Kwanini mahabusu hawasafirishwi kwa staha wanapopelekwa mahakamani?

Kwanini mahabusu hawasafirishwi kwa staha wanapopelekwa mahakamani?

Sexless

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2017
Posts
23,683
Reaction score
55,898
Sioni sababu ya kuwasafirisha mahabusu kwa namna inayofanyika hivi sasa. Mahabusu wanasafirishwa na magari ya polisi huku wakiwa wamechuchumaa.

Kwann lisitafutwe gari ama minibus zuri lenye AC wakaketi wote na kupewa magazeti wayasome wakati wakielekea mahakamani?

Hatuoni kuwa kama taifa tunafanya makosa yale yale wanayoshitakiwa mahabusu, (ya kuzikanyaga haki za wengine)?

Kwahiyo tumeamua kuwa taifa la kutafuta haki kwa kuzikanyqga haki za mahabusu?

Screenshot_20240905-224907_1.jpg

Screenshot_20240905-224945_1.jpg
Picha: Watuhumiwa wa ubakaji wakipandishwa kwenye gari la polisi
 
Sioni sababu ya kuwasafirisha mahabusu kwa namna inayofanyika hivi sasa. Mahabusu wanasafirishwa na magari ya polisi huku wakiwa wamechuchumaa.

Kwann lisitafutwe gari ama minibus zuri lenye AC wakaketi wote na kupewa magazeti wayasome wakati wakielekea mahakamani?

Hatuoni kuwa kama taifa tunafanya makosa yale yale wanayoshitakiwa mahabusu, (ya kuzikanyaga haki za wengine)?

Kwahiyo tumeamua kuwa taifa la kutafuta haki kwa kuzikanyqga haki za mahabusu ??

View attachment 3088487
View attachment 3088488Picha: Watuhumiwa wa ubakaji wakipandishwa kwenye gari la polisi

Ni kwa sababu hayupo wa kuwasemea.

Tumejawa ubinafsi tukidhani umahabusu hautuhusu.

Laiti tungalijua sote tu mahabusu watarajiwa.
 
Nadhani ni katika hali ya kuwadhibiti wasitoroke
Kuna watu wana kesi mbaya ukiamua kuwasafirisha kama watalii wakarudi mtaani hali itakuwa mbaya.
Wako chini ya ulinzi laZima wadhibitiwe.
Ukiwa mahabusu utafungwa pingu, kuchuchumaa n.k kikubwa tukutane na vyombo vya haki ndo vitaamua hatima yako
 
Wewe ungefurahi kama ukisafirishwa hivyo na uelewe mahabusu bado ajapewa hukumu hapo maana anaweza kutwa hana hatia.

Mimi nadhani serikali inatakiwa iboreshe magereza na hali ya hao askari wenyewe pia wakiboresha magerza na vifaa pia ikiwemo magari yatakuwa mazuri tu.
 
Ili wajutie mambo waliyoyafanya,hata wewe au mimi ikibainika nimefanya upuuzi fulani ni haki kupitia hicho wanachofanyiwa,
Au mkuu unadhani wameonewa ?
Sio kila mahabusu ana hatia. Hao sio wafungwa bado. Wakihukumiwa kwa haki, labda ndio wasitetewe. Lakini kwenye hali ya umahabusu, ni kuwa wanatuhumiwa tu. Hata wewe unaweza bambikizwa kesi, na kabla ya kuchomoka, utakuwa umepita hiyo hali ya umahabusu. Ni vizuri mahubusu waheshimiwe tu kama raia.
 
Sasa hapo wanasafirishwa! Ungeingia kwenye vyumba wanamo hifadhiwa, si ndiyo ungechoka kabisa! Mahubusu/jela ukiingia na afya yako mgogoro, unaweza kujikuta umekata moto.
Nilifanya kazi kwenye halmashaur moja Tanzania. Nilikuwa nafanya kazi za ukimwi. Palikiwq na gereza moja la wanaume. Kilichonishangaza robobtatu walikuwa wameathirika hili liliniumixa sana sikujua kwqnn mana sikuwa na room ya kuwahoji
 
Sio kila mahabusu ana hatia. Hao sio wafungwa bado. Wakihukumiwa kwa haki, labda ndio wasitetewe. Lakini kwenye hali ya umahabusu, ni kuwa wanatuhumiwa tu. Hata wewe unaweza bambikizwa kesi, na kabla ya kuchomoka, utakuwa umepita hiyo hali ya umahabusu. Ni vizuri mahubusu waheshimiwe tu kama raia.
Ndo Kwa kipindi yupo chini ya ulinzi hawezi kwenda mahakamani kama mtalii
laZima hayo yamkute
Wewe unataka askari ampe mtuhumiwa masifa na juisi ya baridi.
Kubali tu ukiwa Kwa mazingira ya umahabusu laZima hayo yakukute
 
Sexless uko bar gani muda huu?
Hebu rudia Tena hapo kwenye minibus yenye AC na kupewa magazeti.
Hivi watu hua mnawaza Nini? Vituo vya polisi havina ac halafu watuhumiwa wasafirishwe kwenye gari lenye AC.
Nilitaka tu kuweka msisitizo kwamba mahabusu wasisafirishwe kama wanyama. Kuwepo na utu kiasi.
 
Back
Top Bottom