Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 3,809
- 6,948
Kutokana na hizi changamoto ambazo zinazidi kuwa kubwa za usafirishaji wa abiria kwa njia ya mwendokasi, nimewaza ni kwa nini wenye mabasi ya coaster ya private (yale yasiyo na rangi maalumu za ruti), yasichukue hizi fursa za kusafirisha abiria hawa?
Maana yangu ni kwamba, chukulia wewe una coaster lako. Unatafuta abiria 40 wanaoishi Kimara au Mbezi. Unakubaliana nao, kila siku asubuhi saa 12:30 unawachukua eneo fulani. Na kila siku jioni saa 12:30 unawarudisha kutokea Gerezani/Kivukoni hadi Mbezi/Kimara. Hii ni kwa ruti moja.
Unaweza kuchukua abiria zaidi kwa makadirio ya muda tofauti kwa hiyo unaenda hadi mwisho, unashusha, unawarudia wengine.
Unatumia barabara za kawaida ila bila kusimama katika vituo vya daladala. Unaweza kutaka kulipwa kwa wiki. Nauli inaweza kuwa sawa na ile ya mwendokasi au hata juu kidogo.
Naamini sheria ya leseni ya mabasi ya private inawaruhusu kufanya hivi maana bado ni "private hire" na hawafanyi kama daladala.