Kwanini kuwepo na vibarua (deiwaka) Tanzania wakati hawana haki zozote kisheria kama sio unyanyasaji?

Idrissou02

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2018
Posts
354
Reaction score
656
Habari wakuu
Naomba niwasilishe hii hoja kwenu.
Kima cha chini cha mshahara wa deiwaka kilichowekwa kisheria ni tsh 4400 kwa siku hapa nchini kwetu Tanzania. Kwa mkoa wa dar es salaam, mtu ukimlipa hela iyo kwa siku ni kumuonea kulingana na kazi ngumu wanazofanya.

Lakini mshahara huo sio hoja kubwa, hoja kubwa ni kwamba hawa deiwaka huwa hawana mkataba na waajiri, hivyo wakipatwa na suala lolote kazini, mwajiri hatoshurutishwa kisheria kumuudumia uyo kibarua aliepatwa na tatizo kwani kuna sheria za kulinda haki za wafanyakazi wenye mikataba tu.

Sasa kwa hali hii, inakuaje serikali inaruhusu utumikaji wa vibarua wakati hawajatengeneza chombo chochote cha kuwatetea. Au ndo kwasababu wana shida kwaio wanakua hawana haki?
Asikwambie mtu ndugu zangu, viwanda hapa bongo vinakua na kuendeshwa na hawa vibarua, kazi wanayofanya ni kazi ambayo walistahili angalau tsh 15,000 kwa siku. Angalia jinsi wenzetu katika nchi zilizoendelea wanalipa deiwaka. Nimefatilia nchi ya Canada nimeona deiwaka wengi wanalipwa kwanzia dola 64 kwa siku, sawasawa na 148,000 za kitanzania.

Wanasema nchi imepata uhuru lakini ukweli ni kwamba uhuru huu wanao wenye hela tu sio watu wenye hali ya chini!!!!!! Kufanyishwa kazi ngumu kwa sh 4,000 kwa masaa 12 na kutokua na huduma yeyote ya kukulinda ukiwa kazini huo ni utumwa kabisa.

Maoni yenu tafadhali!!.
 
Watakuaja vibaraka wa CCM kukwambia hapa
''Kama wanalipwa pesa ndogo waache Kazi watafanya wanaohitaji"
Hii Nchi ya kiwendawazimu sana Aisee!
 
Habari wakuu
Naomba niwasilishe hii hoja kwenu.
Kima cha chini cha mshahara wa deiwaka kilichowekwa kisheria ni tsh 4400 kwa siku hapa nchini kwetu Tanzania. Kwa mkoa wa dar es salaam, mtu ukimlipa hela iyo kwa siku ni kumuonea kulingana na kazi ngumu wanazofanya.

Lakini mshahara huo sio hoja kubwa, hoja kubwa ni kwamba hawa deiwaka huwa hawana mkataba na waajiri, hivyo wakipatwa na suala lolote kazini, mwajiri hatoshurutishwa kisheria kumuudumia uyo kibarua aliepatwa na tatizo kwani kuna sheria za kulinda haki za wafanyakazi wenye mikataba tu.

Sasa kwa hali hii, inakuaje serikali inaruhusu utumikaji wa vibarua wakati hawajatengeneza chombo chochote cha kuwatetea. Au ndo kwasababu wana shida kwaio wanakua hawana haki?
Asikwambie mtu ndugu zangu, viwanda hapa bongo vinakua na kuendeshwa na hawa vibarua, kazi wanayofanya ni kazi ambayo walistahili angalau tsh 15,000 kwa siku. Angalia jinsi wenzetu katika nchi zilizoendelea wanalipa deiwaka. Nimefatilia nchi ya Canada nimeona deiwaka wengi wanalipwa kwanzia dola 64 kwa siku, sawasawa na 148,000 za kitanzania.

Wanasema nchi imepata uhuru lakini ukweli ni kwamba uhuru huu wanao wenye hela tu sio watu wenye hali ya chini!!!!!! Kufanyishwa kazi ngumu kwa sh 4,000 kwa masaa 12 na kutokua na huduma yeyote ya kukulinda ukiwa kazini huo ni utumwa kabisa.

Maoni yenu tafadhali!!.
basi kianzishwe chama cha kutetea vibarua
 
Jiajiri tu mkuu, vibiashara vya kijinga tu unaweza kuingiza 10,000/= day.

Hata muosha magari kienyeji tu bila mashine hakosi 10,000/= per day.

Kuna vibiashara mjinga tu unaingiza hela kiulani bila kutumia nguvu huku unapiga miluzi.

Kuliko kuteswa na wahindi kwa buku 4 bora ufunguwe genge la nyanya uweke na maji utapata pesa kuliko hayo mateso ya wahindi, tena nawasifu vijana waliojiongeza kuwa bodaboda wanatumia akili zao vizuri shida tu hawana nidhamu barabarani.

Ila mwisho kabisa dunia haiko fair lazima wawepo watumwa wawe punda wa binadamu wengine, ukijitambuwa ndio unakataa upunda endesha hata bodaboda kuliko kuwa punda wa wahindi.
 
basi kianzishwe chama cha kutetea vibarua
Nani ataanzisha? Maana tatizo litakua vyanzo vya kipato vya chama icho. Utawachaji shilingi ngapi deiwaka kwa mwezi?....suluhisho apo naona ni kuundwa kwa sheria mpya tu ya kulinda vibarua au kusitishwa kabisa kwa vibarua, kila mfanyakazi apewe mkataba rasmi
 
SAWA MKUU
 
Najaribu kuwaza kwa sauti, hawa wazoa taka nao tuandikishane mkataba [emoji3][emoji3][emoji3],

Jambo hili lilishawahi nitokea kipindi nasimamia ujenzi pahali, tukakubaliana na jamaa moja kukata miti na kuchimba visiki kwa 200K. Jamaa akaawaita washikaji zake kama 3 hivi, deiwaka moja akaongezeka wakawa 4 na wakagawana miti ile na kazi ikaanza.

