Kwanini kuna juhudi kubwa za kuhakikisha kuwa Mbowe haendelei kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA

Kwanini kuna juhudi kubwa za kuhakikisha kuwa Mbowe haendelei kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA

Vijana hawa wanamuagiza Mwenyekiti wao aende akawaambie kwa nini watu wanamtukana Lissu. Lakini angalia mtu mzima alivyoileta hoja hiyo hiyo.

Amandla...
 
Hii ni ndefu kwa hiyo kwa wale ambao kusoma para zaidi ya moja ni mtihani wala wasianze kuisoma.

Kuna wanachama na wafuasi wa CHADEMA pamoja na wapinzani wengine wa chama tawala ambao wanaamini kwa dhati kuwa ni wakati muafaka wa kubadilisha approach ya kuleta mabadiliko kwa sababu inayotumika sasa hivi kwa kiasi kikubwa haijafanikiwa.

Wanaamini hii ni kwa sababu Mbowe hawezi kumudu tactics ambazo ni aggresive na confrontational za wakati huo. Na chachu ya tactics hizo itatokana nje ya taratibu za kawaida kama tulivyoona vijana wa nchi jirani walivyotumia tik tok n.k.

Mambo haya yote hayaendani na hulka ya Mbowe ambayo kwa kiasi fulani ni ya traditional politics. Hawa walihitaji kiongozi ambae hana uvumilivu kama wao. Kiongozi ambae yuko tayari kwenda "mano a mano" na serikali bila kujali consequences.

Kwa mtazamo wao Lissu ndio kiongozi anaewafaa. Kwa sababu walimwona Mbowe kama kizingiti kwao wakatumia tactics za kumuaibisha na kumbeza ili aone hahitaji hizo fedheha ajitoe. Bahati mbaya kwao walikuwa hawajamsoma Mbowe vizuri. Hawakujua tactics hizo ndio zitamfanya aone chama chake kinataka kuwa hijacked kihuni.

Kitu vingine ambacho hawakuzingatia ni kuwa watanzania wengi hawapendi confrontation na hivyo kuna uwezekano mdogo wa wao kujitokeza kwa wingi kujiunga nao. Kingine ni kuwa tactic kama hizi hazileti matokeo ya kudumu na mara nyingi zinakuwa hijacked na wana siasa na kufa kifo cha kimya kimya. Tumeona Kenya. Tumeona Malawi. Hata Tunisia na Misri.

Ubaya mwingine ni kuwa ni vigumu ku control ili vurugu zisitawale. Picha za vijana wakiwa wana warushia mawe hazina tija.

Amandla...
Kwanini Kuna juhudi kubwa ya kumzuia na kumponda Lissu juu ya kugombea UMWENYEKITI??

umepata jibu, leta Uzi mwingine 🤔🤔🤔
 
With all due respect, I don't agree with you. Hivi ni nani dhaifu kuliko Mbowe ambae walitegemea atamrithi wakati Makamu wake ni Lissu! Hakuna mtu alie mzuia Lissu kugombea lakini pamekuwa na shinikizo la ajabu la kumtaka Mbowe ajitoe hata kabla hajatangaza nia ya kugombea. Aidha, haushangai kuona CCM wakimsupport Mbowe waziwazi na kwa sauti kubwa. Unadhani hawajui kwa kufanya hivyo wanawaaminisha watu kama wewe kuwa Mbowe ni kibaraka wao na hivyo kuwafanya mumgeuke? Lissu angetangaza kugombea Uenyekiti bila kuwaachia surrogates wake wamchafue Mbowe wote tungefurahia kuwa Chadema inaonyesha maturity kwa kuwa na viongozi wao wawili wa juu kabisa na ambao wana mvuto mkubwa katika chama wanagombea kwa kuheshimiana bila kuchafuana. Aige mfano wa Mbowe ambae hawakuchelea kumtaka kiongozi aliyemkashifu Lissu aombe radhi. Na akaomba radhi.

Lakini haiwezekani kuwa watu wanaodai kuheshimu demokrasia wanafanya kila juhudi ili mtu wao asishandane na mtu atakayempa ushindani. Hivi mtu wao akishinda, atafanya nini katika uhaguzi ujao abapo hatakuwa na mpinzani mwenye stature ya Mbowe. Kama kweli ana nia nzuri na chama chake, Lissu anatakiwa aupoze moto na awahakikishie wafuasi wake kuwa hata kama atashindwa Chadema kitabakia salama. Kama hawezi kusema hivyo basi ni heri aseme wazi kuwa hatabaki katika Chadema ya Mwenyekiti Mbowe.

Amandla...
Miaka kumi ya mwisho ya Mbowe kwenye chaguzi za local 2014/2024, Chadema imepata uwakilishi chini ya 1%... Uchaguzi Mkuu 2020 Chadema ilipata mbunge mmoja wa kuchaguliwa. Kwa vipimo vyote kwa namna siasa za CCM zilivyobailika ni ukweli kuwa Mbowe hawezi kutuvusha
 
Hakuna mtu alie mzuia Lissu kugombea lakini pamekuwa na shinikizo la ajabu la kumtaka Mbowe ajitoe hata kabla hajatangaza nia ya kugombea.
Ni kosa kumzuia asigombee. Huo utakuwa utamaduni wa CCM na Fomu moja. Ni afya kwa chama kuwa na 'incumbent vs Challenger'' . Hiyo ingelikuwa demokrasia ya hali ya juu.
Aidha, haushangai kuona CCM wakimsupport Mbowe waziwazi na kwa sauti kubwa.
CCM hawampendi TAL kwasababu hizi. Mbowe ni 'moderate'' TAL ni extremist.
CCM wangependa mtu wanayeweza kucheza cheza naye mezani kama ''Maridhiano' yalivyopoteza muda wa kudai Katiba. CCM wanamhofia sana TAL kwa misimamo mikali isiyoyumba
Lissu angetangaza kugombea Uenyekiti bila kuwaachia surrogates wake wamchafue Mbowe wote tungefurahia kuwa Chadema inaonyesha maturity kwa kuwa na viongozi wao wawili wa juu kabisa na ambao wana mvuto mkubwa katika chama wanagombea kwa kuheshimiana bila kuchafuana.
Ukweli ni kwamba walioanza ni ''Chawa' wa Mbowe! Trick hizi wamezitumia katika nyakati tofuati, bahati mbaya nyakati ni tofuati. Ukifuatilia kwa makini tatizo lilikuwa kumlinda M/kiti
Natamani yasingetokea ili uwe mfano wa demokrasia nchini.
Aige mfano wa Mbowe ambae hawakuchelea kumtaka kiongozi aliyemkashifu Lissu aombe radhi. Na akaomba radhi.
Hapana! ile ilikuwa mbaya sana ! hata Vijana wa Mbowe waliona ni mbaya! Ilimlazimu Mbowe
Lakini haiwezekani kuwa watu wanaodai kuheshimu demokrasia wanafanya kila juhudi ili mtu wao asishandane na mtu atakayempa ushindani.
Nashangaa sana, Chama cha Demokrasia lazima kionyeshe kwa vitendo.
Kuwa na Wagombea katika ballot box kwa njia za kistaarabu ni maturity na inajenga confidence.
Hii ni missed opportunity kwa Chadema! so sad

