Kwanini kuna juhudi kubwa za kuhakikisha kuwa Mbowe haendelei kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA

Hii ni ndefu kwa hiyo kwa wale ambao kusoma para zaidi ya moja ni mtihani wala wasianze kuisoma.

Kuna wanachama na wafuasi wa CHADEMA pamoja na wapinzani wengine wa chama tawala ambao wanaamini kwa dhati kuwa ni wakati muafaka wa kubadilisha approach ya kuleta mabadiliko kwa sababu inayotumika sasa hivi kwa kiasi kikubwa haijafanikiwa.

Wanaamini hii ni kwa sababu Mbowe hawezi kumudu tactics ambazo ni aggresive na confrontational za wakati huo. Na chachu ya tactics hizo itatokana nje ya taratibu za kawaida kama tulivyoona vijana wa nchi jirani walivyotumia tik tok n.k.

Mambo haya yote hayaendani na hulka ya Mbowe ambayo kwa kiasi fulani ni ya traditional politics. Hawa walihitaji kiongozi ambae hana uvumilivu kama wao. Kiongozi ambae yuko tayari kwenda "mano a mano" na serikali bila kujali consequences.

Kwa mtazamo wao Lissu ndio kiongozi anaewafaa. Kwa sababu walimwona Mbowe kama kizingiti kwao wakatumia tactics za kumuaibisha na kumbeza ili aone hahitaji hizo fedheha ajitoe. Bahati mbaya kwao walikuwa hawajamsoma Mbowe vizuri. Hawakujua tactics hizo ndio zitamfanya aone chama chake kinataka kuwa hijacked kihuni.

Kitu vingine ambacho hawakuzingatia ni kuwa watanzania wengi hawapendi confrontation na hivyo kuna uwezekano mdogo wa wao kujitokeza kwa wingi kujiunga nao. Kingine ni kuwa tactic kama hizi hazileti matokeo ya kudumu na mara nyingi zinakuwa hijacked na wana siasa na kufa kifo cha kimya kimya. Tumeona Kenya. Tumeona Malawi. Hata Tunisia na Misri.

Ubaya mwingine ni kuwa ni vigumu ku control ili vurugu zisitawale. Picha za vijana wakiwa wana warushia mawe hazina tija.

Amandla...

Hivi unaamini kwamba Mbowe ndiye aliyeletaaridhiano yaliyopo au yaliyokuwepo Tanzania ?

Maridhiano ya Mbowe yamesaidia nini kama mwaka mmoja tu baadae Uchaguzi unageuka kuwa vita na wanaouawa ni Wanyonge wasiopesawa Rushwa za Bandari .

Wahenga walikua sio wajinga waliposema amani haiji ila kwa ncha ya Upanga.

Wewe kwa akili yako ndogo kama ya Mbowe unadhani kuna siku Tanzania itakua na katiba mpya ya kupewa mezani na Tume huru itakayowakosesha mamia ya wabunge na madiwani wa CCM nafasi kwenye karatasi za kura halali ?

Kama Mbowe hawezi kuachia chama chake ambacho kinategemea Ruzuku na hamasa ya wanachama pekee itakuaje kwa CCM kuachia nchi ya Tanganyika yenye Rasilimali nyingi kuliko zote Afrika mashariki na kusini kwa Afrika ?Yaani Mbowe anganganie KITI kisicho na benki kuu wala jeshi wala kusaini mamikataba ya madini ,ardhi n.k. iwe Serikali ya CCM ikubali kuachia hata mbunge mmoja aondokane na ulaji mkubwa na utajiri unaopatikana Fasta ndani ya serikali na bunge.?

Kwanza jiulize ni mbunge yupi au diwani yupi wa CCM aliyeko tayari kuachia nafasi yake kwa wapinzani?
Jibu ni hakuna na hatakuwepo milele,iwe ni kwa maridhiano au mawizihao?

Sasa siasa kama hizo unaridhiana nini kama sio ghiliba za Rushwa anazofanya Mbowe .?

Maridhiano yaliyoleta matokeo changa yalikua ni yale ya Maalim Seif na Serikali mpaka wakagawana nafsi ndani ya serikali . Hayakuja kwa kuendekeza Rushwa bali ni uadilifu unaopewa nuru na Mungu ili kuinua watu na kupigania taifa lao.

