Sioni sababu ya kuwasafirisha mahabusu kwa namna inayofanyika hivi sasa. Mahabusu wanasafirishwa na magari ya polisi huku wakiwa wamechuchumaa.
Kwann lisitafutwe gari ama minibus zuri lenye AC wakaketi wote na kupewa magazeti wayasome wakati wakielekea mahakamani?
Hatuoni kuwa kama taifa tunafanya makosa yale yale wanayoshitakiwa mahabusu, (ya kuzikanyaga haki za wengine)?
Kwahiyo tumeamua kuwa taifa la kutafuta haki kwa kuzikanyqga haki za mahabusu ??
View attachment 3088487
View attachment 3088488Picha: Watuhumiwa wa ubakaji wakipandishwa kwenye gari la polisi
Sasa hapo wanasafirishwa! Ungeingia kwenye vyumba wanamo hifadhiwa, si ndiyo ungechoka kabisa! Mahubusu/jela ukiingia na afya yako mgogoro, unaweza kujikuta umekata moto.
Wewe ungefurahi kama ukisafirishwa hivyo na uelewe mahabusu bado ajapewa hukumu hapo maana anaweza kutwa hana hatia.Nadhani ni katika hali ya kuwadhibiti wasitoroke
Kuna watu wana kesi mbaya ukiamua kuwasafirisha kama watalii wakarudi mtaani hali itakuwa mbaya.
Wako chini ya ulinzi laZima wadhibitiwe.
Ukiwa mahabusu utafungwa pingu, kuchuchumaa n.k kikubwa tukutane na vyombo vya haki ndo vitaamua hatima yako
Ili wajutie mambo waliyoyafanya,hata wewe au mimi ikibainika nimefanya upuuzi fulani ni haki kupitia hicho wanachofanyiwa,Bado kujisaidia kwenye ndoo.
Nani wa kuwasemea?
Kila mtu anadhani haimhusu Hadi yamkute.
Huyo ni mahabusu, bado hajahukumiwa. Je, akikutwa hana hatia, na amesingiziwa, hautakuwa uonevu huo aliofanyiwa?Ili wajutie mambo waliyoyafanya,hata wewe au mimi ikibainika nimefanya upuuzi fulani ni haki kupitia hicho wanachofanyiwa,
Au mkuu unadhani wameonewa ?
Sio kila mahabusu ana hatia. Hao sio wafungwa bado. Wakihukumiwa kwa haki, labda ndio wasitetewe. Lakini kwenye hali ya umahabusu, ni kuwa wanatuhumiwa tu. Hata wewe unaweza bambikizwa kesi, na kabla ya kuchomoka, utakuwa umepita hiyo hali ya umahabusu. Ni vizuri mahubusu waheshimiwe tu kama raia.Ili wajutie mambo waliyoyafanya,hata wewe au mimi ikibainika nimefanya upuuzi fulani ni haki kupitia hicho wanachofanyiwa,
Au mkuu unadhani wameonewa ?
Ni kweli hayupo wa kuwasemea, licha ya unafki hofu ile ile bado ipoNi kwa sababu hayupo wa kuwasemea.
Tumejawa ubinafsi tukidhani umahabusu hautuhusu.
Laiti tungalijua sote tu mahabusu watarajiwa.
Nilifanya kazi kwenye halmashaur moja Tanzania. Nilikuwa nafanya kazi za ukimwi. Palikiwq na gereza moja la wanaume. Kilichonishangaza robobtatu walikuwa wameathirika hili liliniumixa sana sikujua kwqnn mana sikuwa na room ya kuwahojiSasa hapo wanasafirishwa! Ungeingia kwenye vyumba wanamo hifadhiwa, si ndiyo ungechoka kabisa! Mahubusu/jela ukiingia na afya yako mgogoro, unaweza kujikuta umekata moto.
Ndo Kwa kipindi yupo chini ya ulinzi hawezi kwenda mahakamani kama mtaliiSio kila mahabusu ana hatia. Hao sio wafungwa bado. Wakihukumiwa kwa haki, labda ndio wasitetewe. Lakini kwenye hali ya umahabusu, ni kuwa wanatuhumiwa tu. Hata wewe unaweza bambikizwa kesi, na kabla ya kuchomoka, utakuwa umepita hiyo hali ya umahabusu. Ni vizuri mahubusu waheshimiwe tu kama raia.
Nilitaka tu kuweka msisitizo kwamba mahabusu wasisafirishwe kama wanyama. Kuwepo na utu kiasi.Sexless uko bar gani muda huu?
Hebu rudia Tena hapo kwenye minibus yenye AC na kupewa magazeti.
Hivi watu hua mnawaza Nini? Vituo vya polisi havina ac halafu watuhumiwa wasafirishwe kwenye gari lenye AC.