JokaKuu
 
CCM hawampendi TAL kwasababu hizi. Mbowe ni 'moderate'' TAL ni extremist. CCM wangependa mtu wanayeweza kucheza cheza naye mezani kama ''Maridhiano' uyalivyopoteza muda wa kudai Katiba.
CCM wanamhofia sana TAL
Mimi sikubaliani kuwa CCM wanamuogopa TAL kuliko Mbowe. TAL ni mtu wa kwenye majukwaa na anachukua misimamo ambayo inawasaidia sana CCM. Kwa mfano kugoma kuingia kwenye majadiliano ya maridhiano while itawafurahisha watu wake lakini kwa wengine ( hasa mataifa ya nje) ataonekana unreasonable. Mbowe amekubali kuingia kwenye majadiliano hayo na yamefanikisha kuachiwa wanachama waliokuwa ndani, viongozi wenzake muhimu ( akiwemo Lissu kuweza kurudi kuongeza nguvu katika mapambano yao) kuruhusiwa mikutano ya hadhara na kufungua njia ya wao kupokea ruzuku. CCM walikuwa hawana jinsi bali kukubali haya ili wasionekane kuwa wao ndio unreasonable. Baada ya kufanikisha haya, Mbowe ameweza kujitoa kwenye hayo majadiliano bila kuonekana kuwa yeye ni mkorofi na unreasonable. Wangesusa kama alivyotaka Lissu yote haya yasingepatikana na mbaya zaidi wanachama zaidi ya mia wangeendelea kusota rumande au jela.
Mbowe amekubali kuingia kwenye uchaguzi akijua thika kuwa watendaji wa CCM watafanya walioyazoea. Sasa akigoma kuingia katika uchaguzi mkubwa ujao ataeleweka. Asingeingia CCM wangeweza kudai kuwa uchaguzi ungekuwa wa haki ila ni uoga wa CDM. Sasa hivi wameshindwa hata kushangilia ushindi wao wa kishindo.
CCM wamekiri kuwa walianza mazungumzo na Msigwa mapema tu. Mbowe alipopata fununu hakusita kumshughulikia kama alivyowashughulikia wakina Sumaye, Mashinji na Nyalambu. CCM wanajua hadanganyiki kirahisi na nyuma ya zile tabasamu ni mtu ruthless linapokuja masuala ya chama chake. Ndio maana strategists wanafanya kila mbinu kuhakikisha Lissu anashinda ikiwa ni pamoja na kumsifia sana Mbowe ili watu waamini amenunuliwa na wasimpigie kura. Mbowe ni hatari zaidi mara 100 kwa CCM kuliko Lissu.

Amandla...
 
Ukweli ni kwamba walioanza ni ''Chawa' wa Mbowe! Trick hizi wamezitumia katika nyakati tofuati, bahati mbaya nyakati ni tofuati. Ukifuatilia kwa makini tatizo lilikuwa kumlinda M/kiti
Natamani yasingetokea ili uwe mfano wa demokrasia nchini.
Sio kweli. Juhudi za kumchafua Mbowe zilianza mapema tu. Alianza Msigwa kwa kutangaza vita ya wazi wazi against Mbowe. Lissu akawa anachochea moto kwa kuzungumzia in public kuhusu uozo ulioko CDM. Wengine tukaanza kujiuliza kuwa inakuaje Makamu Mwenyekiti anaona mahali pekee pa kucriticize chama chake ni in public. He overplayed his hand alipoleta hadithi yake ya kutunga kuhusu Wenje na Abdul na viongozi wengine ( wink wink) waliopokea mshiko kutoka Abdul.

Hapo ndipo vijana wanaomjua Mbowe nq waliokuwa privy na yaliyotokea wakaona enough is enough. Hasa baada ya kuona machawa wa Lissu wakimshambulia Mbowe kwa kila aina ya lugha za kejeli na kebehi. Kumbuka hata kabla hajatangaza uamuzi wake walianza kumuita king'ang'anizi na fisadi. Hao vijana unaowaita chawa wakaona na wao wamwage mboga. Kumbuka hawa vijana ndio wanajua kwa karibu mchango wa Mbowe kuliko sisi tulio nje. Huyo Ntobi na vijana wenzake walikuwa kila mara wanawatembelea watu wa CDM waliokuwa rumande na jela. Hao ndio walikuwa wanahudhuria vikao vyao. Guess who alikuwa anawawezesha kufanya hivyo. Wakati huo huyu revolutionary activist eminent hakuwahi kusimamia hata kesi moja iliyowahusu wale vijana. Halafu wamsikie akiinsinuate kuwa Mbowe ni weak! Lazima wakasirike. Lakini Mbowe akawaambia wasifanye hivyo kitu ambacho Lissu anapata kigugumizi kuwaambia watu wake.

Wahenga walisema, usiache mbachao kwa msala upitie. Na ile nyingine kuwa " all that glitters is not gold".

Amandla....
 
Mimi sikubaliani kuwa CCM wanamuogopa TAL kuliko Mbowe.
Jaribio la kumuua TAL lilifanyika kwasababu hakukuwepo na namna ya kumdhibiti.
Akiwa Bungeni aliongea katika misingi ya sheria, hawakuweza kumfukuza
Akiwa nje ya Bunge aliongea katika misingi ya sheria, kesi zilizofunguliwa zilishindikana kumwadhibu

CCM wanampenda FAM kwasababu wana uwezo wa ku buy time naye.
Mathalan, suala la COVID-19 halikupaswa kufika lilipofika.
Handling
yake ilikuwa poor katika hali ile ile ya FAM kuwa moderate. COVID wanamaliza Bunge!