Kwenye hii Chadema ya Rushwa na Mbowe kamwe haitapata kibali mbele za Mungu na watu hawawezi hata kuandamana maana Hakuna roho ya haki inayotoka kwa Mungu ndani yao.
PAKIWA NA HAKI BILA RUSHWA KWA WANASIASA MUNGU ANAINUA WATU WENYE UWEZO WA KUANDAMANA NA HATA KUWATOA WAOVU MADARAKANI . Mbowe amepoteza kibali kwa Mungu hawezi kamwe kuwavuta WATU labda atumie fedha na yeye anafikiria wananchi wanamkubali kama enzi za Dr. Slaa alikua anatangulia mbele na mke wake wanapigwa mpaka anavunjwa mkono na watu wanasonga mbele . Ni kwa sababu ya Haki ya kiMungu iliyokua ndani yake. Sasa leo hii hata Samia kwa mfano na serikali yake tulivaliwa na Rwanda au Malawi tutapigwa kwa sababu watawala wanaua uzalendo . Itabidi Jeshi lipambane peke yao bila kusaidiana na wananchi kwa kujitolea kama enzi ya vita ya Uganda
 
Umenipoteza uliposema kuwa nina akili ndogo. Lakini kwa kweli sielewi hata unachotaka kusema maana uko " all over the place".

Amandla..
 
CCM wanataka Mbowe abaki kwenye chama kama mwenyekiti,wanachadema wa kawaida wanataka Lissu aingie kama mwenyekiti ili anasue chama kilipokwama.Mbowe kwa miaka 20+ ametumia mbinu zote alizoweza,lakini hakuna mafanikio yanayoleta tija kwa wanachadema ambao kwa namna moja ama nyingine wamekua wakishuhudia watu kupotea na wengine kupatikana wakiwa wameuawa.
CCM mwanzoni walipiga kelele kua Mbowe kakaa muda mrefu,atoke na hawakujua nani ambaye anger badili,kwani walijua mbadala wake atakua dhaifu kuliko yeye Mbowe,alipojitokeza Lissu,CCM wakageukia kwa Mbowe wakimsihi aendelee na serikali yote bilashaka itakua imemhakikishia sapoti ya hali na mali.
Angalia leo polisi walivyolinda maandamano yake,utajua jambo.
Huo ndo ukweli mkuu,walitaraji atakae mrithi mbowe atakuwa dhaifu kuzidi mbowe,kumbe sasa wamejikuta wamepigwa chenga hatari!!!,,haijapata kutoka !!,,ndo maana kelele zimekuwa nyiiingii sana,mi namwomba lissu na wanaomuunga mkono wasigeuke nyuma,ili wasije wakawa mawe.
 
Ubaya mwingine ni kuwa ni vigumu ku control ili vurugu zisitawale. Picha za vijana wakiwa wana warushia mawe hazina tija.

Amandla...
Sijasoma sehemu ya pili hapo chini, lakini nililo soma huku juu ni andiko hafifu sana hili.

Mbowe hana 'tactic' mpya nyingine tena, na wala hizo za zamani zinazo julikana hazina uzito wowote wa kuleta mabadiliko tena chini ya CCM.
Kilicho baki, na kiko wazi kabisa, ni kwamba Mbowe kajiondoa kabisa kwenye mapambano ya kuleta mabadiliko kwa njia nyingine yoyote; sasa kaamua afanye biashara akitumia chama alicho kiongoza kwa muda mrefu.
Hiyo dhana ya 'confrntational' mnayo itanguliza mbele sasa ni vitishio tu; vya kuwatisha watu. Hakuna yeyote anaye pingana na Mbowe aliye tamka kwamba chama kitakapo pata uongozi tofauti na wa Mbowe "vita" itakuwa ime tangazwa.
Kwa mfano: Inapo semwa kuwa hapatakuwepo na uchaguzi kama hapatakuwepo na mabadiliko kuruhusu uchaguzi huru na wa haki; hii mtu mwenye akili timamu ataiita kuwa ni hatuwa 'confrontational'?
Kama uchaguzi unavurugwa kwa maksudi na hao wanaotaka ushindi wa lazima; kwa nini wasilaumiwe wao kuwa ndio wanao sababisha 'confrontation', na badala yake alaumiwe anaye tafuta kuzuia uhalifu?

