Kwanini kuna juhudi kubwa za kuhakikisha kuwa Mbowe haendelei kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA

Kwanini kuna juhudi kubwa za kuhakikisha kuwa Mbowe haendelei kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA

Hii ndiyo JF katika ubora wake. Nasoma neno kwa neno na muda si muda nami nitatoa my two cents. Hongrereni Nguruvi3 na Fundi Mchundo, mmeturudisha zama zile za hoja hujibiwa kwa hoja.

Hata hivyo naomba nimtahadharishe ndugu yangu Fundi Mchundo, usilolijua ni kama usiku wa giza. Kila nikikusoma nakuta najiuliza umepatwa na nini, what happened to the mighty amandla?
Na mimi nakushangaa hivyo hivyo. Hakuna aliyekuwa privy kwa yanayoendelea jikoni.

Mimi siku zote nasema ukweli ninavyo uona. Baada ya yaliyotokea kwa Halima simuamini mtu. Ninachosikitila ni kuwa kuna wakati uliungq mkono lugha ya kejeli dhidi yangu pamoja na kunifahamu kwa miaka mingi. Ndio maana ninamheshimu sana Nguruvi3 ambae pamoja na kutofautiana kimawazo hakuingia katika huo mtego.

Nisichopenda kwa moyo wangu wote ni bullying na ulaghai unaoendelea. Unampa Lissu benefit of the doubt kwa sababu tuu ya oratory skills alizokuwa nazo. Nakushangaa huoni hilo.

Ultimately nataka CDM i survive na I prosper ila nahofia lugha na approach ya Lissu inafanya hilo kuwa ndoto za alinacha.

Amandla...
 
1. Yesu Kristu alikuwa seremala.
2. Mtume Mohammed S.A.W alikuwa hajui kusoma.
3. Malcolm X elimu yake aliipatia jela.
4. Robert Nesta Marley hakwenda shule.
5. Karume hakufika Chuo Kikuu
6. Kleist Sykes hakufika Chuo Kikuu

KatIka hao uliosema wana Ph.D nani anawafikia hata 1/1000 hawa ambao hawakuwa wasomi?

Wewe endelea tu kuabudu Ph.D.

Amandla...
1. Yesu alisoma mbona huko synagogue. Alipewa elimu yote nzuri hakua illiterate.
5. Huyo karume alikua failure tu na ni sababu hakuwa na elimu pia.
6. Robert Marley alikua mwanamuziki sidhani kama burudani ina connection na elimu.

Otherwise kuna magwiji yaliyokua wasomi kina Einstein au richest man in history yaani Elon Musk umesikia hawakupita shule?
 
Mkuu Nguruvi3,
1. Kuhusu Covid-19 Mbowe hakutaka kuwachukulia hatua kali wakina Halima kwa sababu ya ukaribu wake nao. Lakini alipokaa na wenzake wengi hawakuwa katika mood ya kuwasamehe akakubaliana nao. Na toka hapo amekuwa steadfast katika msimamo kuwa walistahili kufukuzwa. Huyo ni mtu anae shaurika na sio dikteta kama ambavyo wengi wanataka tuamini.
COVID-19 walipingwa overwhelmed katika CDM, M/Kiti alikuwa hana choice kwa mujibu wa reliable source
Sijawahi amini ni Dikteta lakini pia kukaa madarakani miaka 21 kunampa nafasi ya kuwa na 'say' .
Mfano, Mbowe akiwa Mwenyekiti J.Pambalu pengine yupo darasa la 3. Ndivyo ilivyo kwa wengi wanaomzunguka.
2. Hakuna mtu aliyetegemea Mahakama iwe upande wa CDM kwenye suala la Covid 19. Hata Lissu alisema kuwa hilo suala wameachana nalo. Walijua ni futile exercise. Na sasa hivi iko kwenye "limbo" kutokana na hilo.
Hoja ni kwamba kulitakiwa kuwe na pre emptive strategy Ndugai na NEC wasingeweza kufanya uhuni
3. . Sio haki kumhukumu Mbowe kwa ukaribu wake na Halima halafu kuona ukaribu wa Lissu na Msigwa sio tatizo. . On the other hand, Msigwa hana topic nyingine bali namna Chadema hakistahili kushika dola, kukichafua machoni mwa umma. Huyu ndie rafiki kipenzi wa Lissu ambae alisimama kidete kuhakikisha Zitto anafukuzwa! Kitu pekee anachosema kuhusu rafiki yake ni "hoja zake zijibiwe". Seriously?
Mahusiano ya Mbowe na Halima si tatizo lakini mbele ya court of public opinion, huwezi kutenganisha mahusiano yao ya Kifamilia na suala la COVID-19. Mbaya zaidi sekretariati ya Mbowe ya akina Kigaila wake zao ni COVID-19.

Kuhusu Msigwa anayofanya ni udhalilishaji binafsi. Msigwa alikuwa na nafasi ya kuhama Chama lakini anachokifanya ni kufakamia matapishi. Huyu alikuwa kiongozi Mwandamizi !
Msigwa anafahamu hawezi kuchaguliwa tena na Wananchi, anachopigania ni alau u-DC

Kama ilivyo kwa Halima na Mbowe, Uhusiano wa TAL na Msigwa haujatengwa.
Kuvuja kwa nyaraka za CDM kunahusishwa na mahusiano ya wawili hao. Hivyo, TAL anaubeba msalaba sawia na ule wa COVID alioubeba FAM
4. Nashindwa kuelewa point yako ya kuwa watu kwa sababu alienda Ikulu alipotoka rumande. Mbona alipowaita kwenye maandamano yaliyokuwa na "baraka" za serikali walijitokeza kwa wingi? Pale serikali inapotoa vitisho wanamuachia Mbowe aandamane na binti yake pamoja na wanawake wa Bawacha.
Hoja, kitendo cha kuachiwa na kuibukia Ikulu kilitia shaka na ku demoralize political base. Hii maana yake ni kwamba aliondoa public trust! Pamoja na sababu zingine za uzembe wa Watanzania, low morality ilichangiwa sana na low public trust.

