Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 9,397
- 12,415
Yesu Kristo - Mbabe wa mapepo, majini, wachawi na roho wabaya wote
"Na pepo waliokuwa waovu walipomwona, walianguka mbele yake, wakapiga kelele wakisema, Wewe u Mwana wa Mungu!" Luka 4:41
Katika ulimwengu wa kiroho, kuna vita visivyoonekana vinavyopiganwa kila siku kati ya nuru na giza. Mapepo na maroho mabaya hutafuta kuharibu maisha ya watu, lakini tunayo habari njema Yesu Kristo ndiye Mbabe wa mapepo na maroho yote mabaya.
Yesu Kristo si wa kawaida. Alikuwepo kabla ya mwanzo wa dunia, akiishi pamoja na Mungu Baba Mbinguni. Mapepo yanamjua tangu enzi hizo, na yanatetemeka mbele yake kwa sababu ya mamlaka aliyo nayo. Katika huduma yake duniani, Yesu alikutana na watu walioteswa na mapepo, lakini kwa neno moja tu, aliwatoa huru.
Katika Marko 5, "Yesu alikabiliana na mtu aliyekuwa na jeshi la mapepo. Walimtambua na kumwomba asiwaangamize. Hili linaonesha wazi kuwa Yesu ana mamlaka kuu juu ya kila roho chafu".
1. Chanzo cha Mapepo, Wachawi, Majini na Roho Wabaya
Kabla ya gharika ya Nuhu, dunia iliharibiwa kwa kiwango kikubwa na viumbe wa ajabu waliotokana na uasi wa malaika waliokosa utiifu kwa Mungu. Hawa malaika walijulikana kama The Watchers (walinzi), waliotumwa kuilinda dunia, lakini walivutwa na uzuri wa wanawake wa kibinadamu. Walimuasi Mungu, wakashuka duniani na kuoa wake:
“Na malaika, wana wa mbinguni, walipoona binti za wanadamu kwamba ni warembo, wakajisemezana: ‘Na tujitwalie wake miongoni mwao.’”
Henoko 3:2
Malaika hawa, wakiongozwa na Semjaza, walikuwa 200 kwa jumla. Walishuka juu ya Mlima Hermoni (Henoko 3:5), na kwa kujamiiana na wanawake wa kibinadamu, walizaa watoto wa ajabu majitu (Nephilim) ambao walikuwa na nguvu nyingi, wakawa watenda maovu duniani.
Majitu hawa waliwageukia wanadamu, wakaanza kuwala, kunywa damu yao, na kufanya dhambi dhidi ya viumbe vyote. Uchafu huu ulienea kwa kasi kubwa.
“Na walipozaliwa majitu, wakaanza kula wanadamu… wakatenda dhambi dhidi ya ndege, wanyama, samaki… wakanywa damu.” Henoko 3:9–10
Wakati huo huo, malaika waliowashuka duniani waliwafundisha wanadamu elimu na ujuzi mbalimbali.
i. Azazel, Mwalimu wa Vifaa vya Vita na Mapambo ya Anasa
“Azazel aliwafundisha kutengeneza mapanga, mikuki, mapambo ya macho…”
Azazel alifundisha wanadamu kutengeneza silaha za vita kama mapanga na mikuki. Hii ilisababisha mwanadamu kuwa mkatili, muuaji, na mwenye kushindana kwa nguvu. Pia, alifundisha matumizi ya mapambo ya macho (make-up), vitu vya kupendeza ambavyo vilizua tamaa, uasherati na upotovu wa maadili. Hii ilikuwa njia ya kupotosha mwanadamu aishi kwa tamaa ya mwili badala ya hofu ya Mungu.
ii. Semjaza Mwalimu wa Uchawi na Mafumbo
“Semjaza alifundisha uchawi…”
Semjaza, akiwa kiongozi wa malaika hao waasi, alitoa elimu ya uchawi, ulozi, na ramli vitu vilivyoleta uhusiano wa moja kwa moja kati ya wanadamu na ulimwengu wa mapepo. Uchawi huu ulikuwa na lengo la kuwapa wanadamu uwezo wa kupenya ulimwengu wa kiroho kwa njia za kinyume na mapenzi ya Mungu. Kwa hiyo, Semjaza alijenga daraja la mawasiliano kati ya wanadamu na roho waovu.
iii. Kokabel, Mwalimu wa Nyota (Astrology)
“Kokabel alifundisha nyota…"
Kokabel alifunua elimu ya astrology (utabiri wa nyota), ambayo leo imegeuka kuwa imani ya kuamini majaliwa ya mtu yanategemea nyota. Badala ya kumtegemea Mungu, watu waliambiwa waangazie nyota kujua mustakabali wao. Hili lilikuwa ni aina ya ibada ya sanamu iliyofichika chini ya "sayansi," na bado linaendelea hata leo katika mfumo wa horoscopes, zodiac signs, na mengine.
iv. Sariel, Mwalimu wa Mizunguko ya Mwezi
“Sariel aliwafundisha mienendo ya mwezi.”
