Kwanini kuwekeza kwenye Ardhi usiyo ijua?

Kwanini kuwekeza kwenye Ardhi usiyo ijua?

Joined
Mar 9, 2022
Posts
5
Reaction score
1
Kwako Mwananchi,

Nchini kwetu kumekua na migogoro mingi au usumbufu mwingi wa masuala ya ARDHI, Moja ya sababu inayochangia migogoro mingi ya ardhi Nchini ni kununua eneo la Ardhi kimazoea au kiholela. Mfano ( A) Imezoelekea kununua eneo la Ardhi kwa kushirikisha Serikali ya mtaa husika,Muuzaji,Mnunuzi na baadhi ya mashaidi. Watu wanaandikishana maisha yanaendelea,
(B) Kiholela,kwakua mnunuzi na muuzaji wanafahamiana basi wanauziana kwa taratibu za kufahamiana, urafiki wao au undugu wao.
Jambo moja la kujua ni kwamba kununua eneo la Ardhi kwa kushirikisha Serikali ya mtaa husika na mashahidi wengine hakukupi hakika ya moja kwa moja ya usalama wa eneo lako.

Jambo la kuzingatia.
Mshirikishe mtaalamu wa Ardhi(Land surveyor) kutoka kampuni binafsi au serikalini.

Mtaalamu wa Ardhi(Land Surveyor) atafanyanini?
Mtaalamu wa Ardhi atatafuta taarifa za eneo husika(Data search),atachukua mipaka ya eneo kwa kutumia kifaa maalumu mara nyingi ni GPS YA MKONONI nakwenda kutafuta taarifa za eneo husika.

Matokeo ya utafutaji wa taarifa yatajibu maswali muhimu kama;
1
Je eneo limepangiwa matumizi gani kitaalamu? isije ikawa unanunua eneo la makaburi au viwanda na wewe una lengo la kufanya makazi, itakula kwako.
2Je eneo linasifa ya kupimika iliupate hati miliki?
3Je eneo husika lilishawahi kupimwa au linaumiliki wowote kisheria?
4Je ukubwa uliotajiwa na muuzaji ni ukubwa halisi wa eneo husika? au umeambiwa ni ekari moja na kumbe ni robo tatu.
5 Je eneo ni sehemu ya barabara? kuepuka Bomoa Bomoa isiyo na malipo kwako.

Mwisho
Ukizingatia jambo ilo utakua katika usalama mkubwa wewe pamoja na Ardhi yako.

Credit.
LAND GENERAL PLANNING COMPANY LTD
KIBAHA,MAIL MOJA.
 
USINUNUE ARDHI BILA KUWA NA MAJIBU YA MASWALI YA FUATAYO.
1
Je eneo limepangiwa matumizi gani kitaalamu? isije ikawa unanunua eneo la makaburi au viwanda na wewe una lengo la kufanya makazi, itakula kwako.
2Je eneo linasifa ya kupimika iliupate hati miliki?
3Je eneo husika lilishawahi kupimwa au linaumiliki wowote kisheria?
4Je ukubwa uliotajiwa na muuzaji ni ukubwa halisi wa eneo husika? au umeambiwa ni ekari moja na kumbe ni robo tatu.
5 Je eneo ni sehemu ya barabara? kuepuka Bomoa Bomoa isiyo na malipo kwako.

Kwa kujibu maswali hayo unaweza kuepuka migogoro mingi ya Ardhi inayoweza kuepukika mapema.

✌️.
 
Back
Top Bottom