaka 20+ ametumia mbinu zote alizoweza,lakini hakuna mafanikio yanayoleta tija kwa wanachadema ambao kwa namna moja ama nyingine wamekua wakishuhudia watu kupotea na wengine kupatikana wakiwa wameuawa.
CCM mwanzoni walipiga kelele kua Mbowe kakaa muda mrefu,atoke na hawakujua nani ambaye anger badili,kwani walijua mbadala wake atakua dhaifu kuliko yeye Mbowe,alipojitokeza Lissu,CCM wakageukia kwa Mbowe wakimsihi aendelee na serikali yote bilashaka itakua imemhakikishia sapoti ya hali na mali.
Angalia leo polisi walivyolinda maandamano yake,utajua jambo.
 
Hili swali lingekuwa hivi:

Kwa nini kuna juhudi kubwa sana za kuhakikisha kuwa Mbowe anaendelea kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA?​

Haujakatazwa kuuliza swali ambalo unadhani ndio lingekuwa sahihi. Unaweza kuanzisha uzi wako unao uliza swali lako. Au ni yale yale ya kupenda mteremko?

Amandla..
 
Wanaamini hii ni kwa sababu Mbowe hawezi kumudu tactics ambazo ni aggresive na confrontational za wakati huo. Na chachu ya tactics hizo itatokana nje ya taratibu za kawaida kama tulivyoona vijana wa nchi jirani walivyotumia tik tok n.k.
This is very true。
Mambo haya yote hayaendani na hulka ya Mbowe ambayo kwa kiasi fulani ni ya traditional politics. Hawa walihitaji kiongozi ambae hana uvumilivu kama wao. Kiongozi ambae yuko tayari kwenda "mano a mano" na serikali bila kujali consequences.
true
Kwa mtazamo wao Lissu ndio kiongozi anaewafaa. Kwa sababu walimwona Mbowe kama kizingiti kwao
true
wakatumia tactics za kumuaibisha na kumbeza ili aone hahitaji hizo fedheha ajitoe.
not true
Bahati mbaya kwao walikuwa hawajamsoma Mbowe vizuri. Hawakujua tactics hizo ndio zitamfanya aone chama chake kinataka kuwa hijacked kihuni.
true
Kitu vingine ambacho hawakuzingatia ni kuwa Watanzania wengi hawapendi confrontation na hivyo kuna uwezekano mdogo wa wao kujitokeza kwa wingi kujiunga nao.
Not true,Watanzania wengi wanataka mabadiliko,baada ya kujaribu njia za amani kwa miaka 25 kushindikana,2025 ni mwaka wa 30,wana opt tujajiribu the confrotation way!,Tundu Lissu is the man for that na sio Sultani Mbowe!
Kingine ni kuwa tactic kama hizi hazileti matokeo ya kudumu na mara nyingi zinakuwa hijacked na wana siasa na kufa kifo cha kimya kimya.
true
Tumeona Kenya. Tumeona Malawi. Hata Tunisia na Misri.
true
Ubaya mwingine ni kuwa ni vigumu ku control ili vurugu zisitawale.
true
Picha za vijana wakiwa wana warushia mawe hazina tija.

Amandla...
Asante
P
 
Hili swali lingekuwa hivi:

Kwa nini kuna juhudi kubwa sana za kuhakikisha kuwa Mbowe anaendelea kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA?​

Acha ujinga. Ukweli ni kwamba hata kabla ya Mbowe kuchukua fomu mlikuwa mnamshambulia sana Mbowe. Hakuna mtu yeyote aliyepo upande wa Mbowe ambaye amehoji kitendo cha Lissu kugombea nafasi ya uenyekiti. Acha ujinga
 
Hii ni ndefu kwa hiyo kwa wale ambao kusoma para zaidi ya moja ni mtihani wala wasianze kuisoma.

Kuna wanachama na wafuasi wa CHADEMA pamoja na wapinzani wengine wa chama tawala ambao wanaamini kwa dhati kuwa ni wakati muafaka wa kubadilisha approach ya kuleta mabadiliko kwa sababu inayotumika sasa hivi kwa kiasi kikubwa haijafanikiwa.

Wanaamini hii ni kwa sababu Mbowe hawezi kumudu tactics ambazo ni aggresive na confrontational za wakati huo. Na chachu ya tactics hizo itatokana nje ya taratibu za kawaida kama tulivyoona vijana wa nchi jirani walivyotumia tik tok n.k.

Mambo haya yote hayaendani na hulka ya Mbowe ambayo kwa kiasi fulani ni ya traditional politics. Hawa walihitaji kiongozi ambae hana uvumilivu kama wao. Kiongozi ambae yuko tayari kwenda "mano a mano" na serikali bila kujali consequences.