Kati kati ya kazi deiwaka akapasua kidole gumba kwa shoka kiasi ambacho kingozi kidogo ndo kikabaki kushika kidole. Kwa sababu nishauza kazi nikaketi pembeni nione yule jamaa anafanyaje kwa yule mwamba aliyepasua kidole, Asee huwezi amini jamaa alimkataa na hakutaka jihusisha na yule mwamba alojikata na shoka.

Nlivyoona amemkataa tukaita boda mm na mwenzangu na kumwelekeza apelekwe Hospital akatibiwe. yule alouziwa kazi ndo tukampa hela ya kwenda naye hospital, baada ya dk 15 hiv jamaa akarudi anasema hela haitoshi, nikaona isiwe tabu nikampatia nyingine. Japokuwa aliifikisha na kulipa kila kitu lkn aliipiga na ile hela kidogo.

Baadae wakarudi baada ya yule mwamba kushonwa vizuri nikamuuliza yule jamaa nlomuuzia kazi vipi unamlipa huyu alojikata bei gani maana hataendelea tena, jamaa akagoma kabisa yule mwamba kupata chochote, ikabidi niwe mkali nikachukua 10k kati ya ile 200k nikampatia yule mwamba akajiuguze.
 
Habari wakuu
Naomba niwasilishe hii hoja kwenu.
Kima cha chini cha mshahara wa deiwaka kilichowekwa kisheria ni tsh 4400 kwa siku hapa nchini kwetu Tanzania. Kwa mkoa wa dar es salaam, mtu ukimlipa hela iyo kwa siku ni kumuonea kulingana na kazi ngumu wanazofanya.

Lakini mshahara huo sio hoja kubwa, hoja kubwa ni kwamba hawa deiwaka huwa hawana mkataba na waajiri, hivyo wakipatwa na suala lolote kazini, mwajiri hatoshurutishwa kisheria kumuudumia uyo kibarua aliepatwa na tatizo kwani kuna sheria za kulinda haki za wafanyakazi wenye mikataba tu.

Sasa kwa hali hii, inakuaje serikali inaruhusu utumikaji wa vibarua wakati hawajatengeneza chombo chochote cha kuwatetea. Au ndo kwasababu wana shida kwaio wanakua hawana haki?
Asikwambie mtu ndugu zangu, viwanda hapa bongo vinakua na kuendeshwa na hawa vibarua, kazi wanayofanya ni kazi ambayo walistahili angalau tsh 15,000 kwa siku. Angalia jinsi wenzetu katika nchi zilizoendelea wanalipa deiwaka. Nimefatilia nchi ya Canada nimeona deiwaka wengi wanalipwa kwanzia dola 64 kwa siku, sawasawa na 148,000 za kitanzania.

Wanasema nchi imepata uhuru lakini ukweli ni kwamba uhuru huu wanao wenye hela tu sio watu wenye hali ya chini!!!!!! Kufanyishwa kazi ngumu kwa sh 4,000 kwa masaa 12 na kutokua na huduma yeyote ya kukulinda ukiwa kazini huo ni utumwa kabisa.

Maoni yenu tafadhali!!.
Kwanza kabisa unapaswa kuelewa kwamba vibarua hata Ulaya, Amerika, China na duniani kote wapo na wanatambulika kulingana na sheria za nchi husika na hawataondoka sababu kuu ni aina ya kazi wanazofanya sio za kitaalamu kwa maana ya professional work, zaidi ni mtu kafundishwa kushika nondo kuitoa kwenye mashine na kuipanga sehemu fulani na kuipakia kwenye lorry au kafundishwa kukunja nguo na kuzipakia kwenye boksi, huyo huwezi kumuita professional na hawezi kuwa professional kwa maana ya professional.

Kimsingi kibarua anatambulika kisheria kwenye The Minimum Wages Act itafute itakuonyesha kila sekta kibarua anapaswa kulipwa kiasi gani na imeboreshwa kiasi fulani.

Sasa Kuna calculation zimefanyika ili kumuwezesha kibarua kupata haki ya kisheria ya malipo yake kulingana na kazi anayofanya na elimu yake.

Kumbuka hata mishahara ya professionals huwa inakuwa calculated kwa siku Ila wanaongezewa baadhi ya malipo kama nauli,lunch, nyumba, simu nk kulingana na mwajiri anavyoona inafaa ndio maana inakuwa mikubwa na kwa sababu analipwa kwa mkupuo kwa mwezi na sio kwa siku (daily basis) Ila kama akilipwa kwa siku unakuta akikatwa Kodi na makato mengine analipwa kama 35 kwa siku tena huyo ni ofisa Ila inategemea na mshahara wake sasa.

Kasome uajiriwe ili ulipwe kwa mwezi plus pension na marupurupu mengine otherwise utaishia kulalamika tu wakati sheria inawatambua na imeboreshwa kiasi.

Ila hussle ya aliyesoma kupata kazi nayo sio rahisi kama ambavyo daily contract worker anavyopata kazi kirahisi maana huyu mwingine ni permanent and pensionable pia.

Sasa the choice is yours, be my guest.
 
Back
Top Bottom