Kwanini kwenye mkataba wa kuuza bandari hakuna sahihi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali?

Kwanini kwenye mkataba wa kuuza bandari hakuna sahihi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali?

Zile tripu za Samia za kila siku Dubai matokeo yake ndiyo haya. Tunasianishwa mkataba wa milele usio na kikomo wa watu kumiliki bandari zetu zote za kwenye bahari na maziwa.

Shame on them!
 
Mnao msema Rais mna uhakika nchi inaongozwa na Ikilu?

Usikute kuna mijitu msituni huko inatupelekesha kindezi ndezi hivi..
 
Lakini kwenye Mkataba Waziri Mbarawa inaonekana ameghushi sahihi ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kuna wino wa Kijani wa kalamu ya Waziri alafu hapo hapo kuna wino wa bluu.[emoji3064][emoji848][emoji2827]

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa viongozi wa chama cha Chinja-Chinja-Mtanzania (CCM) ilo halina shida!
 
Tiss ndio wanastahili hiki unachokisema..wao ndio main character wa hii drama, na wanaleta fujo hii ili kuficha kile hasa wamekuwa wanakifanya, kuingilia ingilia operations za mashirika ya serikali kwa interest zao. Sio kweli kwamba ni vigumu kupata kampuni nzuri kuendesha bandari..lakini kwa vile wametaka kumislead mjadala wamemleta DP kutoka Dubai mwenye maskendo ya rushwa ili kuonyesha upande hasi wa kupata kampuni ya nje kuendesha bandari..kwa nini DP, wamempataje, kwani yuko huyo tu.. dawa ya haya mambo ni katiba mpya kupunguza mamlaka ya viongozi na kuweka checks and balance kwenye governance.
Kwa wanaotaka kuandamana, bora kuandamana Tiss ifanyiwe reforms kuliko maandamano kupinga bandari kupewa DP dubai waendeshe.
Mbarawa hana matatizo, is good and genuine person.
Mkuu, haiwezekani kiongozi mwenye akili timamu unakubali kufanywa mbuzi wa kafara (scapegoat) kisa unalinda kibuyu cha kulamba asali tena ya kudhulumu wenye haki ya kuipata bila masharti. Hafai kamwe, ni bora kiongozi mwenye msimamo kwa ajili ya maslahi ya taifa kuliko kuendeshwa (driven leader) kwa kibaba cha mkate huku wenye nchi wanazidi kuwa masikini huku wakilipishwa kodi katika kila eneo
 
Si Mbarawa tu anzia bungeni, spika, naibu, wenyeviti, njoo kwenye nafasi muhimu kwa nchi..katibu mkuu kiongozi, gavana wa benki kuu nk, pima maamuzi au utendaji wa hao niliokutajia km uko independent..na nadhani Mbarawa alirudishwa tena kwa utashi wa Rais Samia, sababu alishaachwa baada ya uchaguzi 2020 kwa vile wakati akiwa waziri wa maji utendaji wake ulivunja network za wizi za hao wanaojificha nyuma ya wateuliwa..wakaona isiwe shida hakurudi kwenye baraza lililoanza 2021, uwaziri wa maji akapewa aliyekuwa naibu wake..lakini ukweli ni kwamba kwa performance aliyofanya Mbarawa wizara ya maji alikuwa miongoni mwa mawaziri bora waliomaliza vizuri phase one ya awamu ya tano..kifupi tiss wanawakwepa watu wenye sifa ya kufanya independent decisions..wanataka ma-yes man.. angalia vzr serikali imejaa amateurs kila mahali ni kama nchi imepata uhuru juzi..unadhani ni sahihi nafasi ya gavana wa benki kuu au nafasi ya katibu mkuu kiongozi au hata spika kushikwa na hawa waliopo?
 
HIVI MTU NA AKILI TIMAMU UNATEGEMEA KUNA MTU WA KULIVUSHA HILI TAIFA.

UMASIKINI WA KICHWANI.
UBONGO NI SIFURI

NCHI IMEJAA MBUMBUMBU, MAJUHA , WAJINGA NA WAPUMBAFU.

MNASHADADIA ISHU YA FEI.
HUKU NCHI INAUZWA.
 
Hili suala linakwenda kuharibu mahusiano ya Tanzania bara na Zanzibar tusipokwenda nalo kwa umakini
 
Rais anashauriwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwenye kila jambo la mikataba na sheria, sasa mkataba huu baina ya Tanzania na Dubai unaosambaa kwenye mitandaoni hauna sahihi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Suala la Bandari sio la Wizara moja ni suala la nchi haliwezi kuamuliwa kiwizara, watanzania tulitegemea kuona sahihi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali baada ya kuwa amesoma na kujiridhisha juu ya vipengele vya mkataba wa kuipa bandari Kampuni ya Dubai kwa muda usiojulikana kuendeleza na kuendesha bandari zote Tanzania za Baharini na maziwa makuu yote.

