Mafundi wetu bado saana..
Juzi mwezi Februari gari lilileta shida..
Radiator fan ilikuwa ikifunguka, haizimi na inazunguka kwa kasi isiyo ya kawaida..
Injini ikawa inapandisha joto..
Nikafanya diagnosis hapakuonekana code yoyote..
Wapiga ramli hao wakasema swichi ya fan ya radiator ndiyo imekufa...Wakaja mafundi kama watatu wakasema swichi imekufa hivyo ikihisi joto la injini inafungua fan na inashindwa kuzima..
Niakanunua Swichi nyingine, tatizo likawa pale pale...
Nikawaambia huenda thermostat imekufa, wabisha sana wakasema havina uhusiano..
Nikarudi home, nikawasha gari tena nikaacha lipate moto, fan ikawaka, nikashika hose inayotoa maji kwenye inji kuja kweny radiator, ilikuwa ya moto sana kiasi cha kutokushikika..
Hose ya chini inayotoa maji kwenye radiator kwenda kwenye injini ni ya baridi kabisa...Kati ya hose ya chini na injini, ndipo thermostat ya gari langu ilipo....Nikagundua thermostat imekufa kwa mtindo unaoitwa Stuck closed...hivyo maji ya radiaotor hayaingii kwenye injini..
Yale yaliyopo kwenye injini yanachemka sana na ile swichi (sensor) ya kufanya fan iwake , ikawa haizimi kwa sababu maji ya ndani ya inji hayapungu joto.
Nikatoa thermalsta mwenyewe, nikaitest kwa kuichensha jikoni, inafunguka kwa shida sana na kuwa wakati haifunguki..
Baada ya kuitoa tatizo likaisha, joto la injini likipanda fan inawaka na likishuka inazima kama kawaida.
Kwa sasa nataka ninunue thermostat mpya niweke.
Mafundi wetu hawa, mmh...
Binafsi nimeamua kuwa fundi wa gari langu mwenyewe...
Mafundi huwa nawapelekea zile sehemu za kimakanika zaidi, mfano bearing, shockup nk