Kwanini mahabusu hawasafirishwi kwa staha wanapopelekwa mahakamani?

Kwanini mahabusu hawasafirishwi kwa staha wanapopelekwa mahakamani?

Kiufupi hayo mambo yalianzishwa makusudi ili kudhibiti uhalifu kwa kuwajengea hofu raia, hakuna anayependa kufikia hali hiyo. Ndio maana unapaswa kutii sheria na mamlaka za nchi kwa kuwa raia mwema.
 
Mbona kawaida tu wao wamefanya mambo ya hovyo,wafanyiwe kulingana na uovu wao sasa wabakaji wawekwe kwenye gari zuri lenye ac mbona watakuwa wanajikubali sana na hawatajutia ujinga wao
Weka akiba ya maneno ndugu yangu. Ikiwa uko hai usimalize maneno yote. Sio kila unaemuona kwenye defender au karandinga ni muhalifu. Dunia ina mengi.

Kubwa ni kumuomba Mungu wako akulinde usifike huko ila sio kudhihaki mahabusu wa leo ikiwa hata wewe unaweza kuwa mahabusu kesho, tena bila hatia.
 
Mbona kawaida tu wao wamefanya mambo ya hovyo,wafanyiwe kulingana na uovu wao sasa wabakaji wawekwe kwenye gari zuri lenye ac mbona watakuwa wanajikubali sana na hawatajutia ujinga wao
Eti wapewe na magazeti ya kusoma.
 
Weka akiba ya maneno ndugu yangu. Ikiwa uko hai usimalize maneno yote. Sio kila unaemuona kwenye defender au karandinga ni muhalifu. Dunia ina mengi.

Kubwa ni kumuomba Mungu wako akulinde usifike huko ila sio kudhihaki mahabusu wa leo ikiwa hata wewe unaweza kuwa mahabusu kesho, tena bila hatia.
Achana naye mkuu, yeye anajua yupo salama!
 
Tatizo la nchi zetu hizi ukiwa mahabusu/mtuhumiwa we unachukuliwa kuwa tayari ni MHALIFU kwahiyo vipigo, vichura, nk vinakuhusu. Na hata ikija kubainika haukuwa mhalifu, hakuna hata ataekuomba msamaha na huna cha kufanya!
 
Nchi za kiafrica ile dhana ya 'innocent until proven guilty' huwa haipo kabisa.

Kinachosikitisha zaidi ni baadhi ya watu ku comment kwa kebehi kuhusiana na hao mahabusu.

Inawezekana kuwatakia magari yenye ac ni a bit far fetched kwa uhalisia wa nchi zetu ila kuwa treat vizuri tu mahabusu kulipaswa kuwa ni kipaumbele.

Kuwa mahabusu hakumaanishi una hatia sasa mtu akianza kuchezea virungu kipindi cha mahabusu na kesho mahakama imkute hana hatia hapo si itakuwa mtu kapewa adhabu bila sababu.

Neno la ushauri, ikiwa hujawahi lala mahabusu mshukuru Muumba wako na endelea kumuomba usifike huko. Rumande haina mwenyewe, sio kila alie rumande ni muhaini.
 
Hao vibaka acha wasafirishwe hivyo tena mbona wanapendelewa kabisa hzo walitakiwa waburuzwe na minyororo huku ikiwa imefungwa kwenye Gari hata kama bado hawajahukumiwa
 
Alipo ondoka mkoloni Mweupe na kumuacha mkoloni mweusi,hali ilitegemewa kuwa nzuri zaidi lakini mwisho hali ikawa mbaya zaidi.
Kitendo cha kujisaidia kwenye ndoo ni ishara ya kuto kutostarabika kwa mtu mweusi.
 
Kiufupi hayo mambo yalianzishwa makusudi ili kudhibiti uhalifu kwa kuwajengea hofu raia, hakuna anayependa kufikia hali hiyo. Ndio maana unapaswa kutii sheria na mamlaka za nchi kwa kuwa raia mwema.
Usha ambiwa mtuhumiwa huyo sio prisoner na hata prisoner anapaswa kuishi kwenye mazingira mazuri,shida yenu watu weusi ni upumbavu.
 
Vitu vingine sijui ni kutojua kweli!!!
Mbona hukuuliza kwa nini wanajeshi wanapokuwa mafunzoni hawaachwi na nywele zao? Au wanaamshwa usiku?
Kabla hujaanza kutetea ujinga,ungeuliza kwanza huko walipo wanafanyapo nini.
Kesho utauliza mbona wenye familia zao hawapewi nafasi ya kubanjuana na wenza wao!
Sawa,si kwamba wote wana makosa,wengine wanaonewa. Nani wa kuwachambua? Alieuwa nae atafutiwe gari zuri akae vizuri!
 
Mbona hukuuliza kwa nini wanajeshi wanapokuwa mafunzoni hawaachwi na nywele zao? Au wanaamshwa usiku?
Hivi umeelewa msingi wa mada hii? Sababu ya wanajeshi kukata nywele zao wawapo mafunzoni mbona iko wazi kabisa na haihitaji mjadala??

Huyu mahabusu anasafirishwa kama gunia la mahindi kwasabb gani?
 
Hivi umeelewa msingi wa mada hii? Sababu ya wanajeshi kukata nywele zao wawapo mafunzoni mbona iko wazi kabisa na haihitaji mjadala??

Huyu mahabusu anasafirishwa kama gunia la mahindi kwasabb gani?
Ukishaambiwa wewe ni mahabusu ni mwendo wa kutii amri tu hii ni Africa
 
Hao vibaka acha wasafirishwe hivyo tena mbona wanapendelewa kabisa hzo walitakiwa waburuzwe na minyororo huku ikiwa imefungwa kwenye Gari hata kama bado hawajahukumiwa
Ila unatambua kuwa kuna uwezekano hata wewe ukawa mahabusu tena bila ya hatia? Ungependa uburuzwe na minyororo pia??

Mahabusu haina mmoja ndugu na sio kila unaemuona huko anapaswa kuwa huko.
 
Back
Top Bottom