5. Lissu anadai mfumo wa wazi wa fedha bila ku define ana maanisha nini. Anataka majina ya wote wanaochangia chama na pamoja na matumizi yake yawekwe wazi? Yeye mbona hakuwa wazi kuhusu michango ya kumnunulia gari lake? Amejitokeza mwishoni kutoa taarifa ya juu juu kuhusu pesa zilizopatikana na kiasi gani kilichobaki. Huyu anaetaka kutuaminisha kuwa wananchi wako tayari kuchangia pesa za kuendesha chama kama wakiwa mobilised imemchukua miezi kibao kuchangisha pesa ya kununua gari moja itakuwa mabilioni yanayohitajika kila mwaka kuendesha chama! Hayuko serious.
Sidhani kama anataka waliochangia wawekwe wazi ! anataka mapato na matumizi yaonekane kwa uwazi.
Mfano, Team Mbowe haijaweza kujibu pesa za join the chain zipo wapi!
Ukimsikiliza TAL, anaeleza hata matumizi kama ya Chopper kwamba yaeleweke. Kuwa na mfumo mzuri wa pesa ni hoja nzuri

Kuhusu chama kuchangisha pesa, Mbowe yupo madarakani miaka 21. Ikiwa hajaweza kutengeneza source za Chama kujipatia fedha hilo linawapa hoja wanaotaka mabadiliko, kwa maana kwamba ameshindwa na hana mbinu

Si kweli kwamba Chama hakiwezi ku mobilize, Mbowe na Wanawake walipofungwa, katika 24hr zilichangwa milioni 370.

Kuhusu TAL kushindwa mobilization ya gari lake, kuna sababu nyingi kwa mtazamo wangu.
Moja, Chama kilipaswa kumsaidia. Pili, Wananchi wanaogopa isijekuwa ni ''join the chain' nyingine.
Tatu, TAL ame demoralize au paralyse michango yeye mwenyewe. Hakupaswa kuchukua pesa za CCM!
kwa maana kwamba walimwekea katika account kama mtego, kwanini hakurudisha!

6. Ni chama gani cha upinzani kina ukomo wa uongozi duniani? Raila mpaka kesho anaongoza mapambano. Hakainde Hichilema anaongoza chama chake toka 2006 na amegombea urais mara 5 ndio akafanikiwa. ANC iliongozwa na Mandela kwa miaka kibao hata alipokuwa jela. Hawakusema huyu jamaa yuko jela na amekaa kwenye kiti kwa miaka mingi tuchague mtu mwingine. La, hasha. Waliendelea na mtu ambae amezoeleka na jamii mpaka pale waliposhika dola. CCM ina term limits kwa sababu tu cheo hicho kina ambatana na urais. Again, anachopendekeza Lissu ni unrealistic na kitafanya chama chake kidumae.
Mandela akiwa gerezani kiongozi wa ANC alikuwa O.Tambo. Mandela alipachiwa huru , O.Tambo alikuwa mgonjwa.
Mandela aligoma kuwa Mwenyekiti wa ANC akisema '' kwa muda wote mlikuwa na Tambo, huyu ndiye kiongozi wetu''. Mandela akawa Makamu hadi Tambo alipofariki. Hili halifahamiki sana kwasababu Mandela ni iconic figure

Mandela alisema wazi atakuwa rais kwa kipindi kimoja tu. Baada ya hapo walifuata wengine.

Nimemzungumzia Mandela kwasababu si watu wanaozaliwa kila mwaka! Ukomo wa uongozi si jambo geni na halitakuwa ajabu likiwekwa. Kwanini watu wadhani sisi Watanzania tunapaswa kuiga na si kuweka mfano?

Hata hivyo watu wanapotosha hoja ya TAL. Lissu anasema uwepo ukomo kwa viongozi wakiwemo wa viti maalumu madiwani na Wabunge. Hoja ya TAL ni kwamba Viti maalumu viwe 'aunch pad' kwa miaka 5 baada ya hapo Wanawake wagombee majimboni, watakuwa wameiva.

Fikiri hivi, binti anayemaliza chuo akiwa na umri wa miaka 21 akipewa 5 ya viti maalumu atakuwa na 27 wakati anakwenda kugombea jimboni.

Kwa muundo wa sasa kuna waliokaa viti maalumu CDM miaka 15 na 20.
Yule Binti aliyemaliza Chuo akiwa na miaka 21 bado anasubiri Viti maalumu na akipata atakuwa na miaka 41
Ni hoja yenye mantiki sana! Inawafanya Wabunge /Madiwani kutobweteka wakijua hatma yao inategemea juhudi

Hoja ya TAL ina mantiki nyingine! kwamba term limit inampa nafasi kiongozi kutimiza malengo kwa wakati.
Ni mzazi gani anayefarajika kuona mtoto anaomba muda zaidi wa kusoma Form 4 kwasababu hajamaliza homework!

Kuweka term limit ni succession plan, kwamba, wapo wanaopiga Jaramba na hao ndio watakuwa na vision.

Mbowe ame recruit Zitto Kabwe. Kama angekuwa CDM Zitto angestaafu na Mbowe bila kuwa kiongozi jambo ambalo ni ndoto zake! John Heche ni zao la Mbowe, naye ana miaka michache astaafu! na atastaafu kwasababu Mbowe yupo !

Kama unadhani term limit ni mbaya, hebu nieleza, kwa miaka 21 Mbowe ni kiongozi.
Ni jambo gani alilosahau au analotaka alikamilishe kwa miaka 5 ijayo!
7. I. Mimi simuamini kabisa na kwenye hiyo kitchen cabinet yake ya Clubhouse wamejaa watu vindictive sana. Huyu ni mtu ambae tayari ameanza jitihada za watu kuondoa imani katika process nzima ya uchaguzi wake ili akishindwa iwe ni kisingizio atakachoweza kutumia ku mobilise puppets wake.
TAL anasababu za kutilia shaka process nzima. Hivi kwa Katiba ya Chadema ''ZOC'' anatajwa wapi?
Mbowe na Kigaila wametengeneza mfumo wa uchaguzi nje ya ule wa Chama! Ndicho anachosema Tundu Lissu

Kwasababu hizo, wasiomuunga mkono Mbowe kama Rose Mayemba wa Njombe chaguzi zao zimeharibiwa na Kigaila wa Mbowe.

Ukitazama matatizo ya Chaguzi za Kanda, Sekretariati ya Mbowe ikiongozwa na akina Kigaila ni tatizo.

Nimewashauri CDM ili kuondoa malalamiko kwa atakyeshindwa, iundwe Bodi itakayohusisha viongozi nje ya sekretariati.

Nakutakia Noel njema ndugu na jamaa
 
COVID-19 walipingwa overwhelmed katika CDM, M/Kiti alikuwa hana choice kwa mujibu wa reliable source
Sijawahi amini ni Dikteta lakini pia kukaa madarakani miaka 21 kunampa nafasi ya kuwa na 'say' .
Mfano, Mbowe akiwa Mwenyekiti J.Pambalu pengine yupo darasa la 3. Ndivyo ilivyo kwa wengi wanaomzunguka.
Mwenyekiti yeyote worth his or her salt lazima anakuwa na say kubwa katika maamuzi ya chama chake bila kujali amekaa miaka mingapi. Kama hana, huyo ni figure head. Kama angekuwa " authoritanian" hao waliokuwa wanapingana nae wala wasingethubutu. Na yeye mwenyewe angewashughulikia tu baadae kama Lissu anavyodai kuwa amewashughulikia yeye, Msigwa na wengine kwa sababu wametofautiana nae katika suala la maridhiano. Badala ya kuadmit kuwa position yao ilikuwa ya minority ana insinuate kuwa ni authoritarian tendencies za Mwenyekiti wake ndio zili carry the day. Kwangu mimi hapa ni Lissu ndie anayeonyesha hizo authoritarian tendencies.
Hoja ni kwamba kulitakiwa kuwe na pre emptive strategy Ndugai na NEC wasingeweza kufanya uhuni

Toa mfano wa strategy yeyote ambayo ingeweza kufanikiwa wakati ule.