Suala la Maridhiano, ilikuwa ku buy time wakati wanatafuta muda. Walipounda kamati ya Mkandala maridhiano yakafa kwasababu tayari walikuwa na position
TAL ni mtu wa kwenye majukwaa na anachukua misimamo ambayo inawasaidia sana CCM. Kwa mfano kugoma kuingia kwenye majadiliano ya maridhiano ataonekana unreasonable. Mbowe amekubali kuingia kwenye majadiliano hayo na yamefanikisha kuachiwa wanachama waliokuwa ndani, viongozi wenzake muhimu ( akiwemo Lissu kuweza kurudi kuongeza nguvu katika mapambano yao) kuruhusiwa mikutano ya hadhara na kufungua njia ya wao kupokea ruzuku.
Wakati Mbowe (FAM) amekamatwa kutokana na vugu vugu la kudai Katiba.
Pressure ilikuwa kubwa Nchini. Mkutano wa Mwanza alikokamatwa FAM ulikuwa wa Katiba.

FAM akiwa Magereza kwa miezi 8 Wanachama wa CDM na hapa credit kwa Vijana walikuwa mikoani wakieleza umuhimu wa Katiba. FAM akipelekwa Mahakamani wafuasi walijazana Kisutu si kutaka aachiwe bali kudai Katiba Mpya. Nyimbo na ujasiri wa kuwakabili FFU haukuzungumzia Mbowe, ilikuwa Katiba Mpya.

Pressure ilimtisha CCM na Serikali, kwamba, baada ya miezi 8 FAM akiwa ndani moto wa Katiba unawaka nje.
Ilikuwa dhahiri kumfunga FAM kungechochea Katiba. Mbinu iliyotumika ni '' Keep your fiend close and your enemies closer''. Maridhiano yakaasisiwa

Maridhiano ni reconciliation! swali, CDM waligombana na nani?
Huwezi kuwa Victim ukaomba reconciliation.

Kutokana na pressure ya Wanachama FAM alikuwa katika position ya ''strength'' ndio maana alipoachiwa Magereza aliitwa Ikulu kumvunja nguvu kwa kumweleza '' tulia tuongee''. FAM akaingia '' Kingi''

Je maridhiano ni kitu kibaya? Jibu ni hapana, ingawa definition ni awkward tukubaliane tu kwamba ''CDM na CCM walikoseana'' na walihitaji maridhiano.

Watu wanakwenda kwenye maridhiano katika' position of strength wakiwa na bargaining chip .
Katiba mpya ndiyo 'chip' yenyewe. Mbowe kuachiwa, Wafungwa na ruzuku ni haki. Kudai katiba ndilo tatizo

Kosa alilofanya FAM na kumfanya awe weak kuanzia hapo ni hili la kutoka Magereza na kwenda Ikulu wakati Wanachama wake wanamsubiri mahakamani.

Kwenda Ikulu wakati hajakutana na Viongozi wenzake waliokuwa nje na wanaojua hali ya kisiasa.
In essence FAM alionekana very weak mbele ya wenzake na leo tunajua walimpinga!

Hili la kumpinga kwa kura ni matokeo ya weakness aliyoonyesha.

Maridhiano aliyoasisi victim Mbowe yaliua hoja ya Katiba na CCM wakawa na muda wa kutengeneza kamati ya Mkandala. Kamati ya Mkandala ilipopata political legitimacy, maridhiano yakafa , FAM akapoteza kila kitu.

CCM wanataka mtu kama FAM kwasababu for almost 15 years kuanzia zama za JK, wanacheza naye mezani.

CCM walikuwa hawana jinsi bali kukubali haya ili wasionekane kuwa wao ndio unreasonable. Baada ya kufanikisha haya, Mbowe ameweza kujitoa kwenye hayo majadiliano bila kuonekana kuwa yeye ni mkorofi na unreasonable. Wangesusa kama alivyotaka Lissu yote haya yasingepatikana na mbaya zaidi wanachama zaidi ya mia wangeendelea kusota rumande au jela.
Mbowe amekubali kuingia kwenye uchaguzi akijua thika kuwa watendaji wa CCM watafanya walioyazoea. Sasa akigoma kuingia katika uchaguzi mkubwa ujao ataeleweka. Asingeingia CCM wangeweza kudai kuwa uchaguzi ungekuwa wa haki ila ni uoga wa CDM. Sasa hivi wameshindwa hata kushangilia ushindi wao wa kishindo.
CCM wamekiri kuwa walianza mazungumzo na Msigwa mapema tu. Mbowe alipopata fununu hakusita kumshughulikia kama alivyowashughulikia wakina Sumaye, Mashinji na Nyalambu. CCM wanajua hadanganyiki kirahisi na nyuma ya zile tabasamu ni mtu ruthless linapokuja masuala ya chama chake. Ndio maana strategists wanafanya kila mbinu kuhakikisha Lissu anashinda ikiwa ni pamoja na kumsifia sana Mbowe ili watu waamini amenunuliwa na wasimpigie kura. Mbowe ni hatari zaidi mara 100 kwa CCM kuliko Lissu.

Amandla...
 
Jaribio la kumuua TAL lilifanyika kwasababu hakukuwepo na namna ya kumdhibiti.
Akiwa Bungeni aliongea katika misingi ya sheria, hawakuweza kumfukuza
Akiwa nje ya Bunge aliongea katika misingi ya sheria, kesi zilizofunguliwa zilishindikana kumwadhibu

CCM wanampenda FAM kwasababu wana uwezo wa ku buy time naye.
Mathalan, suala la COVID-19 halikupaswa kufika lilipofika.
Handling
yake ilikuwa poor katika hali ile ile ya FAM kuwa moderate. COVID wanamaliza Bunge!

Suala la Maridhiano, ilikuwa ku buy time wakati wanatafuta muda. Walipounda kamati ya Mkandala maridhiano yakafa kwasababu tayari walikuwa na position

Wakati Mbowe (FAM) amekamatwa kutokana na vugu vugu la kudai Katiba.
Pressure ilikuwa kubwa Nchini. Mkutano wa Mwanza alikokamatwa FAM ulikuwa wa Katiba.

