Kwanini magari aina ya Nissan yanasumbua mafundi kwenye matengenezo?

Kwanini magari aina ya Nissan yanasumbua mafundi kwenye matengenezo?

Nashukuru sana kwa ushauri mkuu

Binafsi nitapenda kuirudishia ila lazima iwe genuine...
Japo sina haraka sana..

Itoshe tu kusema "Nissan all the way."[emoji3][emoji119][emoji119][emoji3]
Natafuta fundi mzuri wa Nissan, nina Nissan Cube, 2007, gear hazichenji, reverse poa, kwenda mbele poa, ila gear hazibadiliki, ni kama naenda na gia namba moja tu, na pia wakati wa kuweka gia, gari inakuwa kama inastuka hivi, saidieni ushauri wote tafadhali...
 
Unapokuwa na gari ambayo parts zake ni expensive then usidundulize matatizo. Umesikia inagonga haraka shughulikia tatizo.

Kawaida ya wabongo gari itagonga miguu anauchuna, hadi ianze kuashia na taa za check engine ndio aende gereji. Akifika huko wanamletea msululu wa matatizo kuyatibu inakuwa gharama anaanza oooh toyota sijui nafuu.

Sio kweli. Wewe pay attention na gari yako. Hakikisha unaihudumia on the spot inapokohoa au kupiga chafya. Yaani usilale na tatizo zaidi ya wiki.
True
 
Hebu acha uongo. Hakuna kifaa unakiona kwenye gari kisiwe na kazi yake na ukakitoa gari ikawa haina mushkeli katika kuitumia.

Wewe sema haujui kazi ya kitu ulichotoa sio useme hakina kazi.
umeamua tu kubisha kimhemko. kwa sisi serious offroaders makorokoro kibao yanaondolewa (mfano, ukifanya SAS). parts zinazokuja na gari haziwezi himili mikiki, hivyo kuondoa uwezekano wa kulala porini unaiondoa moja kwa moja. na gari haiwi na "mushkeli". yaani ndo performance yake inaongezeka.
 
Natafuta fundi mzuri wa Nissan, nina Nissan Cube, 2007, gear hazichenji, reverse poa, kwenda mbele poa, ila gear hazibadiliki, ni kama naenda na gia namba moja tu, na pia wakati wa kuweka gia, gari inakuwa kama inastuka hivi, saidieni ushauri wote tafadhali...
Vipi umewahi kubadili oil ya gear box..?
Kama ndiyo, uliweka oil ya aina gani..? tuanzie hapo kwanza
 
Mafundi wetu bado saana..
Juzi mwezi Februari gari lilileta shida..
Radiator fan ilikuwa ikifunguka, haizimi na inazunguka kwa kasi isiyo ya kawaida..
Injini ikawa inapandisha joto..

Nikafanya diagnosis hapakuonekana code yoyote..

Wapiga ramli hao wakasema swichi ya fan ya radiator ndiyo imekufa...Wakaja mafundi kama watatu wakasema swichi imekufa hivyo ikihisi joto la injini inafungua fan na inashindwa kuzima..

Niakanunua Swichi nyingine, tatizo likawa pale pale...
Nikawaambia huenda thermostat imekufa, wabisha sana wakasema havina uhusiano..

Nikarudi home, nikawasha gari tena nikaacha lipate moto, fan ikawaka, nikashika hose inayotoa maji kwenye inji kuja kweny radiator, ilikuwa ya moto sana kiasi cha kutokushikika..

Hose ya chini inayotoa maji kwenye radiator kwenda kwenye injini ni ya baridi kabisa...Kati ya hose ya chini na injini, ndipo thermostat ya gari langu ilipo....Nikagundua thermostat imekufa kwa mtindo unaoitwa Stuck closed...hivyo maji ya radiaotor hayaingii kwenye injini..