Mahusiano ya Mbowe na Halima si tatizo lakini mbele ya court of public opinion, huwezi kutenganisha mahusiano yao ya Kifamilia na suala la COVID-19. Mbaya zaidi sekretariati ya Mbowe ya akina Kigaila wake zao ni COVID-19.
Court of public opinion ni fickle. Wote tunajua hilo. Hiyo sio sababu. Kumuadhibu Kigaila mke wake ni mmoja wa Covid-19 sio fair. Kama nilivyosema Covid-19 hawajawahi kuonyesha chuki dhidi ya Chadema na wakati mwingine nafasi ya mke wa Kigaila inampa access ya pekee kwa CCM. Na itaishia wapi? Ni level gani ya undugu mtu anaruhusiwa kuwa nao na mtu wa upande wa pili? Mtu ana ruhusiwa kuwa na mtoto Chadema? Mjomba je? Kama itathibitika kuwa huo uhusiano wake una affect utendaji wake basi ashughulikiwe lakini sio kwa sababu ya innuendos ambazo wasioitakia mema CDM wanaweza kutumia kuondoa watu wanaowaona kuwa ni tishio.
Kuhusu Msigwa anayofanya ni udhalilishaji binafsi. Msigwa alikuwa na nafasi ya kuhama Chama lakini anachokifanya ni kufakamia matapishi. Huyu alikuwa kiongozi Mwandamizi !
Msigwa anafahamu hawezi kuchaguliwa tena na Wananchi, anachopigania ni alau u-DC

Kama ilivyo kwa Halima na Mbowe, Uhusiano wa TAL na Msigwa haujatengwa.
Kuvuja kwa nyaraka za CDM kunahusishwa na mahusiano ya wawili hao. Hivyo, TAL anaubeba msalaba sawia na ule wa COVID alioubeba FAM
Hauwezi kumfananisha Halima na Msigwa. Kosa kubwa la Halima ni kung'ang'ania nafasi ambayo sio ya kwake. Hajawahi ( in public at least) kuihujumu CDM wazi wazi kama anavyofanya Msigwa. Msigwa ni self-proclaimed adui wa CDM wakati Halima sio. Lissu kumkumbatia na kukataa kabisa kumlaani kunaonyesha kuwa labda kuna kitu ambacho Msigwa anajua ndio kinamfanya asite. Lissu hajawahi kusita kumlaani mtu yeyote ambae anamuona ni threat kwa CDM ( unaweza hata kusema ndio sababu anamuandama Mbowe) kuanzia Zitto na kuendelea. Anapataje kigugumizi kwa Msigwa?
Hoja, kitendo cha kuachiwa na kuibukia Ikulu kilitia shaka na ku demoralize political base. Hii maana yake ni kwamba aliondoa public trust! Pamoja na sababu zingine za uzembe wa Watanzania, low morality ilichangiwa sana na low public trust.
Nadhani una wapa watanzania njia ya kutokea. Mimi nadhani kwa wengi wanafurahia tu ndugu zao kuachiwa. Ingekuwa hamna hiyo public trust wasingejazana kwenye maandamano yenye kibali cha mamlaka. Ni waoga tu. Na wanaona watapoteza zaidi ya kupata kama watashiriki kwenye maandamano.
Sidhani kama anataka waliochangia wawekwe wazi ! anataka mapato na matumizi yaonekane kwa uwazi.
Mfano, Team Mbowe haijaweza kujibu pesa za join the chain zipo wapi!
Ukimsikiliza TAL, anaeleza hata matumizi kama ya Chopper kwamba yaeleweke. Kuwa na mfumo mzuri wa pesa ni hoja nzuri
Yataonekanaje kwa uwazi kama hayawekwi wazi? Wanaotakiwa kujua kwa undani matumizi ya pesa za CDM ni wajumbe wa Kamati Kuu ( KK) wa CDM na CAG. Lissu ni mtu wa pili katika seniority ndani ya CDM na kama hilo tatizo lilikuwa toka awali alitakiwa kulisemea ndani ya KK na kama angeona hasikilizwi angejiuzuru na kuisemea akiwa nje ya KK. Lakini hakufanya hivyo. Mwingine wa kusemea alikuwa CAG lakini anaishia kutoa hati safi. Nakumbuka baada ya Lijualikali kulia Bungeni na kumshutumu aliyemuita "mwamba" kwa kila aina ya dhambi, Ndugai aliiagiza Takukuru ikague mahesabu ya CDM. Hao nao mpaka leo wako kimya. Unadhani wangekuta chembe ya matumizi mabaya wangewaacha salama? Tatizo letu tunapenda na kuamini mno taarifa zinazolenga kubomoa kuliko zinazojenga. Watoto wako wakiwa wanafanya vizuri watu wataamini zaidi kuwa unatumia nguvu za giza kuhakikisha wana pasi kuliko kuwa unawekeza sana katika kuwapa wa ziada wa kujielimisha na kuelimishwa na wengine. Wataingia kutafuta hirizi lakini bookshelf ya vitabu hawataiona. Ndivyo tulivyo.
Kuhusu chama kuchangisha pesa, Mbowe yupo madarakani miaka 21. Ikiwa hajaweza kutengeneza source za Chama kujipatia fedha hilo linawapa hoja wanaotaka mabadiliko, kwa maana kwamba ameshindwa na hana mbinu
Source ipi ya fedha angeweza kutengeneza bila kuzibwa na serikali? Na kwa nini alaumiwe Mbowe peke yake na sio uongozi wote? Chama cha siasa hakitakiwi kufanya biashara. Tunakumbuka ilivyokuwa kwa Sukita. Hao wenye mbinu za kupata pesa mbona siku zote wako kimya? Au Mbowe aliwaziba midomo kutoa ushauri?
Si kweli kwamba Chama hakiwezi ku mobilize, Mbowe na Wanawake walipofungwa, katika 24hr zilichangwa milioni 370.
One off event tunatoa sana. Ndio maana ni mahodari katika kuchangia harusi na msiba kuliko matibabu na elimu. Kumchangia mtu aliyepigwa faini tunaweza sana lakini tunapata shida kuwachangi waliokuwa Mahabusu.
Kuhusu TAL kushindwa mobilization ya gari lake, kuna sababu nyingi kwa mtazamo wangu.
Moja, Chama kilipaswa kumsaidia. Pili, Wananchi wanaogopa isijekuwa ni ''join the chain' nyingine.
Tatu, TAL ame demoralize au paralyse michango yeye mwenyewe. Hakupaswa kuchukua pesa za CCM!
kwa maana kwamba walimwekea katika account kama mtego, kwanini hakurudisha!
Huu ni mchango aliouanzisha Lissu personally na haukuwa wa CDM. Labda kwa CDM haikuwa priority. Lakini hapa pia tunakuwa wepesi sana kumtafutia visingizio Lissu anapokengeuka kuliko mtu mwingine. Kuna tofauti gani kati ya kupokea mchango kutoka CCM kwa ajili ya gari yako binafsi na kupokea kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM kwa ajili ya ujenzi wa kanisa kijijini mwako? Lakini Mbowe analaaniwa wakati Lissu hata hasemwi.
Mandela akiwa gerezani kiongozi wa ANC alikuwa O.Tambo. Mandela alipachiwa huru , O.Tambo alikuwa mgonjwa.
Mandela aligoma kuwa Mwenyekiti wa ANC akisema '' kwa muda wote mlikuwa na Tambo, huyu ndiye kiongozi wetu''. Mandela akawa Makamu hadi Tambo alipofariki. Hili halifahamiki sana kwasababu Mandela ni iconic figure