Hivi nyinyi watu kweli mnazo akili timamu bado; au njaa zenu zimewafanya mkose akili kabisa?

Mfano wa pili: ime kwisha dokezwa, kwamba kuna umuhimu mkubwa wa kukipeleka chama kwa wananchi, wananchi waelewe maana na sababu ya uwepo wa chama hiki na wakielewa wawe ndio wasukuma mabadiliko. Hii nayo ni kuwa 'confrontational'?
Kukaa kwa Mbowe madarakani miaka ishirini, kashindwa kabisa kuwavuta wananchi waone kwamba chama kipo kwa maslahi yao na kwa nchi nzima; sasa wananchi hao unaotaka wajitokeze wakapambane na polisi, kwa manufaa ya nani, ya Mbowe?
halafu unageuka hapa na kuanza kuwalaumu wananchi kuwa siyo waKenya sijui wa wapi huko! Mlaumu Mbowe, aliye shindwa kazi ya kuwashawishi wananchi..

Na sasa, kama atalazimisha kwa kutumia mbinu alizo jifunza kwa wafadhili wake huko CCM, achukuchue uchaguzi ili abaki madarakani; huo ndio utakuwa mwisho wa CHADEMA tuijuayo.
 
With all due respect, I don't agree with you. Hivi ni nani dhaifu kuliko Mbowe ambae walitegemea atamrithi wakati Makamu wake ni Lissu! Hakuna mtu alie mzuia Lissu kugombea lakini pamekuwa na shinikizo la ajabu la kumtaka Mbowe ajitoe hata kabla hajatangaza nia ya kugombea. Aidha, haushangai kuona CCM wakimsupport Mbowe waziwazi na kwa sauti kubwa. Unadhani hawajui kwa kufanya hivyo wanawaaminisha watu kama wewe kuwa Mbowe ni kibaraka wao na hivyo kuwafanya mumgeuke? Lissu angetangaza kugombea Uenyekiti bila kuwaachia surrogates wake wamchafue Mbowe wote tungefurahia kuwa Chadema inaonyesha maturity kwa kuwa na viongozi wao wawili wa juu kabisa na ambao wana mvuto mkubwa katika chama wanagombea kwa kuheshimiana bila kuchafuana. Aige mfano wa Mbowe ambae hawakuchelea kumtaka kiongozi aliyemkashifu Lissu aombe radhi. Na akaomba radhi.

Lakini haiwezekani kuwa watu wanaodai kuheshimu demokrasia wanafanya kila juhudi ili mtu wao asishandane na mtu atakayempa ushindani. Hivi mtu wao akishinda, atafanya nini katika uchaguzi ujao ambapo hatakuwa na mpinzani mwenye stature ya Mbowe. Kama kweli ana nia nzuri na chama chake, Lissu anatakiwa aupoze moto na awahakikishie wafuasi wake kuwa hata kama atashindwa Chadema itabakia salama. Kama hawezi kusema hivyo basi ni heri aseme wazi kuwa hatabaki katika Chadema ya Mwenyekiti Mbowe.

Amandla...
 
Hii ni ndefu kwa hiyo kwa wale ambao kusoma para zaidi ya moja ni mtihani wala wasianze kuisoma.

Kuna wanachama na wafuasi wa CHADEMA pamoja na wapinzani wengine wa chama tawala ambao wanaamini kwa dhati kuwa ni wakati muafaka wa kubadilisha approach ya kuleta mabadiliko kwa sababu inayotumika sasa hivi kwa kiasi kikubwa haijafanikiwa.

Wanaamini hii ni kwa sababu Mbowe hawezi kumudu tactics ambazo ni aggresive na confrontational za wakati huo. Na chachu ya tactics hizo itatokana nje ya taratibu za kawaida kama tulivyoona vijana wa nchi jirani walivyotumia tik tok n.k.

Mambo haya yote hayaendani na hulka ya Mbowe ambayo kwa kiasi fulani ni ya traditional politics. Hawa walihitaji kiongozi ambae hana uvumilivu kama wao. Kiongozi ambae yuko tayari kwenda "mano a mano" na serikali bila kujali consequences.