Kwa mtazamo wao Lissu ndio kiongozi anaewafaa. Kwa sababu walimwona Mbowe kama kizingiti kwao wakatumia tactics za kumuaibisha na kumbeza ili aone hahitaji hizo fedheha ajitoe. Bahati mbaya kwao walikuwa hawajamsoma Mbowe vizuri. Hawakujua tactics hizo ndio zitamfanya aone chama chake kinataka kuwa hijacked kihuni.

Kitu vingine ambacho hawakuzingatia ni kuwa watanzania wengi hawapendi confrontation na hivyo kuna uwezekano mdogo wa wao kujitokeza kwa wingi kujiunga nao. Kingine ni kuwa tactic kama hizi hazileti matokeo ya kudumu na mara nyingi zinakuwa hijacked na wana siasa na kufa kifo cha kimya kimya. Tumeona Kenya. Tumeona Malawi. Hata Tunisia na Misri.

Ubaya mwingine ni kuwa ni vigumu ku control ili vurugu zisitawale. Picha za vijana wakiwa wana warushia mawe hazina tija.

Amandla...
Watanzania wengi hawajui kufanya siasa zenye manufaa kwa taifa.
 
1. Yesu Kristu alikuwa seremala.
2. Mtume Mohammed S.A.W alikuwa hajui kusoma.
3. Malcolm X elimu yake aliipatia jela.
4. Robert Nesta Marley hakwenda shule.
5. Karume hakufika Chuo Kikuu
6. Kleist Sykes hakufika Chuo Kikuu

KatIka hao uliosema wana Ph.D nani anawafikia hata 1/1000 hawa ambao hawakuwa wasomi?

Wewe endelea tu kuabudu Ph.D.

Amandla...
 
Pascal Mayalla
Unasema hajabezwa halafu hapo hapo unamuita Sultan?
Unadhani ile saga ya Wenja ilimuhusu nani? Ni nani, kama sio Mwenyekiti wa Chama? Hayo maneno ya pesa ya Abdul yalimlenga Mbowe 100%.
Mnachonishangaza ni hiyo amnesia ya kujifanya kuwa hizo confrontational tactics hazijawahi kutumiwa na uongozi wa Mbowe. Kifo cha yule mwanafunzi aliyeuawa kwenye basi hakikutokea kwenye picnic ya Chadema.
Mbowe na wenzake walitiwa ndani kwa kile kilichodaiwa kuwa wanakiuka amri halali.
Mbowe na wenzake waliitisha maandamano kupinga matokeo ya uchaguzi wa 2000 lakini watanzania walipoona askari wanafagia wakanywea.
Mbowe alitangaza mpaka tarehe ya maandamano ya kupinga mauaji, upoteaji wa watu n.k ( mambo ambayo utadhani wale wote revolushenaries wangeguswa) wakatokea Mbowe, binti yake na wakina Hilda tu. Wale wote waliokuwa wanatamba humu ndani hawakuonekana. Labda kama walikuwa wameji camouflage kama bodaboda.
Hata wakati wa uchaguzi uliopita. Ukiondoa mashujaa kama yule dada wa Dodoma wengi waliishia kutuma clips na picha walizochukua kwa kujificha.
Watu wa aina hii ndio unataka kutuaminisha kuwa wanamsubiri Lissu aite lamgambo ndio wajitokeze!
Sasa hizo mbinu mpya za confrontational politics ni zipi? Au safari hii watabeba mawe wakiongozwa na jemadari wao?
Hizo zote ni ndoto tu. Hazitatokea.

Amandla...

Pascal Mayalla
 
Acha ujinga. Ukweli ni kwamba hata kabla ya Mbowe kuchukua fomu mlikuwa mnamshambulia sana Mbowe. Hakuna mtu yeyote aliyepo upande wa Mbowe ambaye amehoji kitendo cha Lissu kugombea nafasi ya uenyekiti. Acha ujinga

Kwa hiyo uelevu wako ni kuona kwamba Mbowe ndiye mwenye haki miliki ya kuwa mwenyekiti wa cdm
 
Watoto wa Mama.jpg

After 20 years hana Jipya anafanya Siasa zile zile zilizoiua CUF na sasa CHADEMA.

Labda kama anataka kufia kwenye Uenyekiti.
working-to-death-business-mans-skeleton-using-laptop-in-office.jpg
 
1. Yesu Kristu alikuwa seremala.
2. Mtume Mohammed S.A.W alikuwa hajui kusoma.
3. Malcolm X elimu yake aliipatia jela.
4. Robert Nesta Marley hakwenda shule.
5. Karume hakufika Chuo Kikuu
6. Kleist Sykes hakufika Chuo Kikuu

KatIka hao uliosema wana Ph.D nani anawafikia hata 1/1000 hawa ambao hawakuwa wasomi?

Wewe endelea tu kuabudu Ph.D.

Amandla...
7 mbowe ana uchu wa pesa na madaraka
 
Back
Top Bottom