Mandela alisema wazi atakuwa rais kwa kipindi kimoja tu. Baada ya hapo walifuata wengine.
Sawa. Lakini the gist ni the same. Unahitaji iconic figure kuongoza mapambano dhidi ya utawala. Hata Tambo alikaa kwa muda mrefu na ndivyo ilivyo paswa kuwa.⁵
Nimemzungumzia Mandela kwasababu si watu wanaozaliwa kila mwaka! Ukomo wa uongozi si jambo geni na halitakuwa ajabu likiwekwa. Kwanini watu wadhani sisi Watanzania tunapaswa kuiga na si kuweka mfano?
Hatuwezi kuwa mfano katika jambo lisilo na tija. Lissu amezungumzia Uenyekiti na vyeo vingine. Kwa mantik hii, kama atashinda mwakani hawezi kuwa Mwenyekiti zaidi ya 2035. Tuseme amegombea urais 2030 akashinda basi itabidi kati ya 2035 na 2040 awe chini ya Mwenyekiti mwingine! Hauwezi kuwa na centres of power mbili mkabaki salama. CCM waliona hilo wakaliacha mapema. Aidha, tunaposema muda usio na kikomo hakumaanishi kuwa anaekikalia hapaswi kupimwa regularly kuonekana kama bado anafaa. Akionekana hafai, baada ya term moja tu anaweza kutemwa.
Mbowe amechaguliwa kuwa Mwenyekiti 2004. Kwa dhana hii, 2014 angepaswa kumpisha mwingine. Sidhani kama Zitto au Lissu wangeweza kukiongoza chama kama alivyofanya Mbowe katika ule wakati mgumu wa mpito. Act Wazalendo imeweza ku survive kwa kujionyesha kuwa wao sio threat kubwa kwa CCM na damu mpya ya waliotokea CUF. Angeachia ngazi 2014, tungekuwa tunaimba wimbo mwingine.
Hata hivyo watu wanapotosha hoja ya TAL. Lissu anasema uwepo ukomo kwa viongozi wakiwemo wa viti maalumu madiwani na Wabunge. Hoja ya TAL ni kwamba Viti maalumu viwe 'aunch pad' kwa miaka 5 baada ya hapo Wanawake wagombee majimboni, watakuwa wameiva.

Fikiri hivi, binti anayemaliza chuo akiwa na umri wa miaka 21 akipewa 5 ya viti maalumu atakuwa na 27 wakati anakwenda kugombea jimboni.

Kwa muundo wa sasa kuna waliokaa viti maalumu CDM miaka 15 na 20.
Yule Binti aliyemaliza Chuo akiwa na miaka 21 bado anasubiri Viti maalumu na akipata atakuwa na miaka 41
Ni hoja yenye mantiki sana! Inawafanya Wabunge /Madiwani kutobweteka wakijua hatma yao inategemea juhudi
Hii ya ukomo katika viti maalum ina mantik. Lakini term moja ni ndogo sana. Wanatakiwa angalau wapewe term 2 ili wakomae. Mchango na weledi wa watu kama Halima, Suzan, Esther x 2 katika kuisimamia serikali usingekuwa kama ulivyokuwa kama wangekaa term moja moja.
Hoja ya TAL ina mantiki nyingine! kwamba term limit inampa nafasi kiongozi kutimiza malengo kwa wakati.
Ni mzazi gani anayefarajika kuona mtoto anaomba muda zaidi wa kusoma Form 4 kwasababu hajamaliza homework!
Katika mfumo wetu mimi sidhani mtu anapaswa kuwa na malengo binafsi tofauti na ya chama. Mambo ya mbunge kuomba nyongeza kwa sababu hajaweza kufanikisha ujenzi wa barabara ni usanii.
Kuweka term limit ni succession plan, kwamba, wapo wanaopiga Jaramba na hao ndio watakuwa na vision.

Mbowe ame recruit Zitto Kabwe. Kama angekuwa CDM Zitto angestaafu na Mbowe bila kuwa kiongozi jambo ambalo ni ndoto zake! John Heche ni zao la Mbowe, naye ana miaka michache astaafu! na atastaafu kwasababu Mbowe yupo !
Sio haki ya kila mtu kuwa kiongozi Mkuu. Sio kitu cha majaribio au cha kuchezea "musical chairs". Heche amefanikisha mengi sana na anastahili kuheshimiwa kwa mchango wake mkubwa hata kama hatakuwa Mwenyekiti. Hivyo hivyo kwa Lissu na wengine. Na kwenye siasa hamna umri wa kustaafu.
Kama unadhani term limit ni mbaya, hebu nieleza, kwa miaka 21 Mbowe ni kiongozi.
Ni jambo gani alilosahau au analotaka alikamilishe kwa miaka 5 ijayo!
Hilo ni swali ambalo watakaopiga kura wana haki ya kumuuliza. Asipokuwa na majibu sahihi itabidi wampumzishe. Na sababu za yeye kutaka kuendelea sio lazima ziwe hizo tu. Inawezekana anaona kuwa uhai wa chama uko hatarini na yeye ndie mwenye uwezo wa kukivusha katika kimbungq kinachokuja. Wapiga kura wasipo muamini watampa meli nahodha mwingine.
TAL anasababu za kutilia shaka process nzima. Hivi kwa Katiba ya Chadema ''ZOC'' anatajwa wapi?
Mbowe na Kigaila wametengeneza mfumo wa uchaguzi nje ya ule wa Chama! Ndicho anachosema Tundu Lissu