FAM akiwa Magereza kwa miezi 8 Wanachama wa CDM na hapa credit kwa Vijana walikuwa mikoani wakieleza umuhimu wa Katiba. FAM akipelekwa Mahakamani wafuasi walijazana Kisutu si kutaka aachiwe bali kudai Katiba Mpya. Nyimbo na ujasiri wa kuwakabili FFU haukuzungumzia Mbowe, ilikuwa Katiba Mpya.

Pressure ilimtisha CCM na Serikali, kwamba, baada ya miezi 8 FAM akiwa ndani moto wa Katiba unawaka nje.
Ilikuwa dhahiri kumfunga FAM kungechochea Katiba. Mbinu iliyotumika ni '' Keep your fiend close and your enemies closer''. Maridhiano yakaasisiwa

Maridhiano ni reconciliation! swali, CDM waligombana na nani?
Huwezi kuwa Victim ukaomba reconciliation.

Kutokana na pressure ya Wanachama FAM alikuwa katika position ya ''strength'' ndio maana alipoachiwa Magereza aliitwa Ikulu kumvunja nguvu kwa kumweleza '' tulia tuongee''. FAM akaingia '' Kingi''

Je maridhiano ni kitu kibaya? Jibu ni hapana, ingawa definition ni awkward tukubaliane tu kwamba ''CDM na CCM walikoseana'' na walihitaji maridhiano.

Watu wanakwenda kwenye maridhiano katika' position of strength wakiwa na bargaining chip .
Katiba mpya ndiyo 'chip' yenyewe. Mbowe kuachiwa, Wafungwa na ruzuku ni haki. Kudai katiba ndilo tatizo

Kosa alilofanya FAM na kumfanya awe weak kuanzia hapo ni hili la kutoka Magereza na kwenda Ikulu wakati Wanachama wake wanamsubiri mahakamani.

Kwenda Ikulu wakati hajakutana na Viongozi wenzake waliokuwa nje na wanaojua hali ya kisiasa.
In essence FAM alionekana very weak mbele ya wenzake na leo tunajua walimpinga!

Hili la kumpinga kwa kura ni matokeo ya weakness aliyoonyesha.

Maridhiano aliyoasisi victim Mbowe yaliua hoja ya Katiba na CCM wakawa na muda wa kutengeneza kamati ya Mkandala. Kamati ya Mkandala ilipopata political legitimacy, maridhiano yakafa , FAM akapoteza kila kitu.

CCM wanataka mtu kama FAM kwasababu for almost 15 years kuanzia zama za JK, wanacheza naye mezani.
Awali ya yote, nakushukuru kwa response iliyokuwa measured na civil. Kitu ambacho ni adimu sana siku hizi.

Nadhani katika hili tunaweza kuwa bogged down kwenye semantics.

Tuanze na suala la Covid-19. What were the options? Mass mobilization? Kwa watu ambao wakisikia tu kesho wanajeshi wanafanya usafi hawatoki nje? Mimi personally naamini Mbowe alitaka kuwa lenient kwa wakina Halima. Lakini wenzake walipomtilia ngumu, aliwakubalia na mpaka sasa hivi hajabadilisha msimamo. Hiyo sio sign ya dictator kama Lissu anavyotaka kum portray.

Issue ya reconciliation nimeizungumzia. Mbowe amekaa ndani muda mrefu na kwa kweli juhudi za wakina Martin na wakina mama wa Bawacha zilisaidia sana kuweka presha kwa serikali. Ametoka, ameitwa na Rais ulitaka afanye nini? A sulk na kwenda nyumbani au aende kumsikiliza halafu arudi kuwa brief wenzake kuhusu mazungumzo yake. Alipoenda bila shaka hakujua anaitiwa nini. Labda aliitwa kuombwa radhi kwa yaliyompata n.k. Sasa angeongeaje na wenzake kabla ya kujua nia ya Rais. Alipotoka kwenye huo wito, aliieleza Kamati Kuu kuhusu yaliyosibu. According to Lissu ni yeye, Msigwa, Heche, Lema, Wenje na mwingine ndio walikuwa vehemently against hicho kitu. Mimi sijui ukubwa wa Kamati Kuu lakini nadhani ina wajumbe zaidi ya 12 hivyo hawakuwa majority. Ilikuwa ni haki ya Mwenyekiti kuwa na mawazo tofauti nao na kujaribu wengine waungane nae. Hata pamoja na hayo Heche akawa mjumbe wa CDM katika hayo majadiliano na bila shaka alikuwa atoa taarifa kwa wenzake kuhusu yanayoendelea. Sasa kama Lissu aliendele kubeza waziwazi uamuzi wa Kamati Kuu na kumnyooshea kidole Mwenyekiti anashangaa nini kama Mwenyekiti anaamua kujitenga nae?

Kitu kingine ambacho tunafichwa na hatuambiwi bayana hali ilivyokuwa katika coffers za chama. Mawakili waliokuwa wakiwatetea Mbowe na wanachama wenzake sio cheap. Na wakati ule chama hakipokei ruzuku. Bila shaka Mbowe na mtu kama Mnyika walitambua hiyo situation sio sustainable. Ningependa kujua kiasi ambacho kilichokusanywa na kila mjumbe wa Kamati Kuu ili kukiwezesha chama kiweze kuendelea na shughuli zake katika wakati huo mgumu. Kupatikana kwa ruzuku kulitoa relief. Lissu anasema Mbowe alilipwa hela zote alizokuwa anaidai CDM halafu ana hint kuna mikopo ya kiujanja janja iliendelea ambayo haikupata baraka za KK. Anafanya hivi bila kusema hayo madeni alilipwa lini.

Hakuna wakati CDM iliweka pembeni hoja ya Katiba Mpya. Walikataa kushiriki katika hiyo Kamati ya Mkandala kwa sababu hiyo hiyo ingawa wakati huo walikuwa mezani wakizungumza kuhusu maridhiano. Au mnataka kutuambia CDM haiwezi kutafuna big G wakati wanatembea. Kuwa hawezi kudai Katiba Mpya wakati wako mezani wakijadiliana kuhusu muafaka wa maridhiano. You don't give credit kuwa baada ya kupata baadhi ya mambo muhimu kwao na walipoona hayo mazungumzo ni dead end wakajitoa wakiwa katika stronger kuliko walivyoanza mazunguzo? Walikuwa wanaweza kufanya mikutano ya hadhara ambayo kwa kiasi kikubwa ulidhihirisha wazi nguvu ya CDM. Wangefanya walivyotaka wakina Lissu hayo yasingewezekana. Walikuwa na stream ya pesa iliyowapunguzia mzigo wa kuendesha chama.

