Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Magari ya Nissan hayana shida...Mafundi ndiyo wenye shida hawataki kuumiza vichwa na kujifunza mifumo mipya..Habari wadau,hivi ni kwanini magari aina ya Nissan matengenezo na marekebisho yake yanasumbua mafundi wengi?pia ni gharama kubwa kurekebisha ukilinganisha na Toyota
Hapana mifumo haibadiliki sana, ila ukiangalia magari ya toyota yaliyokuwa yanaingia nchini miaka ya nyuma, yalikuwa hayana mifumo mingi ya umeme kama Magari Nissana. Kwa mfano Injini ya Rav 4 Masawe ile 3s, haina sensors nyingi kama injini ya Xtrail...Tokea yametengenezwa ina maana yanabadilika mifumo kila kukicha
Kwa upande fulani hii hoja ina mashiko...Spare za nissan ni bei lakini wanaofanya ziwe bei ni hao hao wauza spare. Ukiwatajia tu nissan kosa kubwa. Fungua kifaa kilichoharibika nenda nacho ukawaambie naomba spare kama hii. Bei haitakuwa kubwa
Bongo mafundi wengi wavivuBongo fundi akiwa mbovu huwa anasingizia kuwa gari fulani ni bovu na hazifai bongo!😁😁😁
Siyo wavivu mkuu,imagine mtu ameishia darasa la saba halafu hajawahi kwenda VETA wala chuo chochote kile cha ufundi ni amejifunzia tu garage za mitaani huko halafu anakuja kukutana na magari ya siku hizi ambayo ni computerized, mambo ya decoding of codes!😁😁😁Bongo mafundi wengi wavivu
NgumbaruSiyo wavivu mkuu,imagine mtu ameishia darasa la saba halafu hajawahi kwenda VETA wala chuo chochote kile cha ufundi ni amejifunzia tu garage za mitaani huko halafu anakuja kukutana na magari ya siku hizi ambayo ni computerized, mambo ya decoding of codes!😁😁😁
X-trail Gari ya wanyongeHata siwaelewi kitu gani fundi anaweza kushindwa kutengeneza kwenye hizo Nissan zilizopo mnazosema ni mpya...Maana Nissan nyingi ni ngumu kidogo au ninyi ndio mnachelewa kutengeneza gari ikihitaji matengenezo haraka maana gari huwa inaongea inapokua na tatizo kwa mtu wa magari hata Kama sio fundi utajua unaanzia wapi...
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]Shida mafundi wetu wanapiga ramli, gari ni kama binadamu laziza diagnosis ifanyike. Unaweza kununulishwa vifaa na gari isipone
Ipo ya 2015 na 2018 sio ya wanyonge hiyo Mkuu sema iliyopo hapa ni hii...hiyo ya 2018 ni ya kibabe kidogo...X-trail Gari ya wanyonge
nikushauri, kama hiyo gari ni la petroli, na ni automatic, na unalitumia mkoa wenye joto la wastani, achana na thermostat. maana with or without thermostat joto litapanda tu hadi kufikia optimum (magari mengi naona temp. gauge huwa ni katikati ya cool na hot). muhimu hakikisha coolant ipo.Mafundi wetu bado saana..
Juzi mwezi Februari gari lilileta shida..
Radiator fan ilikuwa ikifunguka, haizimi na inazunguka kwa kasi isiyo ya kawaida..
Injini ikawa inapandisha joto..
Nikafanya diagnosis hapakuonekana code yoyote..
Wapiga ramli hao wakasema swichi ya fan ya radiator ndiyo imekufa...Wakaja mafundi kama watatu wakasema swichi imekufa hivyo ikihisi joto la injini inafungua fan na inashindwa kuzima..
Niakanunua Swichi nyingine, tatizo likawa pale pale...
Nikawaambia huenda thermostat imekufa, wabisha sana wakasema havina uhusiano..
Nikarudi home, nikawasha gari tena nikaacha lipate moto, fan ikawaka, nikashika hose inayotoa maji kwenye inji kuja kweny radiator, ilikuwa ya moto sana kiasi cha kutokushikika..
Hose ya chini inayotoa maji kwenye radiator kwenda kwenye injini ni ya baridi kabisa...Kati ya hose ya chini na injini, ndipo thermostat ya gari langu ilipo....Nikagundua thermostat imekufa kwa mtindo unaoitwa Stuck closed...hivyo maji ya radiaotor hayaingii kwenye injini..
Yale yaliyopo kwenye injini yanachemka sana na ile swichi (sensor) ya kufanya fan iwake , ikawa haizimi kwa sababu maji ya ndani ya inji hayapungu joto.
Nikatoa thermalsta mwenyewe, nikaitest kwa kuichensha jikoni, inafunguka kwa shida sana na kuwa wakati haifunguki..
Baada ya kuitoa tatizo likaisha, joto la injini likipanda fan inawaka na likishuka inazima kama kawaida.
Kwa sasa nataka ninunue thermostat mpya niweke.
Mafundi wetu hawa, mmh...
Binafsi nimeamua kuwa fundi wa gari langu mwenyewe...
Mafundi huwa nawapelekea zile sehemu za kimakanika zaidi, mfano bearing, shockup nk