Kwanini Marais wastaafu? Ni upendeleo?

Kwanini Marais wastaafu? Ni upendeleo?

Watoto wa juzi hawa 2003 hawawezi kuelewa hussle za washua enzi za unga wa Yanga!🤓🤓🤓
Kipindi kile hakuna viatu, nguo mpya bali kilaka kipya, hakuna cha dela bali kaniki, sukari gulu, sabuni za mipapai, nguo za mitumba ni dili za misaada kutoka kwa missionaries,kupiga simu hadi usafiri kwenda Posta wakati mwingine mtandao hakuna.
Mzee Mwinyi ndiye aliyetufanya tuanze kuvaa viatu na kubadilisha nguo za material mbalimbali.
 
Shida inaanza pale uamuzi wa jambo fulani lenye kutumia fedha ya serikali unaamuliwa tu na mtu kwa kadiri anavyojisikia nafsini mwake...

Ungewekwa tu utaratibu kwamba, wastaafu wa ngazi fulani wakiomaliza utumishi wao watatunukiwa nyumba au magari n.k.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
tumwombee marehemu apumzike.

alitabiri tutamkumbuka akidhani itachukua miaka kadhaa,ila dalili zinavyoonyesha hata miezi 5 inaweza isiishe[emoji23][emoji23][emoji23].

kwakweli sipendi mama akosee,naumia mnoo,lakini ndio upande aliouchagua.nabaki naumia tu.
Tatizo anataka kujifanya analifurahisha hili genge la mitandaoni hapo ndio atafeli
 
Kipindi kile hakuna viatu, nguo mpya bali kilaka kipya, hakuna cha dela bali kaniki, sukari gulu, sabuni za mipapai, nguo za mitumba ni dili za misaada kutoka kwa missionaries,kupiga simu hadi usafiri kwenda Posta wakati mwingine mtandao hakuna.
Mzee Mwinyi ndiye aliyetufanya tuanze kuvaa viatu na kubadilisha nguo za material mbalimbali.
Halafu kuna makoro wanamuona kama
mzee Pimbi flani! Watu walipitia hussle ngumu kuliko hii aliotupitisha Jiwe!
 
Nashukuru nimeshuhudia nikiwa na akili zangu timamu kipindi Cha mwisho Cha mkapa, kipindi chote Cha kikwete, kipindi Cha magufuli, na kipindi hiki Cha Samia.

Katika vipindi vyote vya uongozi wa hao ndugu hakujawahi kukosekana ukosoaji kutoka kwa wananchi.

Nashukuru pia Mimi nimejiweka pepeni kwenye ukosoaji maana hakuta kuja kwa na kiongozi mwenye kuwawaridhisha wote katika yote ayafanyayo.

Badala yake nimekua nikiangalia kila kifanyikacho kwa jicho la kuto kukosoa ili amani ya moyo indelee kuwepo kwa kiongozi wangu.

Poleni mno wanaharakati .

From the pen of Martin Luther King, Jr.

1. An individual who won't die for something is not fit to live.

2. A nation or civilization that continues to produce soft-minded people purchases its own death on the installment plan.

3. We will have to repent in this generation not merely for the vitriolic words and actions of the bad people, but for the appalling silence of the good people.

4. History will have to record that the greatest tragedy of this period of social transition was not the strident clamor of the bad people, but the appalling silence of the good people.

5. The ultimate tragedy is not the oppression and cruelty by the bad people but the silence over that by the good people.

6. The hottest place in Hell is reserved for those who remain neutral in times of great moral conflict.

7.
 
Unaumia kiukweli au ni wivu tu kwa Mzee Mwinyi kununuliwa zawadi ya Benzi ambalo pengine huna na hutokaa ulipate.
Nilichogundua ni kuwa % kubwa ya Watanzania wamejaa wivu na unafiki wa kijinga.

Sorry just kidding [emoji16][emoji16][emoji16][emoji23][emoji23]
namuonea wivu mzee mwinyi!!![emoji1787][emoji1787].

unaandika hata vitu huvijui,vivu huoneana watu wanaoendana status ya maisha.yaani wa kumwonea wivu mzee mwinyi ni rais au kiongozi mwenzie mstaafu sio mimi.

tataizo lenu wazaramo kila kitu mnakiweka kiswahili swahili tu.
 
Mie Naona kosa la Mama ni 'timing'. Maneno yake wiki iliyopita na matendo yake siku hizi mbili yanakinzana.
 
Rais analizwa na maisha ya Rais mstaafu

Rais anamnunulia BENZI la dollar 187,000 Rais mstaafu.?

Wakati huo mwanae akiwa Rais wa Zanzibar.

Rais anahailisha mechi inayofatiliwa na watu zaidi ya million 200+ Africa kwa sababu ya kitabu cha maisha yake. Maana yake unajali MTU kuliko watu.

Rais anampa nyumba Rais aliyekaa madarakani na kuchuma pesa ndefu sana ndani ya utawala wake zikiwemo kashifa kibao za wizi wa pesa za umma kama Richmond, Escrow, Dowans na kashifa ya bomba gesi kutoka mtwara.

Rais anaagiza Rais aliyefariki madarakani stahiki zake ziwaishwe

Vipi stahiki ya watumishi wengine ambao wamefanya kazi kwa uaminifu na uzalendo lakini mpaka leo wanakanyaga mpaka sole za viatu zinaisha wakifatilia mafao NSSF.