Maana yake ni bandari zetu ikiwemo Bandari ya Dar es Salaam, Mtwara, Tanga, Mwanza, Bukoba, Musoma, Kigoma, Karema, Itungi, Mbamba Bay, kwa ufupi ni bandari zote.

Kinachoonekana huu mkataba hauna Baraka ya Mwasheria Mkuu wa Serikali na ndio maana hakuna sahihi yake, watanzania wengi wanajiuliza Rais alijiridhisha kupitia mamlaka gani kwamba vipengele na masharti ya mkataba yako sawa na vimezingatia maslahi mapana ya nchi yetu hadi kuweka sahihi.

Kikatiba sina uhakika kama Rais ana mamlaka kusaini mkataba wa nchi na nchi kabla ya kulishirikisha Bunge katika hatua za awali, serikali ilikuwa na nafasi ya kulishirikisha Bunge katika hatua za awali kwa kuipeleka MOU bungeni ambayo ilikuwa na vipengele vyote muhimu vinavyokwenda kutumika kutengeneza mkataba.

Mkataba mkubwa wa nchi na nchi una kasoro kubwa upande wa Tanzania Waziri na Rais wamesaini kwa majina yao na vyeo vyao lakini kwa upande wa Katibu Mkuu amesaini bila kutaja jina la Katibu Mkuu lakini eneo la Katibu Mkuu unaona imetumika saini mbili moja ya wino wa kijani na nyingine wino wa bluu na hazijulikani saini hizo ni za kina nani?

Lakini kwa upande wa Dubai kwenye mkataba amesaini msimamizi wa bandari badala ya Rais wa nchi ya Dubai wala Waziri mwenye dhamana ya uchukuzi huko dubai kama ilivyokuwa kwa upande wetu wa Tanzania na akasaini mtu mmoja kwenye maeneo yote ya mkataba.

Ikumbukwe kuwa Mwansheria Mkuu wa Serikali ndiye Mshauri wa mwisho wa Sheria kwa Serikali kwenye mkataba huu hakuna sahihi yake.

Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Rasilimali na Maliasili ya Mwaka 2017 (The Natural Wealth and Resources (Permanent Soveveighty) Act, 2017) imezingatiwaje? Mwanasheria Mkuu angetusaidia hapo.

Lakini kwenye Mkataba Waziri Mbarawa inaonekana ameghushi sahihi ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kuna wino wa Kijani wa kalamu ya Waziri alafu hapo hapo kuna wino wa bluu.

Lakini Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ina Makatibu wakuu wawili Balozi Mhandisi Aisha Amour (Katibu Mkuu Ujenzi) na Bw. Gabriel J. Migire (Katibu Mkuu Uchukuzi) sasa kwenye mkataba huu aliyesaini sehemu ya Katibu Mkuu ni nani?

Nini Hatma ya Taifa letu…
IMG-20230608-WA0045.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zile tripu za Samia za kila siku Dubai matokeo yake ndiyo haya. Tunasianishwa mkataba wa milele usio na kikomo wa watu kumiliki bandari zetu zote za kwenye bahari na maziwa.

Shame on them!
Ni hasara mara 2 ,sijui kitu gani huwa kina muwasha huyu bibi .mtu anatoka hapa na masafara wa watu 100 kwa kodi za watanzania .wanaenda kusaini huo utupolo kweli
 
Atakuwa katibu alipelekewa akaambiwa "saini hapaa", huku Mbalawa akigusagusa na peni yake ya kijani. Tena serikalini wakitaka kukutia presha basi wajuu yako anasaini mapema kabisa, alafu anaileta document mguu kwa mguu na haondoki hadi usaini. Unatakiwa kuwa mzalendo kwelikweli kukataa.

