Lakini walioweka thermostat walifanya research ya kutosha. Ndiyo maana hata magari yatokayo UAE, pamoja na joto la kule, bado yanakuwa na thermostat.
Nina uzoefu wa kuondoa thermostat, na simshauri mmiliki wa gari kutoa. Miaka kama kumi iliyopita nilipata breakdown ya gari, tena Toyota nikiwa Ruvu darajani, fan clutch ilikufa, na gari ikaanza kuchemsha. Nikaiendesha mdogomdogo mpata chalinze. Pale hawa mafundi wetu wakaibana fan, lakini wakanishawishi niitoe thermostat wakidai huku kwetu haina haja ya kuwemo kwenye engine.
Kwa shingo upande, nikakubali kuitoa thermostat lakini sikuwaachia. Nikaanza tena safari kuelekea Mbeya, ila sikufika Iringa. Kila nilipotaka kukanyagia, temperature ilipanda. Nikapumzika comfort motel (enzi zile), baada ya engine kupoa, nikapanda kitonga kwa shida mpaka Iringa.
Pale Iringa nikatafuta Fundi akarudishia thermostat yangu, nikaanza tena safari kwenda Mbeya. Nikakanyagia mashine kwa hasira, haikupandisha temperature kabisa na gari nipo nayo mpaka leo na thermostat sijaitoa.
Kwa uzoefu huu, Mimi simshauri mtu yeyote kuondoa thermostat kwenye engine ya gari yake, labda iwe imekufa, lakini ikifa pia, mpya zipo, una replace tu.