Kwanini Lucky Dube hatambuliki kama muasisi ama legend wa muziki wa reggae duniani?

Kwanini Lucky Dube hatambuliki kama muasisi ama legend wa muziki wa reggae duniani?

Mkuu ukisema Dube muasisi, utakuwa unampa maua zaidi ya anayostahili. Kuna wazee wa zamani walikuwa wanapiga culture hata Bob ni vile tu alikuwa popular sana.

Legend anastahili kabisa, uasisi big no.
 
Kundi la reggae la Wailers liliundwa mwaka 1963 (Bob Marley, Peter Tosh, Bunny Wailer n.k) na walitoa album yao ya kwanza mwaka 1965 (The Wailing Wailers). Lucky Dube alizaliwa mwaka 1964, maana yake akiwa na mwaka mmoja tu wapo watu tayari walishakuwa na album tayari. Legend - Yes, Pioneer - Definitely, big NO.
Hapa tumemaliza ila dube aliwafunika sana
 
The Wailing Wailers (Bob, Peter, Bunny) walifundishwa/mentored na Joe Higgs mwanzoni mwa 1960s, hapo tayari kina Jimmy Cliff, Toots and Mytals, Dennis Brown kusikika duniani.
Bob Marley aliamini katika ONE LOVE
Peter Tosh aliamini katika EQUAL RIGHTS Bunny Wailer yote. Hizo no slogans ni tofauti KABISA na Kwa Bob Marley ilikuwa rahisi sana kuwa promoted pamoja na uwezo wake kuweza kufikia dunia ya tatu zaidi kuliko hata Wacko Jacko...
 
Rasta zile zisikuchanganye mtoto mdogo wewe, Dube ni muimba kwaya tu kama Bahati Bukuku.

Dube tunamjua watu wa huku nchi za SADC.

Duniani huko nani anamjua kwa vya maana.
Muimba kwaya, nona vile vinanda vinawachanganya,

Well, muziki wake una ladha tofauti na nzuri (kwangu mimi). Ni mdau mkubwa sana wa reggae na kwangu Lucky Philip Dube is the best.

Ukiachana na Muasisi Bob, Kuna wengine wengi kama
culture (Joseph Hill)
Gregor Isaacs mzee wa taratiiib
Luciano
Burning spear
Maron usher n.k

Hawa wote wana mziki mzuri sana.
 
Fanya kusikiliza ngoma kama
Crisis
Slogan
One drop
Zion Train
Forever loving Jah
Who cap fit
One love
Zimbabwe
Natural mystic
Concrete jungle
We and them
So much trouble
War
No woman no cry
Baadhi tuu hizoo,
Robert Nesta Marley alijua, amejua na bado anaendelea kujua,
Ukitoka hapo kawasikilize steel pulse na ngoma zao Bodyguard, leave you House, Rollers skate, Man no sober, King James version,
Ukitoka hapo njoo kwa Nasio Fontaine na ngoma zake kama Itiopia, my defense
Kisha malizia kwa mwamba Joseph Hill na kundi lake la culture na ngoma zake kama Riverside, Addis Ababa, Humble African, too long,
Maliza na Babu Winston Rodney a.k.a burning spear na ngoma zake kama Days of slavery, Christopher Columbus, African teacher
Sikiliza hizo chache kisha utajua nafasi ya Dube ni ipi katika muziki wa reggae
 
Wakuu nawaheshimu sana kwa kuwa kanuni mojawapo ya ubinadamu sahihi ni kuheshimu usiemjua mpaka utakapomjuwa:

Mimi ni miongoni mwao wafuatliaji wa muziki wa aina tofauti duniani, kama POP na SOUL POP pia RNB ambayo ndiyo hupendwa na watu wengi duniani kwa kuwa ina vibe na kutoa passion kwa haraka..Pia nikajikuta nimependa huu muziki wa aina ya tatu wa REGGAE ambapo niwe mkweli nilianza kuupenda kutokana na nyimbo za huyu mwamba, nikajikuta pia nawafuatlia na wengine kama kina PETER TOSH,BUNNY WAILER,dingi mwenyewe BOB MARLEY, nk japo katika kufuatilia na kusoma maandiko miziki waliyoimba hawa waasisi ni REGGAE ya aina tofauti japo ujumbe ni ule ule.

Lakini ukweli huyu mwamba DUBE muziki wake ulisumbua na unasumbua masikio ya wengi Duniani na haswa Afrika,mimi huwa namfananisha na Diamond kibongo kwa kuwa aliiamsha REGGAE na kuimodify,jamaa nyimbo zake ni currently japo hata hao wengine zinaishi LAkini ukifuatilia katika orodha ya wakali na malegends wa REGGAE duniani tathmini hazimtaji huyu jamaa why?,Jamaa alifanya show USA na Amerika kusini kote huko na alijaza watu hata mkifuatlia live concert zake ambapo kwa haraka haraka hakuna mwanareggae kuanzia bob Marley kujaza kumbi kiasi kile then why?

Tathmini/machapisho yanawataja bob Marley,Senzo,TOSH,bunny wailer nk ila DUBE hayumo why? Hata Forbes hawamtaji katika ma GOAT au legends wa REGGAE sijajua alifeli wapi ktk muziki wake. .NAWASILISHA:
Sio kweli kwamba hatambuliki. Fuata hii link

 
Unajua maana na matumizi sahihi ya neno Muasisi au unakurupuka? Ni sawa na useme Samia ni muasisi wa CCM, unaweza kuzabwa vibao.