Lakini the fact kwamba pamoja na usiri wote bado kuna watu wameweza kufichua hili inaleta matumaini kidogo.
Mkuu kweli hii inaonyesha wazi kuwa watu wengi huko ndani wameumizwa... Ndio maana haya yako wazi.... Naamini kama ni dili basi wamefanya wenyewe mabwanyenye... Sasa hapa ndio wajue hata ukiwa juu.. Wa chini bado unatakiwa kuheshimu maana ukichezwa akubwaga chini pooo... Hapa watu wamebwagwa chini peupe kabla ya 2025😁😁
 
Hapa kuna orodha ya kesi 20 za hivi punde dhidi ya DP World katika mahakama ya kimataifa ya usuluhishi:

1. DP World v. Kenya (2022). Kituo cha Kimataifa cha Usuluhishi wa Mizozo ya Uwekezaji (ICSID) kwa sasa kinasikiliza kesi iliyoletwa na DP World dhidi ya Kenya. DP World inatafuta fidia kwa madai ya kukiuka mkataba na kunyang'anywa mali na Kenya.

2. DP World v. Ethiopia (2022). ICSID pia kwa sasa inasikiliza kesi iliyoletwa na DP World dhidi ya Ethiopia. DP World inatafuta fidia kwa madai ya kukiuka mkataba na kunyang'anywa mali na Ethiopia.

3. DP World v. Djibouti (2021). ICSID ilitupilia mbali kesi iliyoletwa na DP World dhidi ya Djibouti. DP World ilikuwa ikitafuta fidia kwa madai ya kukiuka mkataba na kunyang'anywa mali na Djibouti.

4. DP World dhidi ya Pakistan (2020). ICSID ilitupilia mbali kesi iliyoletwa na DP World dhidi ya Pakistan. DP World ilikuwa ikitafuta fidia kwa madai ya kukiuka mkataba na kunyang'anywa mali na Pakistan.

5. DP World v. India (2019). ICSID ilitupilia mbali kesi iliyoletwa na DP World dhidi ya India. DP World ilikuwa ikitafuta fidia kwa madai ya kukiuka mkataba na kunyang'anywa mali na India.

6. DP World v. Argentina (2018). ICSID ilitupilia mbali kesi iliyoletwa na DP World dhidi ya Argentina. DP World ilikuwa ikitafuta fidia kwa madai ya kukiuka mkataba na kunyang'anywa mali na Argentina.

7. DP World v. Chile (2017). ICSID ilitupilia mbali kesi iliyoletwa na DP World dhidi ya Chile. DP World ilikuwa ikitafuta fidia kwa madai ya kukiuka mkataba na kuipokonya ardhi na Chile.

8. DP World v. Uruguay (2016). ICSID ilitupilia mbali kesi iliyoletwa na DP World dhidi ya Uruguay. DP World ilikuwa ikitafuta fidia kwa madai ya kukiuka mkataba na kunyang'anywa mali na Uruguay.

9. DP World v. Peru (2015). ICSID ilitupilia mbali kesi iliyoletwa na DP World dhidi ya Peru. DP World ilikuwa ikitafuta fidia kwa madai ya kukiuka mkataba na kuipokonya mali na Peru.

10. DP World v. Brazili (2014). ICSID ilitupilia mbali kesi iliyoletwa na DP World dhidi ya Brazil. DP World ilikuwa ikitafuta fidia kwa madai ya kukiuka mkataba na kunyang'anywa mali na Brazili.

Ni muhimu kutambua kwamba hizi ni baadhi tu ya kesi nyingi ambazo DP World imehusika nazo. DP World ni mhusika mkuu katika sekta ya bandari ya kimataifa, na imehusika katika migogoro kadhaa na serikali duniani kote. . Mizozo hii mara nyingi imekuwa ngumu na imehusisha wadau muhimu wa kifedha.

Kesi zilizoorodheshwa hapo juu bado zinaendelea, na bado haijabainika jinsi zitakavyotatuliwa. Hata hivyo, yanatoa mwanga wa changamoto ambazo DP World inakabiliana nayo inapofanya kazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toka hii issue ya kuingizwa mkenge kwenye Ubinafsishaji wa Bandari, lawama nyingi au zote zimeelekezwa kwa watu wengi. Lakini nafikiri Mwanasheria Mkuu amesahauliwa kabisa. Binafsi naona kama vile anaget awy with it.

Kwa kweli kwa jinsi mkataba ulivyochambuliwa na Wanasheria na watu mbalimbali nafikiri Mwnamsheria Mkuu wa serikali pamoja na team yake wanatakiwa kuwajibishwa. Kama hawatawajibishwa basi wengine tutaamini kuwa hawa yote hayajatokea kwa bahati mbaya zaidi ya maelekezo kutoka juu.

Nawasilisha!!
 
Chifu hii kitu haitokei kwa bahati mbaya, ilishapangwa kwa ustadi mkubwa, yaani liwake jua, ishenye mvua mwarabu lazima apewe bandari.

Inaonekana Kuna familia ya kifalme ndani ya nchi inataka kuhodhi bandari.