Kwasababu hizo, wasiomuunga mkono Mbowe kama Rose Mayemba wa Njombe chaguzi zao zimeharibiwa na Kigaila wa Mbowe.
Haya ni maneno ya Lissu. Sio lazima yaaminiwe. Mimi sijui Rose Mayemba alihumiwa vipi. Lakini najua ni dada mahiri sana. Wakati mwingine nahisi atasema lolote kuwachafua wale anao waona kuwa ni wabaya wake. Kingaila ana wajibika kwa KM sio Mwenyekiti. Lakini sishangai maana naona sasa hivi anafanya juhudi kuwaingiza Lema na Heche katika vita yake. Hiyo sio sawa kabisa.
Ukitazama matatizo ya Chaguzi za Kanda, Sekretariati ya Mbowe ikiongozwa na akina Kigaila ni tatizo.
Chama kama CDM ni lazima kitafanya kila jitihada kuzuia wale wanaodhani wanaweza kuwa mamluki kushika nafasi za uongozi. Hiyo ni kazi ya sekretariat. Kuna wakati inakosea na kuna wakati inapatia. Na kuna wakati inaweza kutumika kwa maslahi binafsi na sio ya chama.
Nimewashauri CDM ili kuondoa malalamiko kwa atakyeshindwa, iundwe Bodi itakayohusisha viongozi nje ya sekretariati.
Labda wapate malaika. Mimi nadhani wanahitaji mfumo wa upigaji na uhesabuji kura ulio wa wazi na efficient zaidi. Paundwe pia chombo cha rufaa kitakachojumuisha watu wanaoaminika na majority ya wanachama. Au wanaweza kuwa na mfumo kama wa arbitration ambapo majina ya wataokuwa katika kamati ya rufaa yanapelekwa kwa wagombea kwa ridhaa yao. Ni wale tuu wanaokubalika na wagombea wote ndio waunde kamati ya rufaa. Na kwa sababu haitakuwa ya kudumu, nafasi za hujma zitapungua.
Nakutakia Noel njema ndugu na jamaa
Na wewe pia nakutakia Noeli, Kwanzaa, Hanukka na MwakaMpya mwema kwako na kwa ndugu na jamaa zako.

Amandla...
 
Uingereza: Waziri Mkuu David Cameron kawasihi Waingereza waikatae BREXIT kwenye kura. Waingereza wakamkatalia Cameron wakaikubali BREXIT. Waziri Mkuu Cameron mara moja akajiuzulu kwa kujua hakubaliki na wananchi.

Tanzania: Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani kashindwa kuiondoa serikali madarakani kwa miaka 20, wala kufanya lolote la maana. Lakini anang'ang'ania aendelee kuwa mwenyekiti kama urais wa Kamuzu Banda. Hata somo la Nyerere la kung'atuka kwa heshima kabla hujang'atuliwa kwa aibu hajalielewa.
 
Mbowe amekaa kimya sana baada ya kutangaza kugombea. Sitashangaa kama atakuja na risiti za kuonyesha mapungufu ya Lissu. Tumeona jinsi alichosema kuhusu Wenje na Abduli kinavyokuwa challenged kidogo kidogo. Mara aliyenipa ushahidi Mwenyezi Mungu amempenda zaidi. Halafu imeshushwa clip ikionyesha kuwa Lissu aliwahi kukiri kuwa alikubali Abduli amsaidie katika kupata malipo yake. Na kuwa alimpa ushahidi.

Kingine ni tamko la Mbowe kuhusu uchangiaji wa CDM na kuwa kila kiongozi ni ombaomba kwenye hilo. Kuna kitu alianza kusema, akajiuma na kusema tuyaachie hapo.

Hii habari haitakiacha CDM salama hata kidogo. Hasa kwa sababu Mbowe hachukui POW.

Apples na Oranges.

Amandla...
 
Apples na Oranges.

Amandla...
Sasa Mbowe kama anataka kututoa kwenye apples atupeleke kwenye oranges, inabidi awe mfano.

Mbowe kusema anataka kuwatoa CCM madarakani na kuleta uongozi mpya Tanzania kwa kuwa CCM wamehodhi madaraka kwa miongo mingi, wakati yeye mwenyewe anang'ang'ania uenyekiti wa CHADEMA hataki kuuachia ingekuwa kichekesho kama isingekuwa janga la kitaifa.

CCM wanaweza kumsema Mbowe kuwa wao wamebadilisha wenyeviti kadhaa wakati Mbowe kagoma kutoka kwenye kiti.

Mbowe kachoka hana mpya sasa hivi, watu washamchoka. Anaendeleza siasa za kumlamba Samia miguu wakati Samia ni Machiavellian maniac anampiga kiswahili cha maridhiano huku kwenye vitendo anaendeleza uhuni wa Magufuli.

CHADEMA inahitaji muelekeo mpya Mbowe kapimwa kaonekana anafanya siasa za career hawezi kuleta mabadiliko yoyote.
 
Hutashangaa Mbowe akija na risiti za kuonesha mapungufu ya Lissu, asipokuja na hizo risiti utafanya nini?

Kwa nini alichosema Lissu kinakuwa challenged kidogo kidogo hakipigwi daflao ya kukimaliza kabisa?

Lissu ka volunteer hiyo habari kwamba aliyempa ushahidi kafariki, it's not like alibanwa ndiyo akasema hivyo. Kwa nini unataka i sound kama alisema hivyo kwa kubanwa?

Clip gani Lissu alikubali Abdul amlipe malipo yake? Iweke hapa.

Mkuu, unafuatilia maneno anayosema Lissu live au unasikiliza clip tu?

Kwa sababu una sound kama unasikiliza clip tu wakati watu tumemsikiliza Lissu akiongea kwa masaa, kwa muktadha. Lissu ndiye ana volunteer habari halafu wewe unafanya kama vile Lissu karekodiwa kwenye clip kisiri imevuja.

Lissu mbona kaeleza vizuri jinsi Abdul alivyotaka kumuhonga na Lissu akasema hataki hela za hongo kama Abdul anataka kumsaidia amsaidie Lissu alipwe hela zake halali? Umesikia kipande hicho? Umemsikia msaidizi wake David Jumbe mbona kaongea mchezo ulivyokuwa kati ya Wenje na Abdul upande mmoja na Lissu na yeye David Djumbe upande wa pili siku ya tukio?

Unajua replays zipo Clubhouse unaweza kusikia masaa yote aliyoongea Lissu si kusikiliza clip tu?

View: https://youtu.be/rpoAjfR3a5g?si=pCXLgDG6lPKoJZBy
 
Sasa Mbowe kama anataka kututoa kwenye apples atupeleke kwenye oranges, inabidi awe mfano.