Sariel alifundisha siri za mizunguko ya mwezi, ambayo ilihusiana na kalenda za kishetani, majira ya tambiko, na ibada za mwezi. Mafundisho haya yalitumika kupanga siku za kafara, laana, matambiko, na hata uchawi wa hedhi kwa wanawake. Leo hii, bado kuna wachawi wanaotumia kalenda ya mwezi kufanya kazi zao za giza.” Henoko 3:11–13
Kwa hiyo, chanzo cha uchawi, mapepo, majini, na mafundisho ya kipepo kilianzia hapa kwa malaika waasi waliowaingiza wanadamu kwenye giza la kiroho.
2. Jinsi Mapepo Walivyozaliwa: Roho za Nephilim
Mungu alipoona uharibifu huo, aliingilia kati na kuamuru kwamba majitu yale (Nephilim) yauwawe. Miili yao ikaangamizwa, lakini roho zao hazikurudi kwa Mungu wala hazikuingia kuzimu. Roho hizo zilibaki duniani kama mapepo (roho wachafu).
“Na sasa roho za majitu… kwa kuwa walizaliwa na watu na malaika, wataitwa roho za uovu juu ya dunia… Roho hizi zitabaki duniani na kuitesa wanadamu.” Henoko 15:8–10
Roho hizi:
Hazina makao ya kudumu, na hutangatanga.
Zinatesa, zinaingia ndani ya wanadamu, na hutumia uchawi kuwafunga watu.
Zinachukia wanadamu kwa sababu wao si wa Mungu, bali wa laana.
Yesu alizungumzia hali hii aliposema:
“Pepo mchafu akitoka kwa mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika…” Mathayo 12:43
Kwa hivyo, mapepo ni roho za watoto wa uasi wa malaika, si malaika wenyewe wala mashetani wa moja kwa moja. Lakini zina chuki, nguvu, na uovu wa hali ya juu kwa sababu ya asili yao haramu.
3. Kwa Nini Mapepo Humwogopa Yesu Kristo?
Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu aliyeumbwa tangu milele. Malaika wote, kabla ya kuasi, walimwabudu Yeye akiwa na utukufu wake wa mbinguni. Malaika waasi na roho za Nephilim wanamjua Yesu, si kwa kusikia, bali kwa kumwona na kuishi naye mbinguni kabla ya kuasi.
“Katika mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwa kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu… Vyote viliumbwa kwa huyo.” Yohana 1:1–3
Ndiyo maana, wakati Yesu alipokuja duniani katika mwili wa kibinadamu, mapepo yalimsujudia kwa hofu kubwa:
“Na pepo waliokuwa waovu walipomwona, walianguka mbele yake, wakapiga kelele wakisema, ‘Wewe u Mwana wa Mungu!’” Luka 4:41
“Je! Umekuja kututesa kabla ya wakati?” Mathayo 8:29
Mapepo yalijua Yesu ndiye atakayeleta hukumu ya mwisho, kama ilivyotabiriwa katika Henoko:
“Na Samlazaz na wenzake wafungwe kwa vizazi sabini chini ya ardhi hadi siku ya hukumu ya milele.” Henoko 4:13
Kwa hiyo, mapepo, majini, wachawi na roho wa uovu wanaogopa mamlaka ya Yesu Kristo, maana wanajua mwisho wao umo mikononi mwake.
4. Jina la Yesu Kristo Silaha ya Kushinda Giza
Nguvu ya kipekee ya kumshinda shetani na mapepo iko katika jina la Yesu Kristo. Jina hilo lina mamlaka mbinguni, duniani, na kuzimu:
“Kwa hiyo Mungu alimwadhimisha mno, akampa jina lipitalo kila jina; ili kwa jina la Yesu, kila goti lipigwe, la mbinguni, la duniani, na la chini ya dunia.” Wafilipi 2:9–10
Yesu mwenyewe alisema:
“Tazama, nimewapa mamlaka ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu juu ya adui zote, wala hakuna kitakachowadhuru.” Luka 10:19
Katika huduma yake:
Yesu alifukuza mapepo kwa neno moja tu (Marko 1:25).
Alifungua waliofungwa na wachawi (Luka 13:11–13).
Aliwapa wanafunzi wake mamlaka ya kufukuza mapepo (Marko 16:17).
“Kwa maana hakuna jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo. Matendo 4:12
Hivyo Yesu Kristo ndiye Mshindi wa giza lote. Roho za uovu mapepo, majini, wachawi, mizimu, na mashetani zote zinaogopa jina lake, kwa sababu:
Zinajua mamlaka yake ya milele.
Zinajua alishinda msalabani.
Zinajua atawaharibu milele.
Kwa hiyo, mtu yeyote aliye ndani ya Kristo hana sababu ya kuogopa giza, maana tunaye Bwana ambaye jina lake linatikisa ulimwengu wa kiroho.