Yale yaliyopo kwenye injini yanachemka sana na ile swichi (sensor) ya kufanya fan iwake , ikawa haizimi kwa sababu maji ya ndani ya inji hayapungu joto.

Nikatoa thermalsta mwenyewe, nikaitest kwa kuichensha jikoni, inafunguka kwa shida sana na kuwa wakati haifunguki..

Baada ya kuitoa tatizo likaisha, joto la injini likipanda fan inawaka na likishuka inazima kama kawaida.

Kwa sasa nataka ninunue thermostat mpya niweke.

Mafundi wetu hawa, mmh...

Binafsi nimeamua kuwa fundi wa gari langu mwenyewe...
Mafundi huwa nawapelekea zile sehemu za kimakanika zaidi, mfano bearing, shockup nk
Hapo mkuu nakushauri nenda veta kapige short course ya Auto electrical,mechanical utakuwa fundi mzuri na pia utakuwa na ujuzi utakaokunufaisha uko baadae
 
Hii hapa imeungua leo.
Screenshot_20210806-211857_Instagram.jpg
 
Bora tu niseme nasumbuliwa na Suzuki fundi aliigusa injection kumbe tatizo ilikuwa plug zile niliweka haziendani from there rpm inakuwa inaelekea 0 , missing etc fundi mzuri wapi
 
Nitakupa mfano kuna nissan ya bi dada m'moja ilikuwa imewasha taa ya ABS. Shida ilikuwa mguu wa upande wa dereva mbele.

Wakafanya wheels alignment, taa bado, wakafungua ile kitu inashika break pads, taa bado, akafumua miguu na kuicheki wapi.

Dada akanunulishwa vifaa hata ambavyo havina shida patupu taa bado. Fundi akataka kudisable mfumo wa sensor sasa kama bahati, mimi nikakutana nae bi dada before zoezi hakijafanyika.

Nikamuuliza uliifanyia gari yako diagnosis kabla ya yote haya, akasema hapana. Ikabidi nimpatie namba ya kijana ambaye anafanya hizo vitu.

Akaenda wakakuta issue ilitakiwa tu kureset taarifa na changamoto ilikuwa ni rotation ya tairi zilikuwa zinapishana so sensor ilisoma na kutoa taarifa.

Ila gari ilirekebishwa na mfumo kuwa reset.
Habari. Naomba namba za mtu anayefanya diagnosis ya nissan boss. Mimi 0717575635
 
Bora tu niseme nasumbuliwa na Suzuki fundi aliigusa injection kumbe tatizo ilikuwa plug zile niliweka haziendani from there rpm inakuwa inaelekea 0 , missing etc fundi mzuri wapi
Mcheki jamaa yuko Mwenge 0717595019
 
Natafuta fundi mzuri wa Nissan, nina Nissan Cube, 2007, gear hazichenji, reverse poa, kwenda mbele poa, ila gear hazibadiliki, ni kama naenda na gia namba moja tu, na pia wakati wa kuweka gia, gari inakuwa kama inastuka hivi, saidieni ushauri wote tafadhali...
Gear box oil
Gear box mounting
 
Wachache ina maana wapo Isanga. Inawezekana si wewe au mtu unayemfahamu.

Achilia mbali nissan xtrail Ndani ya nchi yako Tanzania kuna wakulima wananunua tractor mpya.
Mkuu unachombishia kiongozi Isanga family sidhani Kama uko serious. Gari za 2017 and above tunatafutana. Ingawa kiukweli hakuna asiyependa gari mpya. Ni uchumi tuu unabana.

Ukute mtu kashusha machine ya 2020 AU 2021? Wapo ila ni wa kutafuta kwa tochi. Tena tochi yenye mwanga wa kutosha haswa!
 
Duuu, hii mada ni ya muda hata sikumbuki msingi wa hoja labda niangalie historia, anyways Hatubishani ndugu Masanja, tunapeana challange tu kulingana na uzoefu wa maisha....
 
Back
Top Bottom