Wakati huo bado watoto wetu wanakaa chini

Madawa hakuna kwenye zahanati

Vyumba vya madarasa havitoshi

Walimu hawatoshi

Nyumba za walimu hakuna

Madakitari na manesi hawatoshi

Barabara nyingi bado hazipitiki

Huduma ya maji na umeme bado duni

Hakika nawaambia ccm hii laana itawatafuna kwa miaka mingi ijayo Baba wa taifa na familia yake ndiye alitakiwa kuenziwa kwa vitendo maana yeye hakuiba pesa kama waliomfuata.

Kama nchi tumepotea.
Wivu tu
 
Halafu kuna makoro wanamuona kama
mzee Pimbi flani! Watu walipitia hussle ngumu kuliko hii aliotupitisha Jiwe!
Kabisa Mkuu.
Wazee wetu walihussle bya hatari tena ukizingatie enzi zile za Mwalimu akipambana na vuguvugu za Ukombozi,vita vya Kagera na Harakati za Kupambana na Ubepari...
 
Ila watanzania sisi dah kiuhalisia hatueleweki tunasimama na kipi suala la CAG lilikuja na mambo makubwa zaidi ya hili la BENZ ila ndio hivyo lishapita, anyways tuendelee kulima mahindi mpaka umefunguliwa.
 
namuonea wivu mzee mwinyi!!![emoji1787][emoji1787].

unaandika hata vitu huvijui,vivu huoneana watu wanaoendana status ya maisha.yaani wa kumwonea wivu mzee mwinyi ni rais au kiongozi mwenzie mstaafu sio mimi.

tataizo lenu wazaramo kila kitu mnakiweka kiswahili swahili tu.
Nakutania tu rafiki...
Ni kweli sisi bado vijana tuna nguvu na akili za kusaka mali,ebu tusiichokonoe zawadi hiyo hata kama haikuwa na utaratibu tunaodhani haukuwa sawa.
Mzee Mwinyi ndiye aliyeiingiza nchi yetu katika Dunia ya leo ya utandawazi kiasi ya mimi na wewe kujibizana leo bila kuonana. 😂😂😂🌉🏢🔰🎮
 
Kila level ya utumishi wa umma ina mafao na pensheni zake.
Labda ebu tuwekee hizo titles za watumishi unaosema walifanya kazi kwa uaminifu ili tuone na wao wanastahiki zipi unazotaka ziwe...!!?
Stahiki za watumishi wengine ni pamoja na zile 50% lupmsum ambazo ******** alizozibadili akiwa amelala kitandani kwake kapunguza hadi 25%

Malalamiko haya ya watumishi mpaka leo hayajapata wa kuyatatua bado mpango wa mapunjo ya kuwalipa 25% upo.

Na ni kwa sababu raisi alikomba stahiki hizi kwa jenzi za mabarabara ni dharau ilioje

Kwa nini na wao za kwao wasiziondoe wazipangie matumizi mengine.

Kiufupi viongozi hawaakisi wanayowatendea watumishi wengine.
Ni wapumbav sana
 
..Sheria ya mafao ya viongozi wakuu wastaafu ilipitishwa na BUNGE wakati Dr.Salim Ahmed Salim ni Waziri Mkuu.

..Na ilielekezwa kwamba sheria hiyo inawatambua viongozi wakuu wastaafu waliotumikia kabla na baada ya sheria kutungwa.

..Sasa kuna wazo limenijia. Je, Alhaj Aboud Jumbe Mwinyi ambaye alikuwa Makamu wa Raisi wa JMT alipewa mafao yake kwa mujibu wa sheria hii?

..Naomba majibu toka kwa wenye uelewa wa historia yetu.

Cc Pohamba, Nguruvi3, Mohamed Said
 
Haaaa haaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa haaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Utaratibu wa kuhakikisha tunawajali marais wastaafu unapunguza pressure za kuwafanya
'wajijali wenyewe wanapokuwa madarakani'
Kuna watu hawajui kuwa kila kitu kina gharama. La muhimu ni kuangalia kipi kina gharama zaidi.

Watu hawajui gharama za kutowajali hawa wastaafu, mtu mmoja amesema vizuri, Mwinyi angeamua angekuwa kama Mobutu, na hakuna kitu tungemfanya. Hizi pesa ni peanuts ukilinganisha na kama wangeamua "kujijengea" future zao wenyewe. Kuna rafiki yangu Mkenya, huwa anacheka tu akisikia kashfa zetu za wizi; anakwambia njoo Kenya ndio utaelewa maana ya wizi.

Kutengeneza mazingira mazuri ya watu kustaafu, hasa hasa huku Afrika ni muhimu. Mtu kama Paul Kagame au Museveni sometimes inawezekana wamechoka lakini option ya kustaafu hakuna, wakiacha kiti hawana uhakika na nini kitawakuta.
 
Wewe huna akili...

Utaratibu wa kuhakikisha tunawajali marais wastaafu unapunguza pressure za kuwafanya
'wajijali wenyewe wanapokuwa madarakani'

Faida yake ni kubwa kuliko unavyofikiri..

Halafu huu utaratibu haukuanzishwa na Samia..
Simu Ile ya msiba Kikwete alisema Magufuli alishamwambia nyumba yake iko tayari
Wanasubiri tarehe ya kumkabidhi..

Kwa yote aliyoyafanya Mwinyi nchi hii
Mpumbavu peke yake ndo anaweza sema
'hana faida tena na nchi'..


Jitu kama wewe lisilo na shukran za sacrifices
Walizofanya watu kama Mzee Ruksa Kwa nchi hii ndo jitu lisilo na faida
Pamoja na yote, hastahili kupewa gari kama zawadi ya birth day. Hapa mama kachemka. Sijui ni nani kamuingiza chaka.

Tungemuelewa wote kama hiyo gari wangempatia kuitumia lakini bado ikiwa ni mali ya serikali.
 
Back
Top Bottom