Kwanini MAISHA ya sasa yamepoteza ladha tofauti na zamani

Hata kachumbari ikikatwa ilikua inanukia tofauti yani ukikaa pembeni lazma mate yajae mdomoni, lakini sahivi waaapi.....

Ukila huo ubwabwa unabaki na kazi ya kuwanusisha watu mikono tu kwa ushahidi, ila sahivi wala mikono hainukii tena
Nimeanza kuamini wewe ni muhenga tena pengine ata ni age ya mama yangu 😂
 
Hii ladha ya maisha ambayo sisi tunaanza kuionja uku Tanzania ni ladha ambayo nchi ya magharibi tangu kitambo wanadunda nayo
 
Hata kachumbari ikikatwa ilikua inanukia tofauti yani ukikaa pembeni lazma mate yajae mdomoni, lakini sahivi waaapi.....

Ukila huo ubwabwa unabaki na kazi ya kuwanusisha watu mikono tu kwa ushahidi, ila sahivi wala mikono hainukii tena
Ilikuwa zikiokwa sikonsi kwenye jiko la mkaa zinanukia balaa,bi mkubwa akimaliza kukata madonge anayafunika mnaweka juani yaumuke🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Sio kwa wote , mbona mimi naona maisha ni matamu sana ? Ukiweka thamani yako ipimwe kwa vitu lazima maisha utayaona mabaya tu
Mkuu,
Maisha yapo virtual sana, muda wako mwingi unawasiliana na watu huenda hata hujawahi kuwaona.
Back in the days, mnakutana, mnafurahi kama ndugu/marafiki, upendo uikuwa wa kweli.
Leo hata ukikutana na watu wako, dk5 kila mtu yupo busy na "watu wengine" kabisa!!
 
Inaanza na wewe mwenyewe halafu inafuata ni aina gani ya watu wanakuzunguka ama unawaita wa karibu kwako.
 
umeongea bonge la point
 
Kuna ule ubwabwa maharage wa hapo miaka ya tisini na kitu, ukipikwa nyumbani mtaa mzima unanukia, siku ukiwekwa na nazi ndio balaa.

Ni kweli kabisa ladha zimepotea katika kila kitu.
Mchele ulikua haupatikani kwa wingi hivo kula wali ni mara mojamoja, sasa saivi wali unaliwa kila siku, utaupendaje sasa
 
Watu wanamiliki kila kitu Ila hawana furaha , wapo na Psychomotor impairment
Ukweli ndio huo, maisha tuliyoishi kwa sisi tuliokua watoto miaka ya 90 mwanzon na vijana miaka ya elfu mbili mwanzon, ki ukwel huwa nayamiss sana yale maisha, tulivyoish na ndugu, wakubwa walotuzidi kiumri, mziki, maisha ya kuthaminiana, ushrikiano! Ki ukwel ni maisha ambayo binafs huwa nayamiss
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…