Lissu anasema kuwa lazima kuwe na uwazi katika upatikanaji wa pesa aki conveniently sahau kuwa kuna watu wengi wenye uwezo wasingependa kujulikana kuwa wanachangia CDM.

Anasema kila mwanachama awe na uhuru wa kugombea huku akisahau bila kuwa makini hiyo ingefungua milango kwa mamluki kama rafiki yake Msigwa. Ambae, Unfortunately, CCM walisema wazi kuwa walikuwa na majidiliano nae hata kabla ya saga ya Iringa. Ninashangaa mwana mapinduzi radical huyu anaendelea kumtetea. Ningemuelewa kama Msigwa angehamia ACT Wazalendo lakini sio CCM.

Mtu yeyote anaesema kuwa CCM ingebadilisha njia na kurudisha haki ambazo ziliondoa kwa sababu Lissu na watu wa Club house wanafoka anaishi dunia nyingine. Na hizo serikali za nje ni risk averse. Hauwezi kuwaambia kuwa CCM hawaelewi lugha nyingine bila kuonyesha kuwa angalau umejaribu lugha nyingine hasa kwa sababu kuna Mwenyekiti Mpya.

Amandla...
 
Tuanze na suala la Covid-19. What were the options? Mass mobilization? Kwa watu ambao wakisikia tu kesho wanajeshi wanafanya usafi hawatoki nje? Mimi personally naamini Mbowe alitaka kuwa lenient kwa wakina Halima. Lakini wenzake walipomtilia ngumu, aliwakubalia na mpaka sasa hivi hajabadilisha msimamo. Hiyo sio sign ya dictator kama Lissu anavyotaka kum portray.
Kulikuwa na taarifa za uhakika COVID-19 wameitwa Bungeni kwa njia za ulaghai.
Habari zipo hata JF kama sikosei zikithibitika kwa namba za mawasiliano kati ya ' Wanunuzi' na COVID.

Ni kipindi CCM walinunua Wapinzani kama peremende! M/Kiti angeweza kufanya pre emptive strategy kwa kuliweka wazi hawatapeleka Wabunge! Alikaa kimya

Option ya Pili, immediately walitakiwa kutoa ushahidi kwamba COVID hawana kibali cha Chama.
Kulikuwa na dana dana (latency) na hadi walipotoa ushahidi suala lilikuwa kubwa na system ilishafanikiwa.

Tatu, Kigaila, Naibu KM Bara mkewe ni COVID. Watendaji hawawezi kuwa na conflict of interest jambo linaloeleza kwanini kulikuwa na latency katika kujibu na dilly dally. Mbowe alibanwa between a rock and a hard place! akachagua silence

Nne, COVID-19 walitakiwa wawe katika ''bargaining'' kama ilivyokuwa kwa Wafungwa, ruzuku n.k. katika maridhiano

Tano, maongezi ya kisiasa ya kila siku yalipaswa kuwahusisha COVID, Bunge na Mhakama.
Hili lingekuwa na impact katika public kama kero ! Mwenyekiti akakunja mikono ! basi mungu anaona!

Mbowe amekaa ndani muda mrefu na kwa kweli juhudi za wakina Martin na wakina mama wa Bawacha zilisaidia sana kuweka presha kwa serikali.
Ndicho kipindi pekee kilichoonyesha CDM ilikuwa ni taasisi.
M/Kiti yupo ndani, Mkamu yupo Uhamishoni, Chama kiliendelea na pressure iliyoilazimu serikali kufikiri maamuzi ya kumweka Mbowe ndani. Martin Masesa aliufahamisha Umma in real time nini kinaendelea, BAWACHA wakiwasha moto. Lazima tuwape maua yao! swali, FAM alipotoka pressure imekwenda wapi?

Ametoka, ameitwa na Rais ulitaka afanye nini? A sulk na kwenda nyumbani au aende kumsikiliza halafu arudi kuwa brief wenzake kuhusu mazungumzo yake. Alipoenda bila shaka hakujua anaitiwa nini. Labda aliitwa kuombwa radhi kwa yaliyompata n.k.
Mbowe amekiri kulikuwa na mazungumzo kati ya viongozi wa kiroho na Serikali kabla ya kuachiwa.Ni wazi alijua nini kinaendelea.

Makaburu wa South Africa walimwambia Mandela aachiwe akaishi nje bila siasa. Mandela alikataa.
Wakati mazungumzo yanaendelea Makaburu wakasema Mandela ataachiwa lakini Ulinzi wake utakuwa juu ya ANC. Uongozi wa ANC ukakataa na kuwataka makaburu wachukue dhama ya Usalama.

Mbowe alikuwa na fursa ya kumuomba Rais muda hata siku inayofuata.
Hili halikuwa suala la dharura na Mbowe alijua. Kitendo cha kuibukia Ikulu na kuwaduwaza wafuasi wake kilikera
Wafuasi wapo Kisutu ana kwa ana na FFU, Mbowe yupo Ikulu pengine na glass ya juice! Watu walikata tamaa kabisa

Mbowe alipaswa kutafuta muda wa kuongea na viongozi wenzake kabla ya kwenda hata kwa simu akiwataarifu ! hakufanya hivyo. Hakuongea na yoyote bali yeye kuibukia Ikulu kwa masuala ya Chama!

Kwenda si tatizo, approach ya kuduwaza watu ili demoralize the political base, na tunayoyaona ni vote of no confidence kwake.

Hata wenzake walipomkatalia bado alipaswa kusikiliza hoja zao.
Lakini pia Mbowe alijua political base yake haikubaliani na maridhiano! Mbowe akawaita ''Wahafidhina''

In short, Mbowe alizima moto wa Katiba. Hata pale alipotoka na kusema Vijana waendelee kudai katiba, BAVICHA walipofanya hivyo alikimbilia kuwaambia wachunge ndimi zao!

