Kwanini mafunzo ya mgambo yasiwe "compulsory" kwa wanafunzi wote waliohitimu kidato cha sita ambao hawakubahatika kuchaguliwa kujiunga na mafunzo JKT?

We jamaa una maisha ya kimasikini sana.

Yani badala ya kuhamasisha vijana wajifunze hata ku-code au wajifunze soft skills za kuwafanya wa-cope na utandawazi unaleta hadithi za kufagia uwanja.

Dunia ya sasa haihitaji migambo wala wafagia uwanja. Inahitaji watu smart vichwani.
 
Umemaliza kila kitu mkuu,kila mwenye akili kubwa hapa atakuwa amekuelewa.
 
Kumpeleka mtoto JKT ni kumwandaa kuwa fukara maisha yake yote ,kwasababu

1.Hatakuwa na akili za ubunifu tena zaidi ya kusubiri command tu
2.Unaanda watu ambao hawana mawazo mbadala zaidi ya kutumia nguvu tuu
3.Litakuwa liCcm la kudumu

Hio number 3 umeweka kwa kusisitiza litakuwa liCcm la kudumu 🤣🤣🤣
 
Israel bado inathamini mafunzo ya ukakamavu sio kwa ajili ya kuwafanya vijana waweze kujitegema ni kwa sababu ya vita zake na majirani zake wakati ikiwa na raia wachache hivyo inahitaji jeshi la akiba la uhakika kwa muda wote.
 
Nchi nyingine yenye mambo kama hayo ni Eritrea,Korea ya Kaskazini na Kusini ila nchi nyingi zilizoendelea hazina hayo mambo.
 
Hili wazo lake la kijima sana
 
Mkuu dunia inaenda mbio sana huku sisi tunatembea wenzetu wakombio. Achana na fikra kuwa mekanika lazima awe na mwili kama Mwarabu fighter. Hizo skills hata watoto wa sekondari wakipewa wanafanya haiitaji kuwa na miili au ukakamavu.

Kwenye rangi siku hizi tunatumia gun spray haihitaji mtu mrefu, mekanika nayo haihitaji nguvu nyingi sasa kuna mashine kibao za kurahisisha kazi stadi za nati ya roli hata binti wa miaka 16 anaweza akafungua kwa kutumia mashine,kuna winch, pressing mashine na vifaa kibao na sasa ni zama za electric kila mahali.

Hapa tupindue meza ile stadi za kazi ya shule za msingi baada ya kufundisha watoto kushona vitambaa na mkeka wafindishwe hata kufungua kompyuta,pikipiki, bodaboda, baiskeli na vifaa ambavyo katika Maisha ya kila siku watatumia au kukutana navyo.
 
Kwa msisitizo tu ni kwamba kijana yoyote ambae ni raia wa kuzaliwa ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ambae amemaliza kidato cha sita anapaswa kujiunga JKT kwa mujibu wa sheria.

Hiyo haijalishi umemaliza Mzizima, Al Haramain au Feza boys au Girls.

Iwe ni kwa mujibu kwa sheria ya JMT.

Na hata iwe kwa sababu mbalimbali kijana huyo hakuweza kujiunga huo basi iwe ni deni na atumukie kwa muda utakaofaa.

Nchi kama Israeli, Korea Kusini, Kazakhstan na zingine wanafanya hivyo.

Hii yaondoa matatizo kama kutokuwa mzalendo, uzembe wa kufikiri na ushawishi wa kujiunga na makundi kama yale ya kule Kibiti.

Enzi zetu sisi kaka na dada zenu tulikuwa tukikutana pamoja JKT na bila kujali tajiri au maskini au mtoto wa mkulima wote tulinyoa nywele na kuwa na madenge sawa.

JKT ndipo ndipo misingi ya umoja, amani na upendo baina ya wana wa nchi inapojengwa.

Wengine wanaobadilika kama tunaowaona leo hii na wamepitia JKT ni kwa kudanganywa na vijienti vya hapa na pale.
 
Uongo
 
Naunga mkono hoja.
Dunia ya sasa haiendeshwi kwa njia primitive kama zamani.
Achilia mbali mitaani hata hao maaskari wa nchi za wenzetu vitani hawapigani kwa kutumia miguvu kama zamani ni akili tu na teknolojia.
Mtu yupo Korea analipua marekani
Physical presence katika Vita bado itaendelea kuhitajika. Ni kweli waweza kuilipua Montana ukiwa Tarime, Mannheim, au Bergamo na kinyume chake. Lakini huwezi kuteka nchi kwa kutumia makombora ya masafa marefu, drones nk. Hivyo infantry soldiers wana umuhimu mkubwa na ndio huteka au hukomboa nchi. Bottom line is Kila Askari regardless uko jeshi gani ukakamavu Ni lazima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…