Rais analizwa na maisha ya Rais mstaafu
Rais anamnunulia BENZI la dollar 187,000 Rais mstaafu.?
Wakati huo mwanae akiwa Rais wa Zanzibar.
Rais anahailisha mechi inayofatiliwa na watu zaidi ya million 200+ Africa kwa sababu ya kitabu cha maisha ya mtu ambaye hana tena msaada tena kwa nchi.
Rais anampa nyumba Rais aliyekaa madarakani na kuchuma pesa ndefu sana ndani ya utawala wake zikiwemo kashifa kibao za wizi wa pesa za umma kama Richmond, Escrow, Dowans na kashifa ya bomba gesi kutoka mtwara.
Rais anaagiza Rais aliyefariki madarakani stahiki zake ziwaishwe
Wakati huo bado watoto wetu wanakaa chini
Madawa hakuna kwenye zahanati
Vyumba vya madarasa havitoshi
Walimu hawatoshi
Nyumba za walimu hakuna
Madakitari na manesi hawatoshi
Barabara nyingi bado hazipitiki
Huduma ya maji na umeme bado duni
Hakika nawaambia ccm hii laana itawatafuna kwa miaka mingi ijayo Baba wa taifa na familia yake ndiye alitakiwa kuenziwa kwa vitendo maana yeye hakuiba pesa kama waliomfuata.
Kama nchi tumepotea.