Yaani kudai katiba kunahitaji kuchunga ndimi.
BAVICHA na BAWACHA wakaacha ili kuepusha conflict na chair ! that's it!
Alipotoka kwenye huo wito, aliieleza Kamati Kuu kuhusu yaliyosibu. According to Lissu ni yeye, Msigwa, Heche, Lema, Wenje na mwingine ndio walikuwa vehemently against hicho kitu. Mimi sijui ukubwa wa Kamati Kuu lakini nadhani ina wajumbe zaidi ya 12 hivyo hawakuwa majority.
Kunaweza kuwa na Wajumbe hata 100 kwa mfano, lakini kila chama au taasis ina ''stalwart''.
Ndani ya CCM kuna akina Mangula, Kinana n.k. walikuwa na ''kura' zao hata wajumbe wengine wanaposema tofauti.

Rais Samia alisema, wakati anateuliwa kuwa Mgombea mwenza
'' Sisi katika kamati kuu baadhi tulikuwa tunakaa nje, Vingunge wanaingia ndani'' akimaanisha kuna nyakati maamuzi yalifanywa na wakubwa

Nina maana kwamba Kigaila ambaye mkewe ni COVID ana nini cha kusema ndani ya Kamati kuu?
Mnyika KM ana kipi cha kusema kwa nafasi yake ya uteuzi? Mwalimu Salum pia analipi la kusema?
Ile sekretariati inayoishi kwa kumtegemea Mbowe inaweza kuwa na kipi tofauti ?

Katika wajumbe 12 hao waliosema ni stalwart kuna wengine ni ndiyo mzee! hili ukumbuke

Kupatikana kwa ruzuku kulitoa relief. Lissu anasema Mbowe alilipwa hela zote alizokuwa anaidai CDM halafu ana hint kuna mikopo ya kiujanja janja iliendelea ambayo haikupata baraka za KK. Anafanya hivi bila kusema hayo madeni alilipwa lini.

Mtu yeyote anaesema kuwa CCM ingebadilisha njia na kurudisha haki ambazo ziliondoa kwa sababu Lissu na watu wa Club house wanafoka anaishi dunia nyingine. Na hizo serikali za nje ni risk averse. Hauwezi kuwaambia kuwa CCM hawaelewi lugha nyingine bila kuonyesha kuwa angalau umejaribu lugha nyingine hasa kwa sababu kuna Mwenyekiti Mpya.

Amandla...
Point yangu kubwa si kwamba TAL ana panacea ya matatizo, ni kwamba back lash na opposition ya M/Kiti anayopitia ni matokeo ya uongozi wake uliolega lega.

Hii revolt ni vote of no confidence na anatakiwa aende kwenye ballot box to earn the trust !
Ndio maana nasema ni vema kukawa na watu wanaogombea na washindanishe maono yao juu ya chama.
Hii habari ya kupita bila kupingwa kwa miaka 20 haina afya, inamfanya mtu asiogope nafasi yake !

Je hoja za TAL kuhusu ukomo wa madaraka, mfumo wa uchaguzi na mfumo wa fedha zina jibiwa vipi na Mwenyekiti?
Nini maono ya Mwenyekiti kwa miaka 5 ijayo?
 
Hii ndiyo JF katika ubora wake. Nasoma neno kwa neno na muda si muda nami nitatoa my two cents. Hongrereni Nguruvi3 na Fundi Mchundo, mmeturudisha zama zile za hoja hujibiwa kwa hoja.

Hata hivyo naomba nimtahadharishe ndugu yangu Fundi Mchundo, usilolijua ni kama usiku wa giza. Kila nikikusoma nakuta najiuliza umepatwa na nini, what happened to the mighty amandla?
 
Ni kosa kumzuia asigombee. Huo utakuwa utamaduni wa CCM na Fomu moja. Ni afya kwa chama kuwa na 'incumbent vs Challenger'' . Hiyo ingelikuwa demokrasia ya hali ya juu.

CCM hawampendi TAL kwasababu hizi. Mbowe ni 'moderate'' TAL ni extremist.
CCM wangependa mtu wanayeweza kucheza cheza naye mezani kama ''Maridhiano' yalivyopoteza muda wa kudai Katiba. CCM wanamhofia sana TAL kwa misimamo mikali isiyoyumba

Ukweli ni kwamba walioanza ni ''Chawa' wa Mbowe! Trick hizi wamezitumia katika nyakati tofuati, bahati mbaya nyakati ni tofuati. Ukifuatilia kwa makini tatizo lilikuwa kumlinda M/kiti
Natamani yasingetokea ili uwe mfano wa demokrasia nchini.

Hapana! ile ilikuwa mbaya sana ! hata Vijana wa Mbowe waliona ni mbaya! Ilimlazimu Mbowe

Nashangaa sana, Chama cha Demokrasia lazima kionyeshe kwa vitendo.
Kuwa na Wagombea katika ballot box kwa njia za kistaarabu ni maturity na inajenga confidence.
Hii ni missed opportunity kwa Chadema! so sad

JokaKuu
Upo kaka? 🤣

IMG_7184.jpeg
 
Tuanze na suala la Covid-19. What were the options? Mass mobilization? Kwa watu ambao wakisikia tu kesho wanajeshi wanafanya usafi hawatoki nje? Mimi personally naamini Mbowe alitaka kuwa lenient kwa wakina Halima. Lakini wenzake walipomtilia ngumu, aliwakubalia na mpaka sasa hivi hajabadilisha msimamo. Hiyo sio sign ya dictator kama Lissu anavyotaka kum portray.
Mkuu Fundi
Hapa kuna hoja naomba nizirejee. Kuhusu COVID-19 nimeshaeleza options alizokuwa nazo Mwenyekiti, hata hivyo nikukumbushe, Mbowe aliulizwa kuhusu suala hilo akiwa katika Maridhiano, alijibu ;
'' Suala linashughulikiwa na serikali. Ni suala lililopo katika taasisi linahitaji tuwape muda wa kulishughulikia kitaasisi'' Huyu ni Mbowe anakuwa msemaji wa Serikali ya CCM! Kwanini unadhani CCM haitampenda!

Kuhusu Mass mobilization, halikuwa suala la maandamano kwa nature yake kwavile ni la sheria.
Kama unakumbuka Mahakama ilianza kwa ubabaishaji, baada ya public pressure Mahakama haikuwa na namna ikalimaliza ! Kilichotakiwa ni pressure kwa Speaker aliyetumia Mahakama kama kichaka.
Pressure haikuwepo! Tukaona COVID-19 wakichangia pesa za charity za Mwenyekiti!