Mbowe kusema anataka kuwatoa CCM madarakani na kuleta uongozi mpya Tanzania kwa kuwa CCM wamehodhi madaraka kwa miongo mingi, wakati yeye mwenyewe anang'ang'ania uenyekiti wa CHADEMA hataki kuuachia ingekuwa kichekesho kama isingekuwa janga la kitaifa.

CCM wanaweza kumsema Mbowe kuwa wao wamebadilisha wenyeviti kadhaa wakati Mbowe kagoma kutoka kwenye kiti.

Mbowe kachoka hana mpya sasa hivi, watu washamchoka. Anaendeleza siasa za kumlamba Samia miguu wakati Samia ni Machiavellian maniac anampiga kiswahili cha maridhiano huku kwenye vitendo anaendeleza uhuni wa Magufuli.

CHADEMA inahitaji muelekeo mpya Mbowe kapimwa kaonekana anafanya siasa za career hawezi kuleta mabadiliko yoyote.
Apples and oranges

Amandla...
 
Apples and oranges

Amandla...
Is this the best you can do?

Mbowe kashindwa kuheshimu kanuni za kidemokrasia za kupishana uongozi katika chama ambacho demokrasia ipo katika jina lake.

Kwenye hilo hata CCM wamemshinda.

Anataka kutu Museveni kwenye siasa za upinzani.

Is this what you stand for?
 
Hii ni ndefu kwa hiyo kwa wale ambao kusoma para zaidi ya moja ni mtihani wala wasianze kuisoma.

Kuna wanachama na wafuasi wa CHADEMA pamoja na wapinzani wengine wa chama tawala ambao wanaamini kwa dhati kuwa ni wakati muafaka wa kubadilisha approach ya kuleta mabadiliko kwa sababu inayotumika sasa hivi kwa kiasi kikubwa haijafanikiwa.

Wanaamini hii ni kwa sababu Mbowe hawezi kumudu tactics ambazo ni aggresive na confrontational za wakati huo. Na chachu ya tactics hizo itatokana nje ya taratibu za kawaida kama tulivyoona vijana wa nchi jirani walivyotumia tik tok n.k.

Mambo haya yote hayaendani na hulka ya Mbowe ambayo kwa kiasi fulani ni ya traditional politics. Hawa walihitaji kiongozi ambae hana uvumilivu kama wao. Kiongozi ambae yuko tayari kwenda "mano a mano" na serikali bila kujali consequences.

Kwa mtazamo wao Lissu ndio kiongozi anaewafaa. Kwa sababu walimwona Mbowe kama kizingiti kwao wakatumia tactics za kumuaibisha na kumbeza ili aone hahitaji hizo fedheha ajitoe. Bahati mbaya kwao walikuwa hawajamsoma Mbowe vizuri. Hawakujua tactics hizo ndio zitamfanya aone chama chake kinataka kuwa hijacked kihuni.

Kitu vingine ambacho hawakuzingatia ni kuwa watanzania wengi hawapendi confrontation na hivyo kuna uwezekano mdogo wa wao kujitokeza kwa wingi kujiunga nao. Kingine ni kuwa tactic kama hizi hazileti matokeo ya kudumu na mara nyingi zinakuwa hijacked na wana siasa na kufa kifo cha kimya kimya. Tumeona Kenya. Tumeona Malawi. Hata Tunisia na Misri.

Ubaya mwingine ni kuwa ni vigumu ku control ili vurugu zisitawale. Picha za vijana wakiwa wana warushia mawe hazina tija.

Amandla...
Dogo umejijibubu maswali yako tayari, Mbowe apumuzike tu
 
Is this the best you can do?

Mbowe kashindwa kuheshimu kanuni za kidemokrasia za kupishana uongozi katika chama ambacho demokrasia ipo katika jina lake.

Kwenye hilo hata CCM wamemshinda.

Anataka kutu Museveni kwenye siasa za upinzani.

Is this what you stand for?
Apples and Oranges ina maana unalinganisha vitu viwili tofauti. Mbowe hagombei na hajawahi kuwa Rais wa Tanzania kwa kumlinganisha na Rais wa nchi hii au nyingine ni kutomtendea haki. Kinachopaswa kuangaliwa ni Katiba ya CCM inasema nini kuhusu ukomo wa Mwenyekiti kuhudumia cheo hicho. Ibara ya 113 (1) ya Katiba ya CCM inasema " Mwenyekiti wa Taifa atachaguliwa na Mkutano Mkuu wa CCM wa Taifa na atakuwa katika nafasi hiyo kwa miaka mitano lakini anaweza kuchaguliwa tena baada ya muda huo kumalizika". Haijatoa ukomo wa kuchaguliwa tena. Sasa hawa watapata ubavu wapi wa kuisema CDM kwa kuendelea kumchagua Mwenyekiti huyo huyo kwa zaidi ya mara 10?

Ukomo wa kushika nafasi ni kwa Rais na sio kwa Mwenyekiti. Rais kutoka chama cha Mapinduzi ana haki ya kugombea Uenyekiti wa chama chake baada ya kumaliza muda wake wa kikatiba wa JMT. Mathlani chama chake kikishindwa uchaguzi wa urais baada ya muda wake kwisha atakuwa na haki ya kugombea Uenyekiti ili aongoze mapambano akiwa sehemu ya upinzani.

Amandla...
 
Attachments

  • 1000128036.jpg
    1000128036.jpg
    235.1 KB · Views: 1

Na Kwa nini kuna juhudi kubwa za kuhakikisha kuwa Mbowe anaendelea kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA, vice versa is true as well​

Mwenyekiti yeyote worth his or her salt lazima anakuwa na say kubwa katika maamuzi ya chama chake bila kujali amekaa miaka mingapi. Kama hana, huyo ni figure head. Kama angekuwa " authoritanian" hao waliokuwa wanapingana nae wala wasingethubutu. Badala ya kuadmit kuwa position yao ilikuwa ya minority ana insinuate kuwa ni authoritarian tendencies za Mwenyekiti wake ndio zili carry the day. Kwangu mimi hapa ni Lissu ndie anayeonyesha hizo authoritarian tendencies.
Nakuelewa, unasimama kwa M/Kiti kwa kivuli cha majority! Sijui kama walipiga kura au la.
Ninachoelewa katika mambo ya utawala tathmini hufanywa kwa Quality na Quantity

Nyerere alishauri vyama vingi licha ya 80/20 ya Watanzania kukataa. Suala la vyama vingi lilihitaji hekima na si idadi.