Kwa mtazamo wao Lissu ndio kiongozi anaewafaa. Kwa sababu walimwona Mbowe kama kizingiti kwao wakatumia tactics za kumuaibisha na kumbeza ili aone hahitaji hizo fedheha ajitoe. Bahati mbaya kwao walikuwa hawajamsoma Mbowe vizuri. Hawakujua tactics hizo ndio zitamfanya aone chama chake kinataka kuwa hijacked kihuni.

Kitu vingine ambacho hawakuzingatia ni kuwa watanzania wengi hawapendi confrontation na hivyo kuna uwezekano mdogo wa wao kujitokeza kwa wingi kujiunga nao. Kingine ni kuwa tactic kama hizi hazileti matokeo ya kudumu na mara nyingi zinakuwa hijacked na wana siasa na kufa kifo cha kimya kimya. Tumeona Kenya. Tumeona Malawi. Hata Tunisia na Misri.

Ubaya mwingine ni kuwa ni vigumu ku control ili vurugu zisitawale. Picha za vijana wakiwa wana warushia mawe hazina tija.

Amandla...
Nilijiandaa kusoma makala ndefu..!
 
Sijasoma sehemu ya pili hapo chini, lakini nililo soma huku juu ni andiko hafifu sana hili.

Mbowe hana 'tactic' mpya nyingine tena, na wala hizo za zamani zinazo julikana hazina uzito wowote wa kuleta mabadiliko tena chini ya CCM.
Kilicho baki, na kiko wazi kabisa, ni kwamba Mbowe kajiondoa kabisa kwenye mapambano ya kuleta mabadiliko kwa njia nyingine yoyote; sasa kaamua afanye biashara akitumia chama alicho kiongoza kwa muda mrefu.
Hiyo dhana ya 'confrntational' mnayo itanguliza mbele sasa ni vitishio tu; vya kuwatisha watu. Hakuna yeyote anaye pingana na Mbowe aliye tamka kwamba chama kitakapo pata uongozi tofauti na wa Mbowe "vita" itakuwa ime tangazwa.
Kwa mfano: Inapo semwa kuwa hapatakuwepo na uchaguzi kama hapatakuwepo na mabadiliko kuruhusu uchaguzi huru na wa haki; hii mtu mwenye akili timamu ataiita kuwa ni hatuwa 'confrontational'?
Kama uchaguzi unavurugwa kwa maksudi na hao wanaotaka ushindi wa lazima; kwa nini wasilaumiwe wao kuwa ndio wanao sababisha 'confrontation', na badala yake alaumiwe anaye tafuta kuzuia uhalifu?

Hivi nyinyi watu kweli mnazo akili timamu bado; au njaa zenu zimewafanya mkose akili kabisa?

Mfano wa pili: ime kwisha dokezwa, kwamba kuna umuhimu mkubwa wa kukipeleka chama kwa wananchi, wananchi waelewe maana na sababu ya uwepo wa chama hiki na wakielewa wawe ndio wasukuma mabadiliko. Hii nayo ni kuwa 'confrontational'?
Kukaa kwa Mbowe madarakani miaka ishirini, kashindwa kabisa kuwavuta wananchi waone kwamba chama kipo kwa maslahi yao na kwa nchi nzima; sasa wananchi hao unaotaka wajitokeze wakapambane na polisi, kwa manufaa ya nani, ya Mbowe?
halafu unageuka hapa na kuanza kuwalaumu wananchi kuwa siyo waKenya sijui wa wapi huko! Mlaumu Mbowe, aliye shindwa kazi ya kuwashawishi wananchi..

Na sasa, kama atalazimisha kwa kutumia mbinu alizo jifunza kwa wafadhili wake huko CCM, achukuchue uchaguzi ili abaki madarakani; huo ndio utakuwa mwisho wa CHADEMA tuijuayo.
Umerudia tena kutumia lugha zisizokuwa na staha. Hilo neno "confrontational politics" limetumika na mmoja wa supporters wa Lissu akidai hizo ndio politics za wakati huu na anayeziweza ni Lissu peke yake na sio Mbowe.