Hoja ya watu kisikia maandamano hawatoki!
Kuna sehemu mbili, kwanza ni Watanzania tunaowaulaumu kila siku kwa kutojali mambo yanayogusa maisha yao.

Pili, kuna ukweli kwamba M/Kiti Mbowe akiwa Ikulu aliacha watu wake juani Mahakamani Kisutu.
Nani amwamini tena? Madhara ya kupoteza public trust ndiyo hayo

Na Mwisho, Mbowe akiwa Mwanza alisema '' Jiandaeni na Uchaguzi wa Serikali za mitaa Mwakani. Muda ni mfupi wa kuandika Katiba mpya. Tutaendelea kudai minimal reforms katika Tume ya uchaguzi''
Mwenyekiti wa CDM anakuwa msemaji wa Serikali ya CCM kuhusu Katiba, kwanini CCM wasimpende!

Hayo yote hayaondoi haki ya Mbowe kuwania Uenyekiti. Ni afya kwa CDM kwasababu ni takwa la demokrasia , ni ukomavu wa kisiasa na huenda ikawa template ya vyama vya siasa.

TAL kasema , anataka ukomo wa uongozi ! Mfumo huru na haki wa uchaguzi. Mfumo wa wazi wa fedha
Mwenyekiti anajibu vipi hayo? Kama hana majibu, nini maono yake kwa miaka 5 ijayo ?
 
Hii ni ndefu kwa hiyo kwa wale ambao kusoma para zaidi ya moja ni mtihani wala wasianze kuisoma.

Kuna wanachama na wafuasi wa CHADEMA pamoja na wapinzani wengine wa chama tawala ambao wanaamini kwa dhati kuwa ni wakati muafaka wa kubadilisha approach ya kuleta mabadiliko kwa sababu inayotumika sasa hivi kwa kiasi kikubwa haijafanikiwa.

Wanaamini hii ni kwa sababu Mbowe hawezi kumudu tactics ambazo ni aggresive na confrontational za wakati huo. Na chachu ya tactics hizo itatokana nje ya taratibu za kawaida kama tulivyoona vijana wa nchi jirani walivyotumia tik tok n.k.

Mambo haya yote hayaendani na hulka ya Mbowe ambayo kwa kiasi fulani ni ya traditional politics. Hawa walihitaji kiongozi ambae hana uvumilivu kama wao. Kiongozi ambae yuko tayari kwenda "mano a mano" na serikali bila kujali consequences.

Kwa mtazamo wao Lissu ndio kiongozi anaewafaa. Kwa sababu walimwona Mbowe kama kizingiti kwao wakatumia tactics za kumuaibisha na kumbeza ili aone hahitaji hizo fedheha ajitoe. Bahati mbaya kwao walikuwa hawajamsoma Mbowe vizuri. Hawakujua tactics hizo ndio zitamfanya aone chama chake kinataka kuwa hijacked kihuni.

Kitu vingine ambacho hawakuzingatia ni kuwa watanzania wengi hawapendi confrontation na hivyo kuna uwezekano mdogo wa wao kujitokeza kwa wingi kujiunga nao. Kingine ni kuwa tactic kama hizi hazileti matokeo ya kudumu na mara nyingi zinakuwa hijacked na wana siasa na kufa kifo cha kimya kimya. Tumeona Kenya. Tumeona Malawi. Hata Tunisia na Misri.

Ubaya mwingine ni kuwa ni vigumu ku control ili vurugu zisitawale. Picha za vijana wakiwa wana warushia mawe hazina tija.

Amandla...
Mwenyekiti wa kudumu wa chama cha siasa, jibu nikwamba anahubiri demokrasia lakini yeye hataki mabadiliko wa nyazifa ya uwenyekiti, yaani ujinga ni kufunya jambo lile lile kwa mbinu zile zile, halafu unategemea matokeo chanya

Chadema ni chama kikubwa dhana ya kukijenga chama kwasasa ni ya uongo
 
Mkuu Fundi
Hapa kuna hoja naomba nizirejee. Kuhusu COVID-19 nimeshaeleza options alizokuwa nazo Mwenyekiti, hata hivyo nikukumbushe, Mbowe aliulizwa kuhusu suala hilo akiwa katika Maridhiano, alijibu ;
'' Suala linashughulikiwa na serikali. Ni suala lililopo katika taasisi linahitaji tuwape muda wa kulishughulikia kitaasisi'' Huyu ni Mbowe anakuwa msemaji wa Serikali ya CCM! Kwanini unadhani CCM haitampenda!

Kuhusu Mass mobilization, halikuwa suala la maandamano kwa nature yake kwavile ni la sheria.
Kama unakumbuka Mahakama ilianza kwa ubabaishaji, baada ya public pressure Mahakama haikuwa na namna ikalimaliza ! Kilichotakiwa ni pressure kwa Speaker aliyetumia Mahakama kama kichaka.
Pressure haikuwepo! Tukaona COVID-19 wakichangia pesa za charity za Mwenyekiti!

Hoja ya watu kisikia maandamano hawatoki!
Kuna sehemu mbili, kwanza ni Watanzania tunaowaulaumu kila siku kwa kutojali mambo yanayogusa maisha yao.

Pili, kuna ukweli kwamba M/Kiti Mbowe akiwa Ikulu aliacha watu wake juani Mahakamani Kisutu.
Nani amwamini tena? Madhara ya kupoteza public trust ndiyo hayo

Na Mwisho, Mbowe akiwa Mwanza alisema '' Jiandaeni na Uchaguzi wa Serikali za mitaa Mwakani. Muda ni mfupi wa kuandika Katiba mpya. Tutaendelea kudai minimal reforms katika Tume ya uchaguzi''
Mwenyekiti wa CDM anakuwa msemaji wa Serikali ya CCM kuhusu Katiba, kwanini CCM wasimpende!

Hayo yote hayaondoi haki ya Mbowe kuwania Uenyekiti. Ni afya kwa CDM kwasababu ni takwa la demokrasia , ni ukomavu wa kisiasa na huenda ikawa template ya vyama vya siasa.