Kuna akina Alpha Blond, akina Peter Tosh, Bob Marley na wengineo hawa unawaweka wapi?
 
Kama data zipo sahihi, uzi unastahili kuishia hapa, vijana wote wa miaka ya 2000 wanapaswa kukuelewa.
Tatizo watoto wadogo huwa hawakai chini kwenye mkeka watusubirie wakongwe tupige funda kadhaa za Tembo, kisha tusokote tumbaku kwenye kiko na kubwia ugolo tayari kuwapa historia na elimu kwenye mambo kadha wa kadha.

Vijana ujuaji akienda online akasoma mbili tatu analeta ujuaji. Kuna kamoja juzi hapa kanakuja tuambia Michael Jackson ana ukali gani mbona hana maajabu, aiseee ilikuwa nusu tumtafute tumshitaki mahakamani kwa kosa la kutokujua anachokisema hadharani.
 
2000 sio chini wala juu ya hapo ni Mwaka 2000
Huu mwaka mna raha ukiulizwa mwaka 2055 utakua na umri gani huna haja ya kufikiri sana.

Back to the topic. Marley huwezi mfananisha na Dube.
Sio muasisi alikuja akaimba akatuburudisha na akaenda. Ni mwanamuziki mzuri tena nyimbo zake wakati wa ubaguzi zilikua kali sana.
 
Kwa kifupi LUCKY DUBE hakuwa mpambanaji kupitia reggae, yy alikuwa MWOGA licha ya kushuhudia na kuuishi UKATILI, UNYANYASAJi, DHULMA NA UBAGUZI yy alijikita katika kutousema UKWELI .

Badala yake alitafuta Amani kwa kutaka watu wapatane kama vile HAKI ipo isipokuwa wananchi hawajui ile HAKI inapatikana vp.

Tofauti na MANGULI wengine wa REGGAE MUSIC hawa walijitokeza na kusema ukweli, TABAKA fulani linalinyanyasa tabakq fulani.

Haki hakuna acheni dhulma 'DONT GIVE UP THE FIGHT.'
Haujasikiliza nyimbo zakw vema. Huyo Lucky Dube alikuwa na tungo tata enzi za Apartheid hapo South Africa wakati kaburu akiwatesa watu weusi.

Labda utafute nyimbo zake usikilize vizuri neno kwa neno
 
Tatizo watoto wadogo huwa hawakai chini kwenye mkeka watusubirie wakongwe tupige funda kadhaa za Tembo, kisha tusokote tumbaku kwenye kiko na kubwia ugolo tayari kuwapa historia na elimu kwenye mambo kadha wa kadha.

Vijana ujuaji akienda online akasoma mbili tatu analeta ujuaji. Kuna kamoja juzi hapa kanakuja tuambia Michael Jackson ana ukali gani mbona hana maajabu, aiseee ilikuwa nusu tumtafute tumshitaki mahakamani kwa kosa la kutokujua anachokisema hadharani.
Nenda nao taratibu akili zitakuwa sawa kadri wanavyokua.
 
Lucky Dube hafanyi Reggae,..kama ana nyimbo za mahadhi hayo basi hazizidi Tano,nikumbushe
Kumbe anaimba nini mzee bolingo? [emoji848]

Lucky Dube amekuja na reggae yenye vionjo vya tofauti na reggae ya kawaida yaani South African flavor. Reggae ya Lucky Dube inavionjo vya vinanda vya kwaya, waimbaji wa kwaya, na uimbaji wake ni phenomenal ni kama anahadithia kwa masikitiko au anatoa taarifa hivi kitu ambacho kipo sana kwenye reggae.
 
No woman no cry, stir up, redemption song etc, ukipata nyimbo ya dube ya reggae inaingia hapo kwa ubora, basi tutaanza kumfikiria dube.

Lucky dube ana ngoma kadhaa hivi ukisikiliza beats zake zinafanana na hata melody zake hazipo mbaaali saana, dube alijitahidi ila hakuwa bora kwangu, ila sio wa kuacha kuzungumziwa kabisa, hapo hata mie nashangaa kwanini hatajwi tajwi sababu ngoma zake zilibamba, sijui huko duniani ila kwa afrika alibamba, kama hakubamba huko duniani basi hio ndio sababu kuu.
 
Kwa kifupi LUCKY DUBE hakuwa mpambanaji kupitia reggae, yy alikuwa MWOGA licha ya kushuhudia na kuuishi UKATILI, UNYANYASAJi, DHULMA NA UBAGUZI yy alijikita katika kutousema UKWELI .

Badala yake alitafuta Amani kwa kutaka watu wapatane kama vile HAKI ipo isipokuwa wananchi hawajui ile HAKI inapatikana vp.

Tofauti na MANGULI wengine wa REGGAE MUSIC hawa walijitokeza na kusema ukweli, TABAKA fulani linalinyanyasa tabakq fulani.

Haki hakuna acheni dhulma 'DONT GIVE UP THE FIGHT.'
Prisoner alipiga akimaanisha wapambanaji waliokamatwa na kufungwa jela yaani Dube hakuwa mpambanaji aisee sema Wazulu wanambagua Dube kwa kuwa ni Mzimbabwe..
 
Back
Top Bottom