“Tunasema vijana wajiajiri wakati sisi wenyewe wametuajiri wao, kwanini sisi tusujiajiri kwanza alafu tuone kama kujiajiri ni rahisi ndio tuwaambie nao wajiajiri?”,maneno haya yalisemwa na mbunge mmoja akiwa bungeni wakati wa kuchangia hoja iliyohusu Ukosefu wa ajira.
Ni ukweli usiopingika kwamba mifumo ya elimu inayotumiwa hapa Tanzania ndio inafanya vijana wengi kukosa ajira na kushindwa kujiajiri. Au nani anabisha jamani?
Kwanza kabisa ni kuhusu miaka mingi kijana anayotumia kusoma, unakuta mtoto wa darasa la nne kabebelea madaftari 13 mgongoni eti anaenda shule, alafu mwisho wa siku anakuja kuishia kuyatumia masomo matatu tu huko mbeleni, kwanini masomo yasipunguzwe tangu chini ili mtoto atumie muda ule kufanya stadi zingine kama kujifunza kupika, kulima au ufundi mwingine wowote ambao utakuja kumsaidia hapo baadae?. Haya, matokeo yake anajikuta anatumia takribani miaka 13 kumaliza elimu ya chini ili aingie chuo kikuu, kumbuka muda huo hana stadi yoyote kichwani, anaingia chuo kikuu, anasoma; anamaliza, baada ya hapo hamna kazi, haileti maana kabisa.
Pili, huu mfumo wa elimu tunaotumia ni ule mfumo ulioletwa na wakoloni ili kuwaandaa watu wachache kufanya shughuliza ofisini(white collar jobs), kwa wale wanaokumbuka history vizuri nadhani mnakumbuka ‘characteristics of colonial education’. Elimu hii ilikuwa kwa ajili ya kuandaa watu wachache maana ajira zake zinapatikana kwa uchache lakini hivi sasa nchi nzima tumerundikana kupata elimu ambayo mwisho wake watanufaika wachache na wengine tubaki na umasikini kutokana na ukosefu wa ajira, yaani ni kama tunabeti. Yaani darasa moja badala ya kuwa na wanafunzi 30 linakua na wanafunzi 100 ambao hata mwalimu anapata shida kuwasimamia wote na kujua ni nani ameelewa na ni nani hajaelewa, hapo wanaokuja kumaliza vyuo vema na kupata ajira unakuta ni wanafunzi 10 tu, maanayake ni kwamba wale wanafunzi 0 waliobaki ni muda na rasilimali walikua wanapoteza ambazo endapo wangewekeza muda wao na rasilimali katika kujifunza ufundi na stadi zingine pengine wasingekua wanapata shida.
Mwisho kabisa, serikali haichukui hatua mapema kwenye jambo la msingi kama hili, jambo kama hili linatakiwa litengewe muda maalum wa kutosha ili serikali ilijadili na kupata ufumbuzi mapema kabisa lakini badala yake hili suala linabaki kama hoja za nyongeza bungeni na wanabaki kusema wataboresha kila siku, matokeo yake wanakuja kuboresha baadaya miaka 30 – 40, watu watakaozaliwa mpaka miaka ya 2040 si nao wataendelea kupata shida kama tunayopata sisi?
(Nimeambatanisha picha yenye ujumbe kwa hisani ya tovuti kuu ya serikali)