Kwanini mabasi ya mikoani 'yalazimishwe' kuingia kila stendi?

Kwa nini walipishwe hayo mapato wakati hawakuwa na mtu anayeshuka au kupanda? Mfano unapanda SAULI ya Mbeya na imejaza siti zote, tena abiria wanashuka Mbeya, je ni kwa nini bus ilazimishwe kuingia stend za KIBAHA, Chalinze, Msamvu na nyinginezo??
Zile ni stand za halmashauri husika ni vyanzo vya mapato kwa halmashauri hizo
 
Tena zingine ni vichochoro na siyo stendi, mfano Hungumalwa na Busega kule Mwanza.
Kwa sababu huwezi kujua saa ngapi atakuja abiria was kwenda wapi,,lazima wananchi wawe na uhakika was kusafiri au lah gari zote zitakua haziingii stand wanapakia barabarani
 
Kwa nini walipishwe hayo mapato wakati hawakuwa na mtu anayeshuka au kupanda? Mfano unapanda SAULI ya Mbeya na imejaza siti zote, tena abiria wanashuka Mbeya, je ni kwa nini bus ilazimishwe kuingia stend za KIBAHA, Chalinze, Msamvu na nyinginezo??

Huyu mnyama kuna siku lazima nimpande. Naona ana hulka kama za kwangu za ubabe ubabe! Mara zote nikipita barabara ya Tanzam, lazima umkute ametangulia mbele ya wengine. Yaani hana muda wa kupoteza barabarani!

Napenda sana kujali muda. Sioni mantiki ya gari kutembea masaa 20! Na wakati lina uwezo wa kutumia masaa 12 tu. Umakini barabarani ndiyo kila kitu. Na nitakuwa wa mwisho kuamini kama mwendo kasi/ulio changamka ndiyo chanzo kikuu cha ajali.
 
Kwa sababu huwezi kujua saa ngapi atakuja abiria was kwenda wapi,,lazima wananchi wawe na uhakika was kusafiri au lah gari zote zitakua haziingii stand wanapakia barabarani
Gari za mikoa nauli zake fixed na hawafanyi kama daladala kusimama kila mara na kupakia wanavituo maalum vya kuchukua abiria vikiisha hizo stand wanapitia kutimiza wajibu tu
 
Waweke mabasi express. Yalipe tozo zote za hizo stand, maana ndiyo sababu kubwa. Basi itoke Dar stand ya kwanza Dom. Isimame tu kuchimbisha dawa.
 
Hoja za msingi.
 
Kwakweli inakera! Unatoka mbeya,iringa unaenda Arusha kupitia Dodoma kwa mfano,basi lazima lipite stand jmn ile ya naneane barabara ya kutokea dar,jmn kwnn? Yaani mzunguko usio na maana kabisa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zile ni stand za halmashauri husika ni vyanzo vya mapato kwa halmashauri hizo
Hakuna anayepinga Halmashauri kukusanya mapato, tunachosema yawe mapato halali kwa huduma yenye uhalisia.. Kumbuka hizi stendi na mabarabara yanajengwa kwa kodi pia tunazolipa
 
Msanii yale mawazo yetu sasa 🤣🤣

Wanaopinga wana hoja na tunaoona umuhimu wa stand tuna hoja.

Nchi ngumu hii

Mazingira haya yanataka katiba mpya. Kila kundi liweze kujihakikishia maslahi yake yanalindwa. Matokeo yake ni kuwa na serikali yenye kuwajibika kwa watu.
 
Zile ni stand za halmashauri husika ni vyanzo vya mapato kwa halmashauri hizo
... stendi za halmashauri focus iwe kuhudumia magari yanayotoa huduma ndani ya halmashauri husika na sio kulazimisha long safari's kuingia ili wakusanye mapato? Nchi hii tunapenda sana kuvuna bila kupanda!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…