TAL kasema , anataka ukomo wa uongozi ! Mfumo huru na haki wa uchaguzi. Mfumo wa wazi wa fedha
Mwenyekiti anajibu vipi hayo? Kama hana majibu, nini maono yake kwa miaka 5 ijayo ?
Mkuu Nguruvi3,
1. Ulilosema kuhusu Covid-19 proves my point. Nilisema Mbowe hakutaka kuwachukulia hatua kali wakina Halima kwa sababu ya ukaribu wake nao. Lakini alipokaa na wenzake akaona wengi hawakuwa katika mood ya kuwasamehe akakubaliana nao. Na toka hapo amekuwa steadfast katika msimamo kuwa walistahili kufukuzwa. Huyo ni mtu anae shaurika na sio dikteta kama ambavyo wengi wanataka tuamini.
2. Hakuna mtu aliyetegemea Mahakama iwe upande wa CDM kwenye suala la Covid 19. Hata Lissu alisema kuwa hilo suala wameachana nalo. Walijua ni futile exercise. Na sasa hivi iko kwenye "limbo" kutokana na hilo.
3. Kuwaalika wakina Halima ( na Rais) kuchangia katika ujenzi wa Kanisa lake ni par for the course. Hajawahi kukana ukaribu wake na Halima. Sitashangaa kusikia kuwa Halima huwa anamtembelea. Sio haki kumhukumu Mbowe kwa ukaribu wake na Halima halafu kuona ukaribu wa Lissu na Msigwa sio tatizo. Ukweli ulio wazi ni kuwa Halima Mdee na Esther Bulaya hawajawahi kusimama in public na kukisema vibaya Chadema na viongozi wake. On the other hand, Msigwa hana topic nyingine bali namna Chadema hakistahili kushika dola. Na anafanya kila jitihada kukichafua machoni mwa umma. Ningemuelewa kama angekuwa anamsema vibaya Mbowe peke yake lakini he goes beyond that na anakichafua chama cha Chadema! Huyu ndie rafiki kipenzi wa Lissu ambae alisimama kidete kuhakikisha Zitto anafukuzwa! Kitu pekee anachosema kuhusu rafiki yake ni "hoja zake zijibiwe". Seriously?
4. Nashindwa kuelewa point yako ya kuwa watu hawana imani nae kwa sababu alienda Ikulu alipotoka rumande. Mbona alipowaita kwenye maandamano yaliyokuwa na "baraka" za serikali walijitokeza kwa wingi? Pale serikali inapotoa vitisho wanamuachia Mbowe aandamane na binti yake pamoja na wanawake wa Bawacha. Na aliandamana na binti yake baada ya mashujaa wa mitandaoni kudai kuwa anawachuuza watoto wao wapigwe na polisi wakati wa kwake wako burhani nyumbani kwao.

Wakati huo nyumba ya Lissu ( na ya Mbowe) ilizingirwa na polisi kama ada. Ni reaction ya polisi ya mara zote. Tofauti safari hii ni kuwa Lissu pamoja na kujua hilo litatokea bado alilala nyumbani wakati Mbowe hakulala nyumbani na aliibukia kwenye maandamano! Bado hapo Lissu anaonekana shujaa na Mbowe sio shujaa. Kibaya zaidi maandamano hayo yalihusu wananchi waliopotea ama kuuawa. Suala ambalo linapaswa kuwa above politics na ilikuwa ni namna ya kuonyesha CDM inavyowajali wananchi. Lakini kama ada wananchi ( pamoja na ndugu wa watu waliopatwa na hiyo mikasa) wakaingia gizani. Na hii ni hata baada ya CDM kuwapa nafasi baadhi ya watu waliokuwa affected kueleza magumu wanayopitia baada ya kupotelewa na ndugu zao. Na kutangaza bila kukoma kuwa maandamano bado yapo pamoja na zuio la dola. Wananchi pamoja na Lissu hawakutokea.
5. Lissu anadai mfumo wa wazi wa fedha bila ku define ana maanisha nini. Anataka majina ya wote wanaochangia chama na pamoja na matumizi yake yawekwe wazi? Yeye mbona hakuwa wazi kuhusu michango ya kumnunulia gari lake? Amejitokeza mwishoni kutoa taarifa ya juu juu kuhusu pesa zilizopatikana na kiasi gani kilichobaki. Huyu anaetaka kutuaminisha kuwa wananchi wako tayari kuchangia pesa za kuendesha chama kama wakiwa mobilised imemchukua miezi kibao kuchangisha pesa ya kununua gari moja itakuwa mabilioni yanayohitajika kila mwaka kuendesha chama! Hayuko serious.
6. Ni chama gani cha upinzani kina ukomo wa uongozi duniani? Raila mpaka kesho anaongoza mapambano. Hakainde Hichilema anaongoza chama chake toka 2006 na amegombea urais mara 5 ndio akafanikiwa. ANC iliongozwa na Mandela kwa miaka kibao hata alipokuwa jela. Hawakusema huyu jamaa yuko jela na amekaa kwenye kiti kwa miaka mingi tuchague mtu mwingine. La, hasha. Waliendelea na mtu ambae amezoeleka na jamii mpaka pale waliposhika dola. CCM ina term limits kwa sababu tu cheo hicho kina ambatana na urais. Again, anachopendekeza Lissu ni unrealistic na kitafanya chama chake kidumae.
7. Tofauti na Lissu, Mbowe atawaelezea wanachama wake maono yake atakapokuwa anawaomba kura. Wale ndio audience sahihi. Sio haya ya kuzunguka mitandaoni kuvilify uongozi wa sasa wa chama. Kama alivyosema Lissu correctly ni kuwa mahusiano yake na Mwenyekiti wake sio mazuri. Baada ya haya anayomtuhumu in public atakuwa mnafik kama atamshirikisha zaidi ya kuheshimu nafasi yake ya kikatiba katika chama. In fact, sitashangaa kama akifanya juhudi za kubadilisha Katiba ya chama chake ili hata haki hiyo anyang'anywe. Mimi simuamini kabisa na kwenye hiyo kitchen cabinet yake ya Clubhouse wamejaa watu vindictive sana. Huyu ni mtu ambae tayari ameanza jitihada za watu kuondoa imani katika process nzima ya uchaguzi wake ili akishindwa iwe ni kisingizio atakachoweza kutumia ku mobilise puppets wake.

Nakutakia Noeli njema na nina kuombq radhi kwa kukujibu kwa kirefu sana.

Amandla....
 
Wanapenda siasa za Lissu ila alipopigwa risasi hakuna hata mmoja aliyejitokeza barabarani!
 
Back
Top Bottom