Kwanini magari aina ya Nissan yanasumbua mafundi kwenye matengenezo?

Nakazia mkuu, Gari huwa inaongea haswaa, so ni kazi kwako kusikiliza na kuijali...

Yaani unakuta mtu anasikia kuna abnormal sound halafu anaipotezea kumbe hapo hajui kuwa anazidi kuharibu parts za chuma yake...
 
Umeandika points ila Happ mwishoni umeandika Kama Katibu Mwenezi. Toyota Gari ya kimaskini, wajanja wamehamia Ford
 
Mfano wa fundi wa chini ya miti/std 7 ndio kama huyu sasa.
 
Heh!! Thermostat ina kazi zake nyingi tu, endapo akiitoa lazima kutakuwa na changes kwenye ulaji wa mafuta.
 

Msukuma, kibajaji na wale wenzao wakulungwa mkono na mhe. supika watakupinga kwa nguvu zao zote.
 
Mfano wa fundi wa chini ya miti/std 7 ndio kama huyu sasa.
Kuna garage moja huku kijijini kwetu, gari ikija tu wanamsahuri mwenye atoe thermostat, yakwamba zilitengenezwa special kwa nchi zenye baridi tu... [emoji3][emoji3]

Na kuna ule ujinga wa kuunga direct fan, yaani ukiwasha tu ngoma inaanza kupiga kazi et ni njia bora ya kuzuia engine isichemke... [emoji3]

Walimfungia maza mmoja hiyo kitu, motor ya fani ikawa ni kuungua tu akibadili tu, kinachofuata ni fan kukata blade zake....

Ufundi nyudo kazi kweli kweli...
 
Nakazia mkuu, Gari huwa inaongea haswaa, so ni kazi kwako kusikiliza na kuijali...

Yaani unakuta mtu anasikia kuna abnormal sound halafu anaipotezea kumbe hapo hajui kuwa anazidi kuharibu parts za chuma yake...
Yap upo sahihi kabisa Mkuu ni wachache wanajua code za gari ikishaongea mimi watu wangu wa karibu nilipokua nawaambia hivi walikua hawanielewi kabisa sasa nao wamejua lugha ya gari tunaenda sawa...na pia kununua magari yaliofunguliwa funguliwa mwanzo utashindwa kwenda nayo sawa...
 
Nashukuru sana kwa ushauri mkuu

Binafsi nitapenda kuirudishia ila lazima iwe genuine...
Japo sina haraka sana..

Itoshe tu kusema "Nissan all the way."[emoji3][emoji119][emoji119][emoji3]
 
unamuingiza chaka mwenzio , thermostat sio ya kuitoa hata kama unaishi jangwani
 
Kagari kangu nilipokatoa tu bandarini mwaka huooo,jamaa akaja akaniambia Mwaga oil uwekeSAE 40 ndiyo za nchi za joto..

Mwingine akaniambia inabidi uunge fan direct kwa sababu huku kuna joto kuliko Japan..[emoji3][emoji3]

Tz jamani... [emoji119][emoji119][emoji119][emoji119]
 
Some car owners complain about poor noise insulation, soft metal of the body, the presence of a large number of electronics, which makes car repair and maintenance far from cheap.

hiyo ni article kutoka page ya japanese car market mafundi wanahaja yakusoma na sio kutegemea ujuzi wa garage tu.
 
Habari wadau,hivi ni kwanini magari aina ya Nissan matengenezo na marekebisho yake yanasumbua mafundi wengi?pia ni gharama kubwa kurekebisha ukilinganisha na Toyota
mafundi wengi hawazipatii nazani, maana nna ndugu yangu ana xtrail huu mwaka wa sita na haijawah msumbua, ila ndugu mwingine kataka kununua xtrail juzi juzi fundi kampiga mkwara ooh "hizo hazifai zinasumbua sana ndo maana watu wanaziuza bei rahisi" hadi jamaa kaogopa
 
Heh!! Thermostat ina kazi zake nyingi tu, endapo akiitoa lazima kutakuwa na changes kwenye ulaji wa mafuta.
ni kweli ina kazi nyingi, ila kwa utashi wangu naona kama kitu kikikosekana na maisha yanaenda basi hicho kitu sio lazima kiwepo.

kwenye ulaji wa mafuta sijaona tofauti kwangu.
 
Habari wadau,hivi ni kwanini magari aina ya Nissan matengenezo na marekebisho yake yanasumbua mafundi wengi?pia ni gharama kubwa kurekebisha ukilinganisha na Toyota
Mafundi wengi ni wa zamani hiv.Nisani nyingi zina umeme zaidi,so mafundi wale wenye miguvuguvu tu na siyo akili ukiwapelekea Nisan waniua kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…