Johnny Sack
JF-Expert Member
- Jan 21, 2017
- 8,984
- 19,288
Lipo wazi CCM wengi hawampendi Magufuli, ila wanajitahidi kutomshambulia moja kwa moja sababu alikuwa kiongozi wao waliomuunga mkono alipokuwa kiongozi, CHADEMA ndiyo hawampendi kabisa, ACT ndiyo kabisaa.
Wasomi wengi pia hawamkubali Magufuli, ukiwauliza tu ukiwa nao wengi wanamponda, baadhi walikuwa wakimsifia tu kipindi kile sababu ya woga au kutaka cheo ila wanyonge, kama alivyopenda kuwaita Watanzania wa kawaida, hili ndio kundi kubwa la watu na linamkubali sana, utaona comments zao Facebook na Instagram wakimfagilia, ila hutawaona sana Twitter na hapa JF, hawapendi sana hii mitandao.
Najiuliza ni kwa nini? Magufuli alikuwa akiwaeleza watu Tanzania ni tajiri, miradi mingi tunaifanya kwa fedha zetu, akawaeleza pia yeye siyo miongoni mwa kundi la elites ndani ya CCM walioifisadi nchi.
Pia alisikika akisema mtu katika utawala wa nyuma masikini aliweza kufanywa chochote na tajiri ila katika utawala wake tajiri anaweza kufanyiwa chochote, aliruhusu pia wafanyabishara ndogondogo kufanya biashara popote na kusema yeye ni mkombozi wao.
Alikuwa akiwafokea, kuwatukana na kuwafukuza maafisa wa Serikali waliokuwa wakilalamikiwa na wananchi mbele ya hadhara, na mara nyingi alisimama kusikiliza matatizo binafsi ya wananchi kama vile mirathi.
Haya na mengine mengi yaliwafurahisha sana watu wa tabaka la chini ambalo liliamini shida zao zinatokana na kuonewa na viongozi wa serikali na matajiri
Sasa kwa nini wasomi na wanasiasa wengi wasimpende? Kwa haraka haraka mtu ukitazama uongozi wa Magufuli utaona ni uongozi wa kuleta maendeleo na kuondoa rushwa, kuwapa haki wanyonge dhidi ya matajiri na mabwanyenye na kuipaisha nchi kiuchumi.
Mtu huwezi kusema unaondoa rushwa huku ukiua uwazi, unafunga na kuua wanaokosoa, ukifungia na kuvitisha vyombo vya habari, huwezi kusema utakuza uchumi na kipato cha watu huku unakandamiza sekta binafsi kwa kuvuruga biashara, huwezi kusema hubagui watu kwa vyama huku ukiwaambia mmechagua upinzani maendeleo siwapi, huwezi kusema upo against na mabwanyeye huku ukiwajengea mahekalu wastaafu, na kuteua watoto wao na wake zao kwenye vyeo vya kisiasa badala ya watu wa kawaida.
Huwezi kusema umerudisha nidhamu kwa watendaji wa serikali huku wateule wako wakiingia benki na kupora mchana kweupe, kuvamia vituo vya habari na walinzi wa ikulu, Polisi wakiua na kubambikiza watu kesi, watu wenye uelewa hawawezi kukuelewa kamwe.
Samia kwenye moja ya mahojiano yake, alisema anataka legacy yake iwe ni kuwafanya watanzania kujitambua hasa kwenye mambo ya siasa na uraia, nafikiri ameona watanzania wengi hawajui wana uelewa mdogo sana kwenye siasa na ni rahisi sana kuwalaghai.