Kwanini mafunzo ya mgambo yasiwe "compulsory" kwa wanafunzi wote waliohitimu kidato cha sita ambao hawakubahatika kuchaguliwa kujiunga na mafunzo JKT?

Nadhani FETA Mbegani wanatoa haya mafunzo
 
Nadhani FETA Mbegani wanatoa haya mafunzo
FETA iwe Mbegani au Nyegezi wao hutoa mafunzo ya uvuvi kuanzia ngazi ya cheti.

Nazungumzia kuhusu kutolewa short course za hivyo vitu. Maana ukiangalia syllabus ya FETA wao wana Kozi ya Master Fisherman, Marine engineering ila ndani kuna module wanafundisha diesel engine na kurekebisha injini za boti ila tambua mtu anayetoka hapo outboard engine kasoma nadharia.
 
Huko jkt kuna pesa au ndio mlango wa ajira?!

Nchi hii hakuna HAKI na hilo ndilo tatizo kubwa, sio kutokwenda JKT.
Unampeleka mtu JKT akitoka huko hana kazi miaka 10 yuko mtaani, halafu unataka awe mzalendo, sawa hatuhamasishi ujambazi, wala uasi.

Tuambie kijana kasoma kamaliza chuo ana dgree moja, hana ajira, ana deni la mkopo, ana ndoto za maisha anayotaka yeye, hiyo JKT inamsaidia nini?! Au inamsaidiaje aishi?!

Mnataka akalime sijui, mara ajiajiri huo ni upuuzi tu, frustration zinataka solution siyo panadol.
 
Barikiwa
 
Huko jkt kuna pesa au ndio mlango wa ajira?!
Nchi hii hakuna HAKI na hilo ndilo tatizo kubwa, sio kutokwenda JKT.
Mkuu, usilazimishe ideologies zako ndio ziwe imani ya kila mtu. Wewe unaona nchi hii hakuna haki ila wapo wanaona haki ipo na inatendeka...
 
Mgambo iwe compulsory? Vijana wetu wakasote kuwa jeshi la akiba?
 
Hakuna kubahatika kuingia jkt kwa aliemaliza f6. Kubahatika ni kupata ulichokihitaji sana bila kutarajia. Ni wachache waitwao kwa mujibu na kwenda kwa furaha. Wanakwenda tu kwa kuwa ni sheria.
 
Mfumo wa ufundishaji ulioushauri una walakini. Hao wauza magari wanaokuja kutoa mafunzo wamethibitishwa na nani? Mwisho wa masomo yoyote uthibitisho ni cheti cha kuhitimu, kitatolewa na nani? Kuna VETA ndio watoa mafunzo kwa level za chini, washauri vijana waende huko.
 
Mkuu, usilazimishe ideologies zako ndio ziwe imani ya kila mtu. Wewe unaona nchi hii hakuna haki ila wapo wanaona haki ipo na inatendeka...
Hahaha hivyo nikubali ideology zako za kupeleka watu jkt na mgambo?!

Mawazo yangu ni yangu na yako ni yako.
Huyapendi yangu yaache, nami nisipopenda yako Natayaacha.

Jukwaa huru hili.

Usisahau kumpigia kura Tundu Lisu na CHADEMA kwa Haki, Usawa, Amani na maendeleo ya Tanzania.
 
Mhhh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…