Unasema Mbowe ameacha kupambana na serikali wakati ni hivi karibuni tu aliita maandamano dhidi ya serikali hiyo hiyo kupinga matendo yanayoendelea nchini. Ni huyo huyo Mbowe aliposikia viongozi wenzake wamefanyiwa fujo Mbeya alienda kule haraka na akakamatwa na kurudishwa Dar. Huyo huyo Mbowe alitumia lugha kali wakati wa msiba wa Mzee Kibao kwa Masauni. Au kilichowaumiza ni yeye kuzuia watu wasimpopoe Masauni?

Unapata wapi nguvu ya kusema kuwa wananchi ambao kila kukicha wanaona ndugu zao wanapotea walishindwa kujitokeza kwa sababu Mbowe hakuwahamasisha? Walitaka awape kibahasha ndio waandamane?

Kifo cha Chadema kimetabiriwa kwa miaka mingi mno. Na hata hili litapita. Hata Mbowe akibaki madarakani na watu wachache, wenye moyo watakijenga tena. Hivi hauoni unapoji contradict kwa kuanza kuweka mazingira ya kumnyooshea kidole Mbowe kama mtu wenu atashindwa. Kama hamna imani na uchaguzi ujao mshaurini mtu wenu ajitoe maana kuna vyama vingi tuu ambavyo vina demokrasia iliyokomaa zaidi ya CDM. Sisi wengine tutamkubali yeyote atakayetangazwa mshindi na tutawaachia wana Chadema waungane nae katika kujenga chama chao. Katika demokrasia sio lazima mtu unayemtaka wewe ashinde.

Amandla...
 
Umerudia tena kutumia lugha zisizokuwa na staha. Hilo neno "confrontational politics" limetumika na mmoja wa supporters wa Lissu akidai hizo ndio politics za wakati huu na anayeziweza ni Lissu peke yake na sio Mbowe.
mimi nilikusoma wewe, na nikakutana na neno hilo likiungana na uliyo yaandika wewe; huyo unaye mzungumzia pembeni hayo siyajui.

Hata kama hilo neno hukulianzisha wewe, lakini hoja zako zote zinalielezea hilo hilo kuhusu upande unao mpinga Mbowe.

Mkuu 'Fundi', ni hivi: utahangaika sana kuleta maandiko ya kumsifu sana Mbowe, lakini Mbowe mwenyewe kisha jiharibia sifa na kujiondolea heshima mwenyewe.
Mbowe kwa sasa hawezi kamwe kujitofautisha kwa vyovyote na tunao waona kule CCM.
Sasa, kama ataendelea kuongoza CHADEMA, chama hicho hakitakuwa na tofauti yoyote na hiyo CCM yenyewe.
Hiyo ndiyo hali halisi.
 
Hivi unaamini kwamba Mbowe ndiye aliyeletaaridhiano yaliyopo au yaliyokuwepo Tanzania ?

Maridhiano ya Mbowe yamesaidia nini kama mwaka mmoja tu baadae Uchaguzi unageuka kuwa vita na wanaouawa ni Wanyonge wasiopesawa Rushwa za Bandari .

Wahenga walikua sio wajinga waliposema amani haiji ila kwa ncha ya Upanga.

Wewe kwa akili yako ndogo kama ya Mbowe unadhani kuna siku Tanzania itakua na katiba mpya ya kupewa mezani na Tume huru itakayowakosesha mamia ya wabunge na madiwani wa CCM nafasi kwenye karatasi za kura halali ?

Kama Mbowe hawezi kuachia chama chake ambacho kinategemea Ruzuku na hamasa ya wanachama pekee itakuaje kwa CCM kuachia nchi ya Tanganyika yenye Rasilimali nyingi kuliko zote Afrika mashariki na kusini kwa Afrika ?Yaani Mbowe anganganie KITI kisicho na benki kuu wala jeshi wala kusaini mamikataba ya madini ,ardhi n.k. iwe Serikali ya CCM ikubali kuachia hata mbunge mmoja aondokane na ulaji mkubwa na utajiri unaopatikana Fasta ndani ya serikali na bunge.?

Kwanza jiulize ni mbunge yupi au diwani yupi wa CCM aliyeko tayari kuachia nafasi yake kwa wapinzani?
Jibu ni hakuna na hatakuwepo milele,iwe ni kwa maridhiano au mawizihao?

