Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,307
- 25,932
Nayazungumzia mabasi ya mikoani yanayoanzia Dar es Salaam kupitia barabara ya Morogoro au ile ya Bagamoyo. Yamekuwa na kawaida ya kuingia na kutoka kwenye kila stendi ya mabasi waikutayo ikiwa hata kama hakuna abiria anayeshuka au kupanda. Kiukweli, kuingia na kutoka kwenye stendi hizi (kwa mabasi ya mikoa ya mbali), husababisha muda kuisha na kuchelewesha abiria kufika waendako.
Kwa mfano, mabasi yaendayo Songea hufika Stendi Kuu iliyopo Shuleyatanga kuanzia saa tatu usiku hadi saa tano usiku badala ya saa moja au mbili usiku kutokana na ingia-toka hiyo niliyoizungumzia. Basi hilo huingia na kutoka Mailimoja/Kibaha, Chalinze, Msamvu/Moro, Ilembula/Iringa, Makambako/Njombe na Njombe Stendi Kuu kabla ya kufika. Yapo mabasi yanayoingia na kutoka kwenye stendi nyingi zaidi ya hizo.
Kwanini hasa mabasi haya ya mikoani 'yalazimishwe' kuingia na kutoka kwenye kila stendi ya mabasi hata kama hayana hitaji la kufanya hivyo?