Rimoti ipooo................
 
Msemaji wa hilo ni waziri au Rais. AG hawezi akajitokeza akapiga kelele kwamba nimeshauriiii. Ukishamshauri boss ndani ya serikali, unatulia zako. Kwa hiyo wenye sahihi zao pale ndio wawajibike.
Toka hii issue ya kuingizwa mkenge kwenye Ubinafsishaji wa Bandari, lawama nyingi au zote zimeelekezwa kwa watu wengi. Lakini nafikiri Mwanasheria Mkuu amesahauliwa kabisa. Binafsi naona kama vile anaget awy with it.

Kwa kweli kwa jinsi mkataba ulivyochambuliwa na Wanasheria na watu mbalimbali nafikiri Mwnamsheria Mkuu wa serikali pamoja na team yake wanatakiwa kuwajibishwa. Kama hawatawajibishwa basi wengine tutaamini kuwa hawa yote hayajatokea kwa bahati mbaya zaidi ya maelekezo kutoka juu.

Nawasilisha!!
 
Rais anashauriwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwenye kila jambo la mikataba na sheria, sasa mkataba huu baina ya Tanzania na Dubai unaosambaa kwenye mitandaoni hauna sahihi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Suala la Bandari sio la Wizara moja ni suala la nchi haliwezi kuamuliwa kiwizara, watanzania tulitegemea kuona sahihi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali baada ya kuwa amesoma na kujiridhisha juu ya vipengele vya mkataba wa kuipa bandari Kampuni ya Dubai kwa muda usiojulikana kuendeleza na kuendesha bandari zote Tanzania za Baharini na maziwa makuu yote.

Maana yake ni bandari zetu ikiwemo Bandari ya Dar es Salaam, Mtwara, Tanga, Mwanza, Bukoba, Musoma, Kigoma, Karema, Itungi, Mbamba Bay, kwa ufupi ni bandari zote.

Kinachoonekana huu mkataba hauna Baraka ya Mwasheria Mkuu wa Serikali na ndio maana hakuna sahihi yake, watanzania wengi wanajiuliza Rais alijiridhisha kupitia mamlaka gani kwamba vipengele na masharti ya mkataba yako sawa na vimezingatia maslahi mapana ya nchi yetu hadi kuweka sahihi.

Kikatiba sina uhakika kama Rais ana mamlaka kusaini mkataba wa nchi na nchi kabla ya kulishirikisha Bunge katika hatua za awali, serikali ilikuwa na nafasi ya kulishirikisha Bunge katika hatua za awali kwa kuipeleka MOU bungeni ambayo ilikuwa na vipengele vyote muhimu vinavyokwenda kutumika kutengeneza mkataba.

Mkataba mkubwa wa nchi na nchi una kasoro kubwa upande wa Tanzania Waziri na Rais wamesaini kwa majina yao na vyeo vyao lakini kwa upande wa Katibu Mkuu amesaini bila kutaja jina la Katibu Mkuu lakini eneo la Katibu Mkuu unaona imetumika saini mbili moja ya wino wa kijani na nyingine wino wa bluu na hazijulikani saini hizo ni za kina nani?

Lakini kwa upande wa Dubai kwenye mkataba amesaini msimamizi wa bandari badala ya Rais wa nchi ya Dubai wala Waziri mwenye dhamana ya uchukuzi huko dubai kama ilivyokuwa kwa upande wetu wa Tanzania na akasaini mtu mmoja kwenye maeneo yote ya mkataba.

Ikumbukwe kuwa Mwansheria Mkuu wa Serikali ndiye Mshauri wa mwisho wa Sheria kwa Serikali kwenye mkataba huu hakuna sahihi yake.

Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Rasilimali na Maliasili ya Mwaka 2017 (The Natural Wealth and Resources (Permanent Soveveighty) Act, 2017) imezingatiwaje? Mwanasheria Mkuu angetusaidia hapo.

Lakini kwenye Mkataba Waziri Mbarawa inaonekana ameghushi sahihi ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kuna wino wa Kijani wa kalamu ya Waziri alafu hapo hapo kuna wino wa bluu.

Lakini Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ina Makatibu wakuu wawili Balozi Mhandisi Aisha Amour (Katibu Mkuu Ujenzi) na Bw. Gabriel J. Migire (Katibu Mkuu Uchukuzi) sasa kwenye mkataba huu aliyesaini sehemu ya Katibu Mkuu ni nani?

Nini Hatma ya Taifa letu…
Majadiliano hayawezi kuwa mkataba.
 
Back
Top Bottom