Sasa siasa kama hizo unaridhiana nini kama sio ghiliba za Rushwa anazofanya Mbowe .?

Maridhiano yaliyoleta matokeo changa yalikua ni yale ya Maalim Seif na Serikali mpaka wakagawananafsi ndani ya serikali . Hayakuja kwa kuendekeza Rushwa bali ni uadilifu unaopewa nuru na Mungu ili kuinua watu na kupigania taifa lao.

Kwenye hii Chadema ya Rushwa na Mbowe kamwe haitapata kibali mbele za Mungu na watu hawawezi hata kuandamana maana Hakuna roho ya haki inayotoka kwa Mungu ndani yao.
PAKIWA NA HAKI BILA RUSHWA KWA WANASIASA MUNGU ANAINUA WATU WENYE UWEZO WA KUANDAMANA NA HATA KUWATOA WAOVU MADARAKANI . Mbowe amepoteza kibali kwa Mungu hawezi kamwe kuwavuta WATU labda atumie fedha na yeye anafikiria wananchi wanamkubali kama enzi za Dr. Slaa alikua anatangulia mbele na mke wake wanapigwa mpaka anavunjwa mkono na watu wanasonga mbele . Ni kwa sababu ya Haki ya kiMungu iliyokua ndani yake. Sasa leo hii hata Samia kwa mfano na serikali yake tulivaliwa na Rwanda au Malawi tutapigwa kwa sababu watawala wanaua uzalendo . Itabidi Jeshi lipambane peke yao bila kusaidiana na wananchi kwa kujitolea kama enzi ya vita ya Uganda
Amina baba mchungaji
 
mimi nilikusoma wewe, na nikakutana na neno hilo likiungana na uliyo yaandika wewe; huyo unaye mzungumzia pembeni hayo siyajui.

Hata kama hilo neno hukulianzisha wewe, lakini hoja zako zote zinalielezea hilo hilo kuhusu upande unao mpinga Mbowe.

Mkuu 'Fundi', ni hivi: utahangaika sana kuleta maandiko ya kumsifu sana Mbowe, lakini Mbowe mwenyewe kisha jiharibia sifa na kujiondolea heshima mwenyewe.
Mbowe kwa sasa hawezi kamwe kujitofautisha kwa vyovyote na tunao waona kule CCM.
Sasa, kama ataendelea kuongoza CHADEMA, chama hicho hakitakuwa na tofauti yoyote na hiyo CCM yenyewe.
Hiyo ndiyo hali halisi.
Siko hapa kubishana na mtu. Ungekuwa na nia ya mjadala ungesoma hilo neno nimelitoa wapi.

Mimi namsifu Mbowe na ninatambua mchango wake mkubwa kwa CDM. Wewe inaelekea hautambui umuhimu wake na unaona bora aondoke. Ni mtizamo wako na tukubali kutofautiana na tuishie hapo.

Kwangu mimi mjadala na wewe umeishia hapa.

Amandla...
 
Kuna jambo moja ambalo linanishangaza. Hata kabla Mbowe hajatangaza nia ya kugombea, humu ndani mlijaza sababu za kwa nini huu ni wakati wa yeye kurithiwa na Lissu. Baadhi ya sababu hizo ni:
1. Amekaa mno katika Uenyekiti kwa hiyo itakuwa vyema asipongombea ili dhana ya Uenyekiti wa kudumu iondoke.
2. Ni mzee, kwa hiyo mambo ya siku hizi hayawezi.
3. Ni mfanyabiashara na priority yake ni biashara zake kuliko chama. Hiyo inamfanya kuwa mpole kwa watawala kwa sababu analinda biashara zake.
4. Ni mpole na muoga kwa hiyo hawezi kutetea maslahi ya chama na taifa lake. Badala yake anainyenyekea mno serikali.
5. Anaitumia CDM kama Saccos yake na wale anaowapenda.
6. Ni corrupt. Amehongwa na utawala uliopo.
7. Ni mkabila na amegeuza CDM chama cha wachaga.
8. Hakubali mtu yeyote agombee nafasi yake. Yuko hata tayari kuua kulinda nafasi yake.
9. Alihusika katika COVID-19 kuingia Bungeni. Sasa hivi ana mpango wa kuwarudisha CDM. Akishinda atawarudisha.