Mwl Nyerere alipoita Kamati kuu kujadili mgomo wa Wanafunzi wa UDSM, majority walimwambia awafukuze! ikiwezekana washtakiwe. Mwl akawaambia, Wanafunzi wametoa hoja zao, zipingine! Wajumbe hawakuweza !
Mwl akawambia mawazo hayapigwi rungu. Maaa yake, Mwl alijali quality kuliko quantity

Mzee Warioba anasema Tume ya ya Katiba alimtaka kila mmoja azungumze, si kupiga kura.
Maana yake, alizingatia quality kuliko quantity

Je, FAM alisikiliza manguli waliopishana naye au alikimbilia kura ?
Tazama Kamati kuu ya CDM halafu uniambie 2/3 ya Wajumbe wanaweza kusema nini against FAM.
Toa mfano wa strategy yeyote ambayo ingeweza kufanikiwa wakati ule.
Nilishaeleza, kulikuwa na taarifa za uhakika kwamba Ndugai ameongea na COVID-19, mratibu alikuwa KM CCM.
Mbowe angetoka na kusema '' CDM haitapeleka Wabunge na atakayekwenda Bungeni si wa CDM''
Ndugai, KM CCM na System wasingeweza kwasababu habari ingevuja kabla. FAM alikaa kimya
Yataonekanaje kwa uwazi kama hayawekwi wazi? Wanaotakiwa kujua kwa undani matumizi ya pesa za CDM ni wajumbe wa Kamati Kuu ( KK) wa CDM na CAG. Mwingine wa kusemea alikuwa CAG lakini anaishia kutoa hati safi.
CAG anakagua hesabu zilizopo. Ikiwa fedha za join the chain hazikuingia katika System ya CDM, CAG atakagua vipi?
Kwanini watu hawatoki na kueleza join the chain pesa ziko wapi ili kumaliza hii hoja once and for all
Chama kama CDM ni lazima kitafanya kila jitihada kuzuia wale wanaodhani wanaweza kuwa mamluki kushika nafasi za uongozi. Hiyo ni kazi ya sekretariat. Kuna wakati inakosea na kuna wakati inapatia.
Rose Mayemba ni CDM kindaki ndaki! alitangaza kumuunga mkono Msigwa hadharani (Tweet).
Kigaila amekwenda mara 2 akiruhusu uhuni ili uchaguzi urudiwe. Rose amekata rufaa, Kigaila ameikalia kimya
Kamati kuu inakaa kila mara, suala la Rose Mayemba limewekwa kapuni na Sekretariati ya JJ Mnyika na Kigaila.

Mwenyekiti Mbowe yupo kimya licha ya wewe kusema ana ''say kubwa'' hili ni suala linalojenga hisia mbaya, linatakiwa kushughilikiwa. FAM na Sekretariati yake akiwatumia akina Kigaila wanataka kulifinyanga.
Nani ana imani tena na system iliyopo ya uchaguzi?
Mimi nadhani wanahitaji mfumo wa upigaji na uhesabuji kura ulio wa wazi na efficient zaidi. Paundwe pia chombo cha rufaa kitakachojumuisha watu wanaoaminika na majority ya wanachama. Au wanaweza kuwa na mfumo kama wa arbitration ambapo majina ya wataokuwa katika kamati ya rufaa yanapelekwa kwa wagombea kwa ridhaa yao. Ni wale tuu wanaokubalika na wagombea wote ndio waunde kamati ya rufaa. Na kwa sababu haitakuwa ya kudumu, nafasi za hujma zitapungua.

Amandla...
Hili nimeshauri sana na ndilo litaisaidia CDM! Kigaila na Wenzake hawana hata sifa ya kushika karatasi ya kura
Ni corrupt, compromised na wahuni.
 
Apples and Oranges ina maana unalinganisha vitu viwili tofauti. Mbowe hagombei na hajawahi kuwa Rais wa Tanzania kwa kumlinganisha na Rais wa nchi hii au nyingine ni kutomtendea haki. Kinachopaswa kuangaliwa ni Katiba ya CCM inasema nini kuhusu ukomo wa Mwenyekiti kuhudumia cheo hicho. Ibara ya 113 (1) ya Katiba ya CCM inasema " Mwenyekiti wa Taifa atachaguliwa na Mkutano Mkuu wa CCM wa Taifa na atakuwa katika nafasi hiyo kwa miaka mitano lakini anaweza kuchaguliwa tena baada ya muda huo kumalizika". Haijatoa ukomo wa kuchaguliwa tena. Sasa hawa watapata ubavu wapi wa kuisema CDM kwa kuendelea kumchagua Mwenyekiti huyo huyo kwa zaidi ya mara 10?

Ukomo wa kushika nafasi ni kwa Rais na sio kwa Mwenyekiti. Rais kutoka chama cha Mapinduzi ana haki ya kugombea Uenyekiti wa chama chake baada ya kumaliza muda wake wa kikatiba wa JMT. Mathlani chama chake kikishindwa uchaguzi wa urais baada ya muda wake kwisha atakuwa na haki ya kugombea Uenyekiti ili aongoze mapambano akiwa sehemu ya upinzani.

Amandla...
Kitu cha kwanza kabisa sijamlinganisha Mbowe kama rais wa Tanzania, hata David Cameron hakuwa rais wa Uingereza wala head of state wa Uingereza. Nimelinganisha kiongozi wa kitaifa anavyoweza kufuata kanuni za kidemokrasia za kuona kashindwa kazi na kung'atuka kwa heshima kabla hajang'atuliwa kwa aibu.

Haya, ukisema David Cameron ni kiongozi wa serikali, Mbowe hakuongoza serikali, Uingereza Neil Kinnock, kiongozi wa Labor, baada ya kushindwa mara kadhaa, alikubali kwamba anajiuzulu kupisha wengine, Neil Kinnock hakuwa kiongozi wa serikali, alikuwa kiongozi wa opposition.

Soma hotuba ya Neil Kinnock alipoachia ngazi hapa Neil Kinnock resigns as Labour leader: from the archive, 14 April 1992

Pili, umefanya logical fallacy ya argument from dictionary. Suala ni kanuni ya kidemokrasia ya kupishana uongozi, bila kujali katiba inasema nini, katiba inaweza kuwa haina demokrasia ikabadilishwa, ndiyo maana kuna mabadiliko ya kikatiba, lakini, kanuni ni kwamba demokrasia inaendana na kuachiana madaraka. Hakukuwa na haja ya ku cite katiba, in fact ulivyo cite katiba umeonesha CCM wanafuata demokrasia ya kupishana kwenye uenyekiti bila hata ya kulazimishwa na katiba, kitu ambacho Mbowe kashindwa. Mbowe anataka kuwatoa CCM wakati kwenye suala la mwenyekiti kupisha wengine kwa hiyari CCM wamemshinda.

