Kwanini Landrover Defender zinapendwa sana?

"Ukitaka kwenda porini, nenda na land rover ila ukitaka kwenda porini na kurudi nenda na Land cruiser"
true story braza, hasa hako ka Baby defender ka kisasa ndio katawatia nyongo watu maana kana umeme mwingi.
 
Hio V8 ya petrol ukiikuta kwenye Discovery 2 ina balaa ina mbio na muungurumo wa kibabe sana.

Habari ya mafuta unaweza ukasahau kila ukikanyaga peda ya mafuta unaposikia ngurumo ya simba dume.
Katika discovery nazokubali ni discovery 2 V8! Ile mashine ukiiwasha tu sound lake ni noma na nusu. I feel like its the best sounding v8 engine pamoja na ile ya Range Rover P38 4.6 HSE
 
1PZ sijawahi kuzielewa kwa kweli ila 13B ni ya kibabe 😂😂😂!!!

1HZ ndio mashine ya ndima kwa miaka na miaka na still anaendelea kuitumia tu hata kwenye matoleo ya 2020! Siku akikatisha production ya 70 series watu wengi tutaumia sana.

Ila 1VD sijawahi itumia japo nikafeel pulling yake ila kwa body jepesi la 70 series itakuwa ina move sio kitoto.
 
Daah! Tuombe asifike huko. Au aamue kutoa LC automatic transmission sijui itakuaje Chief.
 
The same to Toyota Sequoia. Zote zina engine kubwa sana! I prefer Toyota Tacoma Trd V6 nzuri sana hasa upate stick shift
Nimefatana na Sequoia juzi liko kemchwa kemchwa namba C ila lina sticker ya V8! Ni noma sana lile dude sema zile gari ni kwa soko la US ndio maana yana engine za kibabe. US pesa ya mafuta sio ishu sana kwao.
 
Mie naonaga hii gari ya Mhindi iko over rated.. Serikalini walizishibokea sana miaka hiyo ila wakaona zinakufa mapema kuliko Landcruser ya mkonga, wakazi diss!
We nae toka lini land rover ni gari ya mhindi? Au umemaanisha nini?
 
Nimefatana na Sequoia juzi liko kemchwa kemchwa namba C ila lina sticker ya V8! Ni noma sana lile dude sema zile gari ni kwa soko la US ndio maana yana engine za kibabe. US pesa ya mafuta sio ishu sana kwao.
Off course US mafuta bei rahisi sana. Wanauza mafuta kwa gallon. Ambapo gallon yenye litre 4 ni kama dollar 2 tu.
 
Daah! Gari ngumu zote zinazidi kupotea sasa.
Na hii system ya hybrid ndio imeharibu kabisa. Mwisho utasikia LC 70 series hybrid
ile chuma hawawezi kuitia hybrid. Ni chuma ya kazi na ndio maana hawaziuzi US! Ni Australia, Uarabuni na Africa only ambako hamna mbwembwe za Exhaust gas Emission Policies.

Hizo sera zao za ajabu hapo marekani ndio zinaharibu magari! 70 series hazifati viwango vyao ndio maana hutakaa uikute USA ingawa wamarekani wanazitamani mno.
 
Huu uzi mtamu sana kuusoma wakuu tupieni madini.

Mimi nanatamani sana brand za Landrover, Nikaanza na Freelander ila changamoto zake zikanishinda nikapiga chini.
Nikipata hela nitarudi tena.
 
Hiyo Grenadier haitokuwa na jipya kwenye uwanja wa off road. Hawa gari zao wameweka injini za BMW ambapo mwenzao Land Rover Defender aliwahi kutumia na hazikufanya vizuri..
sema Landrover hakubase sana kutengeneza engine zenye cc kubwa kama cruiser.labda kwa discovery 3 and 4
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…