Ikiwa Mungu anatoa muongozo wake kwa kupitia roho mtakatifu basi hakuwa na haja ya kuleta mitume wala Yesu asingekuja duniani! Kumbuka wanafunzi wa Yesu walimuona Yesu akisali na wakamuuliza na wao wasali vp? kwanini hakuwaachia roho mtakatifu awafundishe kusali kisirisiri kila mmoja? badala yake aliwafundisha nini waseme na si ndo sala mnayoitumia madhehebu yote hii? hata kama kuna nyengine mnatofautiana lakini sidhani kama mnapingana kwenye sala hii.Roho Mtakatifu
Hiki kisingizio cha kuongea na roho mtakatifu ndo maana kila siku mnapata watu wanaojiita manabii, mara wameenda mbinguni na kuongea na Yesu n.k., na kama utaangalia vizuri utagundua kwamba huu upotoshaji ulianza kwa Paulo coz yeye hakuwahi kumuona Yesu lakini ilimbidi awaaminishe watu kwa kusema katokewa na Yesu mafundisho yake yapate uzito.
Sorry kama nimekukwaza kiimani, lakini nia yangu ni kujaribu kuangazia tu mapungufu katika kuegemea kwenye kitu ambacho huwezi kuki-quote na kikawa reference ya ibada.