Kinacho ni shangaza ni kuwa pamoja na mapungufu haya makubwa wafuasi wa Lissu wanafanya kila jitihada ili asigombee. Ningedhani kumshinda mtu muovu kama huyu ingekuwa kama kumsukumiza mlevi maana tunaambiwa ushahidi upo.

Wengine wanasema ana watu wake watakaomsaidia kushinda. Kama mnajua hivyo si hakikisheni kuwa uchaguzi unafanyika katika mazingira ya uwazi na haki sawa kwa wagombea wote?

Na hata kama ni hivyo, mimi ningedhani kwa vile watakaopiga kura wanawajua kwa undani wagombea wote ( kuliko sisi ambao tunawaona kwenye luninga) basi itakuwa rahisi kuwa convince wamteme mtu muovu.

Badala yake waliungana na wapinzani wao kuleta figisu figisu ili asichukue fomu za kugombea.

Au hawana imani kuwa mtu wao atashinda mbele ya watu wanaowajua?

Amandla...
 
So long as katiba ya chama chao inawapa wote haki ya kugombea, I don't see any reason ya watu kipigizana kelele.
 
Lyatonga Mrema alipogombea urais wengi waliamini kuwa ataiondoa CCM. Watu walimwamini kutokana na matendo yake kukemea dhulma alipokuwa serikalini. Watu wakawa wanasukuma gari lake kuonyesha mapenzi yao. Mwalimu aka caution kuwa Mrema bado. Sio presidential material. Watu wakampuuza na kuendelea kumshangilia Messiah Mrema. Muda umethibitisha kuwa Mwalimu alikuwa sahihi.
Slaa alipokuwa KM wa CDM alibeba hisia za wananchi kwa kukemea maovu bila uoga wowote. Lakini nae alipotoka CDM na kufanywa Balozi akawa mtetezi wa serikali iliyokuwa madarakani. Nakumbuka alisema kuwa Ulaya ukiisha uchaguzi mambo ya mikutano nayo inaisha. Inawezekana alisema yale kwa sababu alikuwa mtumishi wa umma lakini credibility yake ilikuwa affected.
Kwa kweli inabidi tuwe makini tunapompigia mtu debe.

Amandla...
 
Mtu kakaa miaka 20+ Bado anataka tu hapana, ajaribu kwanza mwingine
 
Huo ndo ukweli mkuu,walitaraji atakae mrithi mbowe atakuwa dhaifu kuzidi mbowe,kumbe sasa wamejikuta wamepigwa chenga hatari!!!,,haijapata kutoka !!,,ndo maana kelele zimekuwa nyiiingii sana,mi namwomba lissu na wanaomuunga mkono wasigeuke nyuma,ili wasije wakawa mawe.
Mkuu its quite opposite, CCM wana strategy ya kutaka weak Chadema ikiwa watalazimika kufanya fair play kwenye siasa za ushindani 2025 tunapoelekea uchaguzi mkuu.
Na kombora mmojawapo la maagamizi kutoka chama tawala ni misinformation aka alternative facts ikiwalenga Chadema.
Watu wale wale wa chama kile kile waliomkejeli Mbowe kuwa ni kiganganizi kukaa miaka 20 akiwa mwenyekiti ghafla anapewa airtime ya TBC na ulinzi wa mikutano na polisi bila yeye kuomba !!!
CCM ina mkono mrefu,inatengeneza bonge la movie,inayowafanya waongeze washabiki,wapenzi na wanachama wa Chadema wanamuone Mbowe kama msaliti.
Hata wale waliokuwa hawamtaki Lissu wamemezwa na kimbunga cha Mbowe must go.
Wakisha mchinja Mbowe kwenye sanduku la kura sio muda mrefu makomredi wa Chadema (people's power)ndipo watagundua wamedanganywa kwa hila.

Mbowe alifikiri ni business as usual kumbe.... nadhani ameshtuka lakini kachelewa sana.
Yajayo yana.......
 
Mbowe alifikiri business as usual nadhani ameshtuka lakini kachelewa sana.
Yajayo yana.......
Mbowe atakasiki hata kwa jiki.
 
Back
Top Bottom