Kwanini Lucky Dube hatambuliki kama muasisi ama legend wa muziki wa reggae duniani?

Mkuu ukisema Dube muasisi, utakuwa unampa maua zaidi ya anayostahili. Kuna wazee wa zamani walikuwa wanapiga culture hata Bob ni vile tu alikuwa popular sana.

Legend anastahili kabisa, uasisi big no.
 
Hapa tumemaliza ila dube aliwafunika sana
 
The Wailing Wailers (Bob, Peter, Bunny) walifundishwa/mentored na Joe Higgs mwanzoni mwa 1960s, hapo tayari kina Jimmy Cliff, Toots and Mytals, Dennis Brown kusikika duniani.
Bob Marley aliamini katika ONE LOVE
Peter Tosh aliamini katika EQUAL RIGHTS Bunny Wailer yote. Hizo no slogans ni tofauti KABISA na Kwa Bob Marley ilikuwa rahisi sana kuwa promoted pamoja na uwezo wake kuweza kufikia dunia ya tatu zaidi kuliko hata Wacko Jacko...
 
Rasta zile zisikuchanganye mtoto mdogo wewe, Dube ni muimba kwaya tu kama Bahati Bukuku.

Dube tunamjua watu wa huku nchi za SADC.

Duniani huko nani anamjua kwa vya maana.
Muimba kwaya, nona vile vinanda vinawachanganya,

Well, muziki wake una ladha tofauti na nzuri (kwangu mimi). Ni mdau mkubwa sana wa reggae na kwangu Lucky Philip Dube is the best.

Ukiachana na Muasisi Bob, Kuna wengine wengi kama
culture (Joseph Hill)
Gregor Isaacs mzee wa taratiiib
Luciano
Burning spear
Maron usher n.k

Hawa wote wana mziki mzuri sana.
 
Fanya kusikiliza ngoma kama
Crisis
Slogan
One drop
Zion Train
Forever loving Jah
Who cap fit
One love
Zimbabwe
Natural mystic
Concrete jungle
We and them
So much trouble
War
No woman no cry
Baadhi tuu hizoo,
Robert Nesta Marley alijua, amejua na bado anaendelea kujua,
Ukitoka hapo kawasikilize steel pulse na ngoma zao Bodyguard, leave you House, Rollers skate, Man no sober, King James version,
Ukitoka hapo njoo kwa Nasio Fontaine na ngoma zake kama Itiopia, my defense
Kisha malizia kwa mwamba Joseph Hill na kundi lake la culture na ngoma zake kama Riverside, Addis Ababa, Humble African, too long,
Maliza na Babu Winston Rodney a.k.a burning spear na ngoma zake kama Days of slavery, Christopher Columbus, African teacher
Sikiliza hizo chache kisha utajua nafasi ya Dube ni ipi katika muziki wa reggae
 
Sio kweli kwamba hatambuliki. Fuata hii link

 
Unajua maana na matumizi sahihi ya neno Muasisi au unakurupuka? Ni sawa na useme Samia ni muasisi wa CCM, unaweza kuzabwa vibao.

Kuna akina Alpha Blond, akina Peter Tosh, Bob Marley na wengineo hawa unawaweka wapi?
 
Kama data zipo sahihi, uzi unastahili kuishia hapa, vijana wote wa miaka ya 2000 wanapaswa kukuelewa.
Tatizo watoto wadogo huwa hawakai chini kwenye mkeka watusubirie wakongwe tupige funda kadhaa za Tembo, kisha tusokote tumbaku kwenye kiko na kubwia ugolo tayari kuwapa historia na elimu kwenye mambo kadha wa kadha.

Vijana ujuaji akienda online akasoma mbili tatu analeta ujuaji. Kuna kamoja juzi hapa kanakuja tuambia Michael Jackson ana ukali gani mbona hana maajabu, aiseee ilikuwa nusu tumtafute tumshitaki mahakamani kwa kosa la kutokujua anachokisema hadharani.
 
2000 sio chini wala juu ya hapo ni Mwaka 2000
Huu mwaka mna raha ukiulizwa mwaka 2055 utakua na umri gani huna haja ya kufikiri sana.

Back to the topic. Marley huwezi mfananisha na Dube.
Sio muasisi alikuja akaimba akatuburudisha na akaenda. Ni mwanamuziki mzuri tena nyimbo zake wakati wa ubaguzi zilikua kali sana.
 
Haujasikiliza nyimbo zakw vema. Huyo Lucky Dube alikuwa na tungo tata enzi za Apartheid hapo South Africa wakati kaburu akiwatesa watu weusi.

Labda utafute nyimbo zake usikilize vizuri neno kwa neno
 
Nenda nao taratibu akili zitakuwa sawa kadri wanavyokua.
 
Lucky Dube hafanyi Reggae,..kama ana nyimbo za mahadhi hayo basi hazizidi Tano,nikumbushe
Kumbe anaimba nini mzee bolingo? [emoji848]

Lucky Dube amekuja na reggae yenye vionjo vya tofauti na reggae ya kawaida yaani South African flavor. Reggae ya Lucky Dube inavionjo vya vinanda vya kwaya, waimbaji wa kwaya, na uimbaji wake ni phenomenal ni kama anahadithia kwa masikitiko au anatoa taarifa hivi kitu ambacho kipo sana kwenye reggae.
 
No woman no cry, stir up, redemption song etc, ukipata nyimbo ya dube ya reggae inaingia hapo kwa ubora, basi tutaanza kumfikiria dube.

Lucky dube ana ngoma kadhaa hivi ukisikiliza beats zake zinafanana na hata melody zake hazipo mbaaali saana, dube alijitahidi ila hakuwa bora kwangu, ila sio wa kuacha kuzungumziwa kabisa, hapo hata mie nashangaa kwanini hatajwi tajwi sababu ngoma zake zilibamba, sijui huko duniani ila kwa afrika alibamba, kama hakubamba huko duniani basi hio ndio sababu kuu.
 
Prisoner alipiga akimaanisha wapambanaji waliokamatwa na kufungwa jela yaani Dube hakuwa mpambanaji aisee sema Wazulu wanambagua Dube kwa kuwa ni Mzimbabwe..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…