Kwanini Majaji wanaapa mbele ya Rais na sio Jaji Mkuu?

Kenya wenzetu wameondokana na hizi teuzi kwa kiasi kikubwa sana!
Nafasi nyingi hutangazwa kisha watu huomba!
Nafasi kama IGP n.k wanafanya kuomba na usaili wa wazi kufanyika kumpata anaestahili!
Wenzetu walishaona mapungufu makubwa yaliyopo kwenye teuzi wakaamua kuondokana nazo !


Sent using Jamii Forums mobile app
 
leo TUNAJIFANANISHA NA WALE TUNAOWAITA MABEBERU.
baniani mbaya.kiatu chake dawa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rais ndie huteua Majaji,Majaji hawateuliwi Na Jaji Mkuu huteuliwa Na Rais

Hivyo ni sahihi Rais kuwaapisha kwa Kuwa Yeye ndie kawateua!
Labda tuhoji Kwanini Majaji wa Mahakama kuu Na ya Rufaa huteuliwa Na Rais badala ya Jaji Mkuu kwa kushauriwa Na Mamlaka husika?

Haiingi akilini Jaji Mkuu kuapisha Mtu ambae hajamteua
Kwa RC kumuapisha DC anafanya hivyo kwa Kuwa amekasimiwa hayo majukumu ya Mkoa Na Rais Mwenyewe kwa hiyo anawaapisha ma DC kwa niaba ya Rais

Hata Kwenye Majeshi ngazi Za Juu Za Maafisa wanadhimu wa Majeshi wanateuliwa Na kuapishwa Na Rais sio Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi

Rais wa Nchi Ana kofia Mbili Za Ngazi ya Utawala

1) Mkuu wa Serikali ( Head of Executive)
2) Mkuu wa Dola ( Head of state)

Akiteua Mkurugenzi wa Halmshauri Au WaZiri hapo inakuwa Kama Mkuu wa Serikal

Lakin akiteua Jaji Mkuu Au Katibu wa Bunge hapo anafanya kazi Kama Mkuu wa Dola ( Head of state)

Head of state maana yake Ana simamia Nchi Na mihimili yake yote mitatu ndio sababu ana Mamlaka ya Kuvunja Bunge Na Hata kufukuza Jaji Mkuu japo kwa Jaji kumewekwa Urasimu kidogo ili kutofautisha Na wateule wengine
 

Kaimu Jaji Mkuu atamuapisha Rais wa Jamhuri then Rais wa Jamhuri anaweza kumthibitisha Jaji Mkuu au kuteua Mwingine kwa nafasi hiyo
 
Asante mkuu
 
Hapo hata mimi sielewi.Jaji anaapishwa na Rais wakati huohuo Rais akishachaguliwa anaapishwa na jaji hivi hii imekaaje.wataalam tupeni taaluma zenu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio hapo watu waelewe,sio hizi kelele za mihimili sijui upuuzi gani huko.
 
Ama kweli Roma ina nguvu sna aisee japo nnatoka nje ya mada lakini hawa majaji kuvaa kama mapadri wa kiroma au wasaidizi wao ndo imenifanya nianze kulichukulia tofauti kabisa hili kanisa la Roma

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kenya ukilinganisha
Kenya hawana demokrasia komavu kama Marekani.
Ni kweli mfumo wao wa sasa Jaji mkuu anaomba kazi na kupitia katika mikono ya usaili toka kwa manguli wa sheria. Pamoja na hayo, bado mfumo huo una mapungufu mengi hasa ukikuta Jaji Mkuu ana msimamo mkali ambao hauzingatii matakwa ya maslahi mapana ya Taifa.
Fikiria kitendo cha mahakama kufuta uchaguzi mkuu wa Kenya mwaka jana. Hakuna anaepinga gharama za demokrasia na utawala wa sheria. Mwisho wa siku uchaguzi umerudiwa na fedha nyingi zimetumika, na alieshinda ni yule yule Uhuru Kenyatta.

Fedha zile zingeweza kufanya miradi ya kugusa wananchi moja kwa moja kama vile maji, huduma ya afya, mikopo inayoibua ajira endelevu kwa vijana na mambo kama hayo
 
Hapo hata mimi sielewi.Jaji anaapishwa na Rais wakati huohuo Rais akishachaguliwa anaapishwa na jaji hivi hii imekaaje.wataalam tupeni taaluma zenu

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii ni takwa la kisheria na katiba.
Katiba imeainisha wazi kuwa Rais akichakuchaguliwa na wananchi na matokeo kutangazwa na Tume ya Taifa ya uchaguzi, Rais atakula kiapo mbele ya jaji mkuu.
Hata Marekani ambao ni magwiji wa Kidemokrasia, Rais wao nae anakula kiapo mbele ya Jaji Mkuu.

Katiba iko online. Unaweza kui-download na soma Ibara ya 42, kifungu cha kwanza mpaka cha tano kuna maeliezo mazuri ya kujibu hoja yako
 
Ni katiba ndo inasema hivyo.

Halafu kusema kuna mihimili mitatu naona ni geresha tu. Mi naona kuna mhimili mmoja (serikali) na matawi yake mawili (mahakama na bunge)
 
Eti mihimili mitatu. hapa kwetu hiyo ni geresha tu. watu ni wezi wanaogopa siku hiyo mihimili ikifanya kazi yake vyema watu wataumbuka. tunapelekana hivyo hivyo siku zinaenda. Haki haiwezi kutendeka kwa katiba tuliyo nayo
 
Na nani anamwapisha Rais? Jibu ni Jaji Mkuu. Kwa hiyo ngoma sawa
 
Kwa maelezo yako hayo yanadhihirisha kuwa rais wa nchi ndiye bosi wa majaji wote, na hivyo akiwapa maelekezo bila shaka watatumia kila wawezalo ili kuyatekeleza. Na hapo ndipo watu wanatia shaka ya kweli kabisa juu ya uhuru wa mahakama zetu hasa pale kesi itakapokuwa inayagusa maslahi ya utawala.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…