CCM wenyeviti hawalazimiki kung'atuka, lakini wanang'atuka, bila kushurutishwa na katiba. Katika hili wamemshinda Mbowe. Mbowe anakosa moral high ground kusema CCM wanang'ang'ania madarakani wakati yeye mwenyewe kakaa kwenye uenyekiti wa CHADEMA kupita mwenyekiti yeyote wa CCM.

Huelewi wapi?
 
Pascal Mayalla
Unasema hajabezwa halafu hapo hapo unamuita Sultan?
Unadhani ile saga ya Wenja ilimuhusu nani? Ni nani, kama sio Mwenyekiti wa Chama? Hayo maneno ya pesa ya Abdul yalimlenga Mbowe 100%.
Mnachonishangaza ni hiyo amnesia ya kujifanya kuwa hizo confrontational tactics hazijawahi kutumiwa na uongozi wa Mbowe. Kifo cha yule mwanafunzi aliyeuawa kwenye basi hakikutokea kwenye picnic ya Chadema.
Mbowe na wenzake walitiwa ndani kwa kile kilichodaiwa kuwa wanakiuka amri halali.
Mbowe na wenzake waliitisha maandamano kupinga matokeo ya uchaguzi wa 2000 lakini watanzania walipoona askari wanafagia wakanywea.
Mbowe alitangaza mpaka tarehe ya maandamano ya kupinga mauaji, upoteaji wa watu n.k ( mambo ambayo utadhani wale wote revolushenaries wangeguswa) wakatokea Mbowe, binti yake na wakina Hilda tu. Wale wote waliokuwa wanatamba humu ndani hawakuonekana. Labda kama walikuwa wameji camouflage kama bodaboda.
Hata wakati wa uchaguzi uliopita. Ukiondoa mashujaa kama yule dada wa Dodoma wengi waliishia kutuma clips na picha walizochukua kwa kujificha.
Watu wa aina hii ndio unataka kutuaminisha kuwa wanamsubiri Lissu aite lamgambo ndio wajitokeze!
Sasa hizo mbinu mpya za confrontational politics ni zipi? Au safari hii watabeba mawe wakiongozwa na jemadari wao?
Hizo zote ni ndoto tu. Hazitatokea.

Amandla...

Pascal Mayalla
Not enough to convince
Amelegea juzi ccm wakashinda 99%

Kwa sasa Hawezi komaa na kaulimbiu ya ""no reform no election""

Tuombe lissu atuvushe
 
From the archive, 14 April 1992: Neil Kinnock resigns as Labour leader​

This article is more than 9 years old
“My sorrow is that millions, particularly those who do not have the strength to defend themselves, will suffer because of the election of another Conservative government”

1da7e93f-a1e7-4c8f-ab0b-c440a6b11109-2060x1236.jpeg

Neil Kinnock, with his wife Glenys, giving a speech to Labour Party workers at their Walworth Road HQ after losing the 1992 general election. Photograph: Sean Smith/taken from picture library

The following is the text of yesterday’s statement by Neil Kinnock:

In the wake of the election defeat I am taking action which, in my judgment as leader, will serve the best interests of the Labour Party.

I trust that members and supporters will readily come to understand and support the course I am going to follow.

The decisions which I have made will require rapid change. Those decisions have not, however been taken hastily. They result from rational consideration which I have given over a period of time to the future of the Labour Party.

I will not be seeking re-election as leader of the Labour Party. In order to ensure that the new leadership elections can be completed without delay, I will be proposing to the special National Executive Committee meeting tomorrow [Tuesday] that the elections be held as quickly as proper organisation allows. The elections will therefore take place in the second half of June.

My resignation from the position of leader of the Labour Party will take effect on the date of the elections. The deputy leader Roy Hattersley shares my view of the course which must be followed and will be acting accordingly.

This timetable will make it possible for the Parliamentary Labour Party to elect a new shadow Cabinet well before the summer recess. In providing for these developments, I am seeking to ensure that the Labour Party can get on with its work with maximum speed and effectiveness.

This will prove to be particularly important when the Government has a small majority and faces the continuing and very deep economic difficulties that it has caused for the country. In these circumstances, I am certain that it would not be right for the Labour Party to wait for the six months until October before establishing the leadership team and the political course which must be followed.

As the election process opens, I have only one piece of advice for the labour movement at every level: do not feed and do not believe the press and broadcasting media in their reporting of these events. The Labour Party must conduct its own democratic election and do it in a way that brings credit and strength to the party. That was done in 1983. I am sure that it will be done again.

I am taking the opportunity of this statement to notify the Labour Party of my intention to seek election to the constituency section of the National Executive Committee at this year’s annual conference. My purpose in doing that is to try to continue to play an active and supportive part in sustaining the advances in democracy and policy which I believe to be vital to the future success of the party.

I want to record my heartfelt thanks to Roy Hattersley, the rest of the shadow Cabinet, and the National Executive Committee for their loyalty and for their hard work...

I also want to express my admiration for members of the Labour Party, old and new... I want them and the many others who have sent countless numbers of moving messages of support to Glenys and myself in the last three days to know that I deeply appreciate their great kindness.

I assure them very firmly that the action that I am taking is an essential act of leadership. It is not to do with any personal sensitivity - it arises entirely from my desire to see that the Labour Party will gain further strength and be better able to serve the people of Britain and the wider world community...

There will be many opportunities to consider the causes and consequences of last Thursday’s election result. I will not dwell on them here.

I will content myself, for the moment, with drawing attention to the words of the former treasurer of the Conservative Party, Lord McAlpine, in yesterday’s Sunday Telegraph:

“The heroes of this campaign,” said Lord McAlpine, “were Sir David English, Sir Nicholas Lloyd, Kelvin McKenzie and the other editors of the grander Tory press. Never in the past nine elections have they come out so strongly in favour of the Conservatives. Never has their attack on the Labour Party been so comprehensive... This was how the election was won, and if the politicians, elated in their hour of victory, are tempted to believe otherwise, they are in real trouble next time.”

Lord McAlpine could not be expected to acknowledge the degree of misinformation and disinformation employed in the attacks on the Labour Party, but in all other respects his assessment is correct.

The government elected on 9 April 1992 does not have and will not develop the policies necessary to strengthen the British economy and will not try to address the injustices in British society.

My great regret is that I failed to ensure that enough people understood that and the implications which it has for the future. My sorrow is that millions, particularly those who do not have the strength to defend themselves, will suffer because of the election of another Conservative government.

I make and I seek no excuses, and I express no bitterness when I say that the Conservative-supporting press has enabled the Tory Party to win yet again when the Conservative Party could not have secured victory for itself on the basis of its record, its programme or its character.

The relationship between the Conservative Party and those newspapers which Lord McAlpine describes as being edited by “heroes” is a fact of British political life. I did think that it would be possible this time to succeed in achieving change in spite of that. Clearly it wasn’t. Success will therefore have to wait. But it will come, and I will work for it.
 
Back
Top Bottom